jkipaji
JF-Expert Member
- Sep 22, 2019
- 5,690
- 7,556
Umekariri sana Elimu ya Makaratasi Kama yule professor wa Kyela,yaani hadi unasahau kua Maisha yanakwenda vizuri zaidi na uhalisia wake!!Maendeleo hayapimwi kwa kuangalia majengo yaliyopo CBD... usinilishe maneno!!
Kwamba eti maendeleo ya haraka haraka, hiyo kauli ni kiroja!!! Hivi huoni aibu kusema eti "nataka maendeleo ya haraka haraka" kwa taifa ambalo lipo huru kwa karibu miaka 60 sasa!!!
Kiroja kingine ni pale unapoleta habari za Jiwe!! Hiyo speed yake ipo kwenye nini?! Kuleta white elephant project kwa kununua ndege kwa billions of dollars?!
Hivi kwa mtu mwenye ufahamu anaweza kulinganisha hata tija ya ujenzi wa UDOM na zile ndege?!
Au unazungumzia speed ya kujenga international airport kijijini kwao na kuhamisha wanyama kutoka mbuga zingine na kuwapeleka Chato?!
Speed ipi hasa unayozungumzia wewe!
Au haya majengo mnayoita hospitali wakati hata madaktari hawaajiri?! Btw, kama kujenga hayo majengo ndo speed kwani ina tofauti gani na shule za kata zilizojengwa nchini mzima hasa ukizingatia program ya shule za kata ndo ile ile iliyoleta ujenzi wa vituo vya afya?!
Speed gani hasa unaisema?! Au speed ya kujenga bwawa la umeme wakati Kusini kuna gas imejaa kibao na hana dira yoyote ya kugeuza gesi ile injini ya uchumi!!!
Hivi unafahamu economic multiplier effect ambayo ingepatikana endapo angeelekeza nguvu kwenye gesi pengine kuliko hata hayo madini aliyoamua kuyajengea ukuta?!!
Unafahamu by-products zinazotokana na gas processing zinavyoweza kuchochea uanzishwaji wa viwanda vingine kama vile vya mbolea na plastic let alone gas yenyewe kutumika kama nishati for domestic use pamoja na umeme?!
Unaweza kueleza additional multiplier effect inayotokana na uwekezaji kwenye bwawa la umeme ambayo haipo kwenye gas exploitation?!
Au unazungumzia SGR mnayodanganywa kwamba inajengwa kwa pesa za ndani wakati deni la taifa (foreign) linaendelea kupanda?!
Hivi ulishawahi kujiuliza ikiwa Kenya yenye uchumi mkubwa hadi kesho SGR yao ni loss making na watu wanaikimbia, what's so special itakachofanya SGR ya Tanzania kuwa economically viable?!
Ulishawahi kujiuliza ni kwanini watu hawatumii TAZARA kusafirisha mizigo to Zambia na bado wanang'ang'ania malori wakati TAZARA na yenyewe ni standard gauge?!
Hicho mtakachofanya na kusababisha transportersz kutumia SGR and nothing else kwanini hamkifanyi upande wa TAZARA?!
Hiyo speed unayoisema wewe ni ipi?!
Au ni speed ni ya ku-deal na middle raking public servants na kuwaacha wezi wakubwa wa nchi hii ambao ni high profile politicians pamoja na top government officials?! Au ni high speed ya kuvuruga private sector?!