Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

Jasusi said:
Mlalahoi,
Tunahitaji GACACA nyingi tu. Tuanze na gacaca ya wala rushwa, tupate Truth Commission ili watu wajue nani anatajirika kwa rushwa na kutafuta njia za kuitokomeza rushwa. Or maybe this is an issue for another topic?

Jasusi,umeadimika kidogo mzee.Binafsi ninamiss sana michango yako iliyokwenda shule.
 
Nimetoa hukumu kwa sababu ninaamini kuwa masikini kama Charles, hana hela za kumpa mtu rushwa, unless kama alipata bahati nasibu kabla au wakati wa uchaguzi,

Mtu ambaye nauli tu ya kwenda huko jimboni alikuwa hana ilikuwa kila wakati mchango! mchango!, leo akafika huko akataoa rushwa? Sihitaji mahakama kutoa hukumu!

Hukumu nimeitoa nikiwa wapi, hiyo ni kama kawaida lazima issue igeuzwe iwe Es!, Je in the future ninatakiwa nitoe hukumu nikiwa wapi ndio itakuwa fair kwako Mzee Wangu?
 
Mzee ES,

Kwa maelezo yako huyu anaonekana kaonewa, lakini hata asiyejua sharia Kajege ana maswala ya kujibu rushwa ni rushwa hata kama umetoa nyanya na mwingine katoa mamilioni. Ukisikiliza mazingira ya ya utoaji hizo takrima kama mnavyoziita huko CCM, Kajege anatakiwa aieleze mahakama, yaani mpaka shemeji yake ambaye ndo alimsaidia kuwakusanya akina mama waje wapate riziki yao naye kamgeuka?
Lazima na yeye kuna kitu kawakosea tena kikubwa inaelekea kakiuka makubaliano.
Hawa watu kusema wamenunuliwa na wakubwa ni kuwatusi,ila waliponunuliwa na Kajege walikuwa safi? jamani tunakwenda wapi yaani mtu akiwa mshikaji wako basi kila anachofanya ni haleluyah?
 
Nimekusikia Mkuuu!, lakini bado ninasimama na a Friend kuwa amefanyiwa njama tu, kwa sababu hela za kutoa rushwa as rushwa, ya kumfikisha mahakamani hakuwa nazo na mpaka leo hii hana hiyo hela,

Now sheria ni sheria, ni lazima ichukue mkondo wake na yes ninaamini kuwa anaweza kushindwa, lakini haitabadili msimamo wangu kuwa the guy is innocent isipokuwa ni siasa za bongo zinazotuambia kuwa toka tupate uhuru kiongozi mkubwa wa serikali aliyekamatwa akiiba ni Mlingwa tu, aliyekuwa katibu wa wizara ya ujenzi enzi ya Mwinyi, maana ndiye peke yake so far aliyewahi kuhukumiwa mahakani,

Je are you down with that? Ndio maana tunasema tunaielewa hii siasa na sheria za bongo!, kwamba hapa kuna namna!
 
ES

Na ukiona hivyo ujue ha kuiba za kutosha (Mlingwa). Ukiiba za kutosha haufungwi bongo. Bongo magerezani wamejaa vibaka wadogo wadogo na wasio na uwezo kifedha.
Anyway hilo jimbo lake tunalitaka 2010, ashinde asishinde tunaliwania 2010 (ndani ya CCM)

FD
 
Mlalahoi,
Nipo. Ila majukumu nayo yanazidi. Lakini napitia pitia mijadala kukomaza akili, kwa hiyo utanisia tu.
 
Mzee Es
What are you trying to tell us ? Je unachokataa ni kutoa rushwa kwa ndugu yako ama kuiba kura ? Maana hapa kuna mawili ambayo ndani ya Serikali ya CCM hayaachani . Kuiba kura na kutoa mlungula . Huyu jamaa yako kwanza alifanya vituko mno hadi kuingoza ukabila na uchawi kwenye kampeni zake. Haya yote huyasemi unalia kaonewa ?Huyu shemeji yake yeye anaisaidia Mahakama kuujua ukweli na kutenda haki. Wabunge wengi wa CCM waliingia madaraka kwa nguvu za JK lakini bado rushwa kibao kam alivyo JK mwenyewe .Semeni wana CCM makundi na mapesa yaliyo tumika kumpa JK ukandideti wa CCM .

Jimbo la Mwibara kama sikose rushwa ilitembea kuanzia na mgombea hadi Chama chenyewe na ukweli ndiyo huo .
 
