Ingekuwa ni kenya huyu mbunge asingechaguliwa tena na wananchi wake
Last edited by a moderator:
mkuu sio hivyo tu kenya waka mbali mfano kwa siku ndege zinazotoka kenya kwenda dubai ni nne sisi tuna moja tu ambayo ni emirates na wala haijaindugu yangu wewe ita vyovyote vile plan mchakato mipango ,,lakini kinachotakiwa ni uhalisia nikupe mfano watalii asilimia kubwa wanatua kenya wanatalii kwanza halafu ndio wanaingia tz angalia idadi ya ndege toka duniani ni ngapi kwa siku halafu linganisha na jk air port ,,angalia mauwa yote ya arusha na moshi yana pitia nrb kwenda ulaya..
Wamenunua ndege ya kubebe tani 120 inasafiri zaidi ya mara tatu kwenda ulaya kupeleka mauwa tu...viwanja vipya international kisumu taveta na kule tarakea vyote hivyo wametubana sisi tumelala..bandari wanapanua mombasa na lam wanajenga kubwa wao wanabenki na shoping mall huku kwetu sisi hatuna hata blue band zinatoka kwao mimi huwa napenda kwenda mombasa likizo huduma na mandhari ni nzuri kuliko kwetu si zungumzii ushabiki ni uhalisia
Watanzania hawana sababu ya kujilinganisha na masikini, ukifikia lengo la kuona upeo wako ni Kenya basi ujue umefilisika kwa kila hali. Watanzania wapo katika level nyingine na katu hawawezi kujilinganisha na manyang'au. Tunajaribu kuwafikia wale walio kwenye the real 21st century.
Hapo kuna vitu viwili tofauti:
1.Vision
2.Plan na programu
Kenya wamejaribu kutoa kwa ufupi plan yao kulingana na vision, lakini Tanzania wametoa doc yenye vision kwa ujumla lakini malengo kama hayo utayapata kwenye national plan na development programu ambazo wizara mbalimbali zilikuwa zinaandaa, sina uhakika zimefikia wapi ila ya miaka mitano mitano utaipata ambazo zinatekeleza hiyo vision.
Hata hivyo, kuna vitu ambazo nchi kama nchi imeshaanza kutekeleza kama suala la special economic zone, miji ya kitalii na kibiashara ipo kwenye plan labda utekelezaji tu unatakiwa kuanza.
Hiyo doc ni jinsi ya kuiwasilisha tu. Inaaminika vitu vingi wabongo tunavianzisha katika maandishi na vinakubalika sana na wenzetu wajanja wanakopy na kuanza kuvifanyia kazi. Hivyo, basi hakuna jipya ambalo wakenya wameliandika hapo ambalo halipo katika plan na development programme zetu.
hani tuna kila sababu ya kujilinganisha na Kenya.... kutetea vision iliyo blind ni kujipofua permanently