w0rM
Member
- May 3, 2011
- 68
- 164
Katiba ya Tanzania, Ibara ya 41 (6) inasema Mgombea yeyote wa Kiti cha Rais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata Kura Nyingi Zaidi kuliko Mgombea mwingine yeyote
Katiba ya Kenya, Ibara ya 165 (4) inasema Mgombea atatangazwa kuwa Rais Mteule ikiwa atakuwa amepata zaidi ya Nusu ya Kura Zote zilizopigwa katika Uchaguzi na angalau 25% ya kura zilizopigwa katika maeneo mengi
Aidha, Katiba hiyo ya Kenya inasema iwapo hakuna Mgombea aliyechaguliwa Uchaguzi mwingine mpya utaifanyika katika kipindi cha Siku Thelathini (30) baada ya Uchaguzi uliopita
Katika Uchaguzi huo mpya, wagombeaji watakuwa Mgombea au Wagombea waliopata kura nyingi zaidi na Mgombeaji atakayepata idadi kubwa zaidi ya kura atatangazwa kuwa Rais
Katiba ya Uganda, Ibara ya 103 (4) inasema, Mgombea atatangazwa kuwa Rais Mteule ikiwa atakuwa amepata Zaidi ya Asilimia 50 ya kura zote halali zilizopigwa katika Uchaguzi
Lakini pia, Katiba ya Uganda inasema kama mshindi hatapatikana basi ndani ya siku 30 utafanyika uchaguzi mpya na Wagombea waliokuwa na kura nyingi watashiriki. Atakayekuwa na kura nyingi katika Uchaguzi wa Pili atatangazwa kuwa Rais
KUHUSU MSAMAHA WA RAIS
Katiba ya Tanzania, Ibara ya 45 (1), Rais anaweza kutoa msamaha kwa mtu aliyepatikana na hatia Mahakamani kwa kosa lolote, msamaha huo unaweza kuwa na masharti au la kwa mujibu wa sheria
Rais anaweza kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote iwe adhabu tahafifu au kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa ajili ya kosa lolote
Katiba ya Kenya, Ibara ya 172 (1) inasema kutakuwa na Mamlaka ya Msamaha ambao utatekelezwa kwa ombi la Rais wa Taifa kwa mtu yeyeyote kulingana na ushauri wa Kamati ya Ushauri
Rais wa Kenya ataweza kumsamehe mtu aliyepatikana na hatia kwa masharti au la, Kuhahirisha kwa muda fulani maalumu au kwa muda usiojulikana utekelezaji wa adhabu, Kusamehe semu ya adhabu au adhabu yote
Katiba ya Uganda, Ibara ya 121 (1) inasema Kutakuwa na Kamati ya Ushauri ya Utoaji Msamaha itakayokuwa na Mwanasheria Mkuu (Mwenyekiti) na Raia 6 mashuhuri wa Uganda watakaoteuliwa na Rais
Kwa ushauri wa Kamati, Rais anaweza kumpa mtu yeyote aliye na hatia, msamaha wa bure au chini ya masharti halali, Kusamehe semu ya adhabu au adhabu yote, Kurahisisha adhabu kali aliyopewa mtu