Maelezo yanayotolewa humu tuyachukulie with a pinch of salt, yaani mtu akae wizarani tangu mwaka 1984 halafu asome kishidashida? kipindi hicho ilikuwa ukiwa serikalini basi na wewe ni ccm hakuna chaguo, masha karejea post 1995 sasa hawa wanafanana vipi...

Mwanakijiji huyu mheshimiwa namba yake ni +255 787 065169 hebu mpigie umhoji, nimekuwa mshabiki wa kijiji siku hizi...


Halafu mtu huamuliwa mahakamani kama ni mwizi au la sio urafiki ndio uamue, huwezi kusema mimi naona huyu rafiki yangu sio mwizi, huku ni kulindana, so much kwa mtu anaedai kuwa ana machungu na nchi yake!
 
maneno mazito kwa mara ya kwanza toka kwako tafiti ili uweze kujadili . safi mno kijana .
 
ahsante mzee murangira Mahatma GHANDHI alisema:
First they ignore you
Thenthey laugh at you
then they fight you
Then you win!
 
Yale yale,

(1). Charles amesoma Uturuki, kwa msaada wa Dr. Hussein Mwinyi, halafu akarudi bongo na kufanya kazi foreign, na baadaye kwenda Florida kusoma Masters, at one point JK akiwa waziri alopoonana naye pale ubalozini NY, ilibidi ampe hela zake za mfukoni kutokana na matatizo aliyokuwa nayo ya kipesa,

Unajua mtu mzima unapoandika maneno ya kuharibu jina la mtu usiyemfahamu jaribu kumuogopa Mungu wako kidogo, huyu Charles huko foreign aliwahi kushika nafasi gani muhimu? Hata kwenda nje kuwa diplomat hajawahi! kwa sababu ya kuwa mkweli na asiyependa unafiki ndio maana kama mwenziwe Kamandoo, wamebaki walipo mapaka leo, na wote waliamua kugombea ubunge, Charles akashinda, Komandoo akashindwa, lakini Komandoo alifanya kazi na JK CCM Dodoma zamani yeye mambo yake safi, lakini sio huyu masikini wa Mungu,

Samahani sana mzee wangu ni kwamba watu tunaowaita marafiki huwa tunasimama nao, na pia viongozi tunaowajua kuwa ni wasafi huwa tunawasimamia, isipokuwa viongozi kama RO, wanaopewa nafasi kwa kujuana ndio tuna matatizo nao na huwa hatunyamazi,

Viongozi wasafi kama Kibelloh wanaposingiziwa uizi, huwa tunauliza hadaharani hapa bila kuogopa kwamba ni rafiki au si rafiki, na wananchi wenye busara kama Kulikoni wanakubali mbele ya umma hapa kuwa kweli kwenye hili Kibelloh ni clean, ila wanafiki kama wewe wanakuja hapa na kujidai walimtembelea Kibelloh, waliyetuambia huko nyuma kuwa Kibelloh ana-SEXUAL RELATIONSHIP na secretary wake pale London, ambaye ni M-Sirilanka, ulipoulizwa FACTS, hakuna lakini ukapata time ya kwenda kumtembelea kiongozi huyo huyo, sasa ukweli uko clear kuwa hakuiba picha hapo badala ya kukubali, unakimbilia pembeni kuhusu Mwanaidi,

Sasa here you are tena ati unamjua Charles, ati na Masha alirudi 1995, alirudi wapi? Kwani siku zote alikuwa wapi? Kwa taarifa yako ni kuwa Dr. Lau Masha, alikuwa akiishai NY MT. Vernon City, ambako baba yake alikuwa Director wa Information wa UN, for 30yrs, Lau na mdogo wake Major Mugisa(JWTZ-Monduli), wamekuwa wakisoma NY na Bongo kwa vipindi mbali mbali vya maisha yao, lakini makao yao yalikuwa ni New York, baadaye Masha aliingia Mlimani bongo lakini likizo zote alikuwa NY, alipomaliza akawa na Mahalu Law Firm, baadaye akaenda Georgetown kufanya Masters, akahamia NY baada ya kumaliza, baada ya mwaka mmoja, akarudi na kuwa Secretary wa TZ Oxygen, na badaye Acting Director hapo hapo, baadaye akarudi NY tena, na baadaye akarudi tena bongo this time akajiunga na IMMA LAW FIRM, akagombea Vijana CCM Mwanza, akapata na baadye akagombea ubunge na sas ni waziri, kwa hiyo Iknow the guy bro, na tulirudi kwa pamoja tukiwa watano, na wote tuko CCM,

