Tanzania vs Kenya vs Uganda: Zisemavyo Katiba kuhusu Ushindi wa Mgombea Urais na Msamaha unaotolewa na Rais wa Nchi

w0rM

Member
May 3, 2011
45
150
Katiba ya Tanzania, Ibara ya 41 (6) inasema Mgombea yeyote wa Kiti cha Rais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata Kura Nyingi Zaidi kuliko Mgombea mwingine yeyote

1.PNG

Katiba ya Kenya, Ibara ya 165 (4) inasema Mgombea atatangazwa kuwa Rais Mteule ikiwa atakuwa amepata zaidi ya Nusu ya Kura Zote zilizopigwa katika Uchaguzi na angalau 25% ya kura zilizopigwa katika maeneo mengi

Aidha, Katiba hiyo ya Kenya inasema iwapo hakuna Mgombea aliyechaguliwa Uchaguzi mwingine mpya utaifanyika katika kipindi cha Siku Thelathini (30) baada ya Uchaguzi uliopita

Katika Uchaguzi huo mpya, wagombeaji watakuwa Mgombea au Wagombea waliopata kura nyingi zaidi na Mgombeaji atakayepata idadi kubwa zaidi ya kura atatangazwa kuwa Rais

2.PNG

Katiba ya Uganda, Ibara ya 103 (4) inasema, Mgombea atatangazwa kuwa Rais Mteule ikiwa atakuwa amepata Zaidi ya Asilimia 50 ya kura zote halali zilizopigwa katika Uchaguzi

Lakini pia, Katiba ya Uganda inasema kama mshindi hatapatikana basi ndani ya siku 30 utafanyika uchaguzi mpya na Wagombea waliokuwa na kura nyingi watashiriki. Atakayekuwa na kura nyingi katika Uchaguzi wa Pili atatangazwa kuwa Rais

3.PNG

KUHUSU MSAMAHA WA RAIS
Katiba ya Tanzania, Ibara ya 45 (1), Rais anaweza kutoa msamaha kwa mtu aliyepatikana na hatia Mahakamani kwa kosa lolote, msamaha huo unaweza kuwa na masharti au la kwa mujibu wa sheria

Rais anaweza kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote iwe adhabu tahafifu au kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa ajili ya kosa lolote

1.PNG

Katiba ya Kenya, Ibara ya 172 (1) inasema kutakuwa na Mamlaka ya Msamaha ambao utatekelezwa kwa ombi la Rais wa Taifa kwa mtu yeyeyote kulingana na ushauri wa Kamati ya Ushauri

Rais wa Kenya ataweza kumsamehe mtu aliyepatikana na hatia kwa masharti au la, Kuhahirisha kwa muda fulani maalumu au kwa muda usiojulikana utekelezaji wa adhabu, Kusamehe semu ya adhabu au adhabu yote

2.PNG

Katiba ya Uganda, Ibara ya 121 (1) inasema Kutakuwa na Kamati ya Ushauri ya Utoaji Msamaha itakayokuwa na Mwanasheria Mkuu (Mwenyekiti) na Raia 6 mashuhuri wa Uganda watakaoteuliwa na Rais

Kwa ushauri wa Kamati, Rais anaweza kumpa mtu yeyote aliye na hatia, msamaha wa bure au chini ya masharti halali, Kusamehe semu ya adhabu au adhabu yote, Kurahisisha adhabu kali aliyopewa mtu

3.PNG
 

Pelle mza

JF-Expert Member
May 15, 2008
3,048
2,000
Kurudia uchaguzi kwa kigezo cha kutopata kupata zaidi ya % ni waste of money na ajabu wanaporudia % haizingatiwi!
 

ROMUARD KYARUZI

JF-Expert Member
Sep 18, 2018
683
500
Kiongozi wa nchi anayeshinda majority votes 50% or+1 ya kura za wagombea wote wa kura za uraisi ndie anakuwa amekubaliwa na wananchi wote.Kusema eti mgombea akikuzidi kura moja au mbili ameshida siyo sawa maana karibu nusu ya wananchi wanakuwa wamekukataa hawajakupa ridhaa yao
 

Olororo

New Member
Dec 3, 2018
1
20
Katiba ya Kenya iko vizuri zaidi kuliko ya kwetu Tz na Uganda, zaidi kwwnye suala la mamlaka ya rais.
 

Nemean lion

Member
Jan 2, 2020
25
45
Kiongozi wa nchi anayeshinda majority votes 50% or+1 ya kura za wagombea wote wa kura za uraisi ndie anakuwa amekubaliwa na wananchi wote.Kusema eti mgombea akikuzidi kura moja au mbili ameshida siyo sawa maana karibu nusu ya wananchi wanakuwa wamekukataa hawajakupa ridhaa yao
Kama sio sawa mbona ikishindikana kupatikana mshindi wanatumia idadi kwa mara ya pili
 

nditolo

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
2,448
2,000
Soon majirani wajiandae kupokea wakimbizi kutoka Tanzania. Hii katiba imempa raisi madaraka makubwa sana.

Na serikali inatuhumiwa kufanya utekaji, uuwaji na upigaji watu.risasi (Tundu lissu na Akwilin)

Kwahiyo sidhani **** tutakuwa salama mwaka huu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

young solicitor

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
1,062
2,000
Katiba ya Kenya iko vizuri zaidi kuliko ya kwetu Tz na Uganda, zaidi kwwnye suala la mamlaka ya rais.
are you sure!!??
under BBI it's suggested that
1. mawaziri watokane na wabunge

2. uwepo wa nafasi ya waziri mkuu na kiongozi wa upinzani bungeni

3. tume ya uchaguzi itakayo husisha wanasiasa

mnachokikataa wenzenu wanakipigania.

NB: wapinzani Tanzania mnataka nini?
kupunguza mamlaka ya raisi, ili iweje??

tume huru ya uchaguzi, ifananeje!!??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom