Tanzania ya 2008

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Badala ya kuomba msaada watutengenezee Barabara sie tumeona bora tujengewe uwanja wa Taifa

Hii ndiyo hali halisi ya barabara kuu ya KIGOMA,leo ni siku ya tatu kukiwa hakuna kutoka kuelekea mikoa mingine kutokana mvua zisizokoma katika barabara zetu za mfinyanzi.


DSC06074.jpg



MABILIONI yaliyotumika hapa si wangejenga kilometa kadhaa za barabara?


ground.JPG



halafu mnatafuta mchawi ni nani
 
GT- kila jambo na purpose yake, wangetengeneza kilometa kadhaa lakini tatizo lisingekwisha . na wala hiyo haifit katika stratergy ya "prioritization" . mathalani kwa hiyo picha uliyoiweka hapo suppose wasingetengeneza huo uwanja na kutengeneza hicho kipande cha barabara, mtu mwingine angeweza kupiga picha kama hiyo hiyo katika kipande kingene ambacho hakijatengenezwa au katika mikoa mingine.

sasa ni lini tutatengeneza barabara za kutosha ili tuwe na uwezo wa kusema sasa tutengeneze uwanja mzuri na bora?.bila shaka hilo si la miaka 20 au hata 50, sasa kweli tungoje that long mzee?.

no way!. mimi nasema ni vizuri sana serikali ilivyojenga uwaja ule, na pia ni jukumu la serikali kufight in both fronts tuwe na barabara nzuri na viwanja vingine vizuri
 
Badala ya kuomba msaada watutengenezee Barabara sie tumeona bora tujengewe uwanja wa Taifa

Hii ndiyo hali halisi ya barabara kuu ya KIGOMA,leo ni siku ya tatu kukiwa hakuna kutoka kuelekea mikoa mingine kutokana mvua zisizokoma katika barabara zetu za mfinyanzi.


DSC06074.jpg



MABILIONI yaliyotumika hapa si wangejenga kilometa kadhaa za barabara?


ground.JPG



halafu mnatafuta mchawi ni nani

G-T,

Labda wewe ukisema watakusikia.
Unategemea nini kama kipande cha sam nujoma kimechukua miaka kujenga licha kuwepo na business complex pale mlimani! Je ni wapi hawa watafanya the right thing?

Kama Kigoma ingekuwa imeunganishwa vyema na sehemu nyingine za Tanzania, yanayotokea Kenya na hatima yake kwa Uganda, Rwanda, na Burundi (kumbukia ile thread yako ya kufaidika kutokana na yanayotekea kwa jirani) yasingefikia kipimo hiki.

Mkoa wa Kigoma ungetakiwa upewe priority kubwa sana zaidi ya uwanja wa mpira. Haijalishi gamba atatoa mifano mingine kiasi gani. Mkoa wa kigoma unaunganisha nchi zaidi ya 4 ambazo ziko landlocked (kama ukiweka Sudan na zingine zinazofuata huko kwa kufuata ecnon-link theory).

Ni wakati wa kuacha kutafuta wachawi na kudeal na aliyepo saasa hivi - uongozi duni na usio na dira wa serikali ya ccm.
 
Priority setting- how do we carefully use our meagre resources?

1. Ningekuwa mimi... strategically ningetumia raslimali nyingi sana ktk barabara, elimu na afya, na chakula in the 1st 10 years!

2. Then next 10 yrs ningereview progress na kuinvest ktk sector zingine! Uwanja may be kama tungepata mfadhili nigefikiria in the 2nd phase!

3. Nigeziba kapu linalovuja, kuweka nidhamu ya hali ya juu ktk matumizi ya pesa ya serikali na kukusanya kodi kwa nguvu zote. Hizo 133 bil zilizoibwa sii zingejenga km zaidi ya 400 lami toka Dar hadi Moshi?? Hii ni scandali moja tuu..!
 
Informal sector ya uchumi wa kiafrika ambayo inaajiri zaidi ya 60% ya labor force. Na ni hii sector ndiyo inachangia karibia 40% ya GDP. Lakini jamaa wameitelekeza na kukimbilia kuomba wawekezaji kutoka nje. Muwekezaji gani atawekeza sehemu ambayo haina hata barabara? Hasara kubwa sana.
 
eee bwana kweli lakini Kigoma nasikia hauna barabara inayounganisha na sehemu nyingine ya nchi,sasa hapo ndio unakumbuka zile billion 133 zingesaidia almost watu milion 4 kwa miaka kibao na kuwaletea hali nzuri ya maisha kwa kujenga hiyo barabara...lakini cha ajabu mafisadi wataingia 2010 na wananchi wataimba CCM oyeee,Oyee na anayesema ufisadi ziiiiii,ziiiiii then wanachukua kiti kiulaini sana na kwaheri ya kuonana after five yrs..bullshit!
 
Back
Top Bottom