Na on this wote tunamsaidia rafiki yetu hadi mwisho, sheria ni lazima ifuate mkondo wake so far ni mashaidi wa prosecution ndio waliopewa nafasi kwanza kama sheria ya nchi yetu inavyotaka, baadaye itakuja zamu ya mashaidi wa Mr. Charles, tunaomba haya magazeti yasipate ububu itakapofikia hapo, hatujalala katika kumsaidia mshikaji, na ndio maana ya ushikaji, sio kuwakimbia wakati wa shida, hawa Charles na Masha, pamoja na utafiti wako huwafahamu bro,

Na ya wengine wote nimeyasikia huko juu na nimewasikieni vizuri sana, lakini Charles ni rafiki masikini ambaye siwezi kumkimbia kwa sababu ya matatizo hiyo ni tabia yangu siku zote, kama ninavyowasaidia wananchi wengi humu ambao siajwahi hata kuwaona, sifa temporarly za hii forum ni one thing, na rafiki ni another thing, na ninasema kuwa hatulali katika kutafuta kila njia ya kumsaidia, mtu yoyote mwenye uchungu na bongo atatafuta michango ya huyu shujaa Charles ndani ya bunge na kuelewa ninachosema,

Namba ya kumpata kwa kijana yoyote yule mpenda maendeleo ya nchi yetu, ni hii hapa # 745-664-907!

Sheria ni sheria, na rafiki ni rafiki!
 
Mzee Yomba Yomba,

Ninaomba niwakumbushe watu wote wa aina yako, kwamba kama una data zimwage lakini usilete hadithi za ukitaka tutasema semaa, ninajua jinsi Dr. Mwinyi alivyomsaidia akiwa Uturuki, kwa sababu kuna wakati mwingi baaada ya kuwa maswaiba Charles aliishiwa kabisa hela za kuishi pale ikabidi Hussein awe anamsaidia, na ndiye hasa aliyemsaidia sana hata kupata, ubunge, kwa sababu hata Nauli Charles alikuwa hana ya kwenda jimboni, na hata ya kuolea alikuwa hana,

I mean no question kuwa unamfahamu, je hela za kuhongea rushwa hebu nisaidie since, wewe unamjua zaidi kuliko mimi? Au hizo sehemu ulizozitaja ndizo alipata utajiri? Msumbiji alikatisha tour baaada ya miezi miwili tu kwa sababu ya kwenda kusoma Miami, la kwamba aliondolewa kwa tuhuma hilo ndo kwanza leo ninaliskia? Hebu nielezee zaidi?

Kessy ninamfahamu tena sana, maana alikuwa shule na washikaji wangu wengi pale Forodhani, na ninajua kuwa sasa yuko France ambako ninaongea all the time na Kibelloh, lakini siwezi kumpigia simu kwa hili maana what is the point? Ninampigia kumuuliza nini? Kwamba Hussein alimsomesha Charles pale Uturuki, na wakati ninajua kuwa bila ya Huseein asingemaliza ile degreee? Mimi sijasoma Uturuki na Charle au Hussein, lakini hayo ni maneno ya owte wawili between Hussein na Charles, je unamfahamu vizuri Hussein kwamba huwa hachezi na maneno, na ndio maana ninaamini kuhusu the whole uturuki story,

Kama unayoyajua sema mzee, lakini hadithi ya niseme nisisseme mimi binafsi ninaona ni utoto, maana hapa tunaandika kuwasaidia wengi na pia sisi wenyewe kusaidiwa, ni kweli kwamba unamfahamu lakini hujasema ukweli katika mambo yanayomhusu, na besides hata unayosema na utakayosema yatakuwa yana ukweli, maana kama ninakuelewa ni kwamba Charles hayumo kwenye haya matatizo kwa bahati mbaya,

Great, he is still a friend na hata siku moja siatrudi nyuma kwenye kumsaidia, sheria ni lazima ifuate mkondo wake, lakini rafiki masikini bado ni rafiki hata masikini kiasi gani, na wakati utakapofika wa mashahidi wake kuongea ukweli, pasiwe na ububu kwa watu kama mnaomfahamu!

Ninasubiri more ya jinsi unavyomfahamu na nisivyomfahamu, ili kuweka sawa point ya kuwa hana makosa anayosingiziwa, maana ndio issue yangu hapa!, na issue sio kumfahamu kama ilivyotaka kupindishwa na mzee wa kupindisha issues, TAFITI!

Ya Canada, sijawahi kusikia nilijua alikwenda kusoma, akashindwa kulipiwa pesa za shule, ala kumbe alikwenda ubalozini akafukuzwa ka muda mfupi hivyo, hebu niwekee, maana nitaamuuliza kwa kirefu na nitaleta ukweli hapa hapa?
 
manen yako Mzee Es yamejaa walakini na hili linanipa wasi wasi na misimamo yako mingi hapa kiwanjani.Leo unasema kwa hali na mali mtamsaidia kijana Charles aendelee kuwa Mbunge .Wewe Es uko kwenye state na watu wa aina yako yaani Usalama na wengine ndiyo aidha waliiba kura ama walileta mbinu za hongo .Mlalamikaji si mjinga kuamua kufungua kesi na huyo jamaa yako ni mchafu maana alitumia hata maneno ya vitisho na ushirikina kwenye siasa .Yote haya leo yanaelezwa kwa uwazi. Ukisema atashinda kwa kuwa Serikali ni ya CCM ni sawa maana si kawaida na haitatokea CCM kutenda hadi kweney uchaguzi wowote .Ila mwisho wa mambo ya namna hii huwa ni mabaya .Mimi nadhani Es huwa hutetei haki ama Nchi yako bali unatetea maslahi na wote wanaona sasa kwa ushahidi wa wewe kupamba kesi na kusema jamaa ni innocent na hakutoa rushwa .Je kwani wewwe ulitaa atoe nini ujue kwamba hii ji rushwa ? Pale ni Charles anashitakiwa na CCM kwa wizi ama kuhonga .
 
Mzee wa kunyumba,

Nimekusikia, ila tafadhali sifanyi kazi usalama, hapana na sijui unakofanya kazi na tusihitaji kujua tunakofanya kazi, sio issue, kuhusu misimamo yangu you have all the rights kuitafsiri, lakini haibadili what I stand for,

kwamba Charles hana hela ya kumpa mtu rushwa, na hajawahi kuwa nayo maishani mwake, unaless kama alikuwa akificha na kujiabisha kwa marafiki huku nyuma kumbe anazo,

I am praying kwamba siku moja kwenye hii forum tutakata issues bila ya mimi kuwa subject, ingawa I do not mind maana ndipo utamu wa malumabno unapokuja, waliotoa ushahidi ni watu wa upande wa mashitaka so far, kwa hiyo bado pia na wa upande wa charles wanakuja,

Hayo ya usalama na serikali, siyajui na sitayagusa, mimi ni mwanasiasa ndani ya CCM na serikali, lakini sio usalama!
 
Rushwa ya wawekezaji wageni yapofusha viongozi serikalini

Ndyesumbilai Florian na Ramadhan Semtawa
BAADHI ya viongozi katika serikali ya Tanzania ni miongoni mwa watu wanaoelezwa kupofushwa na rushwa inayotolewa na makampuni makubwa ya uwekezaji kutoka nchi 30 maarufu duniani ili kupindisha sheria na kanuni, ripoti ya hivi karibuni ya Shirika la Transparency International (TI) imefichua.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo wa TI, walengwa wakuu katika mtego huu wanaelezwa kuwa ni viongozi wa serikali, mashirika yake ambao hongo imewalevya, hivyo kuwalainisha kupitisha miradi, zabuni, uwekezaji au biashara.

Katika orodha hiyo, (nakala tunayo), hata hivyo, makampuni kutoka Ufaransa, Italia na India, ndiyo yanadaiwa kuongoza kwa uchafu huo wa kuchochea rushwa.

Orodha ya nchi hizo 30, inaongozwa na Uswisi iliyopewa alama 7.81 (kati ya 10 za juu), ingawa India ni ya mwisho ikiwa na alama 4.62. Mataifa tajiri, Uingereza iko katika nafasi ya sita ikiwa na alama 7.36, Marekani, nafasi ya 10 (pointi 7.22) ikifuatiwa na Japan (7.10).

Barani Afrika, imo Afrika Kusini yenye alama 5.61, ikiwa katika nafasi ya 24 huku ikiwa ya kwanza kwa bara la Afrika. Nchi hiyo, pia ni mwekezaji mkubwa miradi mbalimbali iliyoko Tanzania.

Nchi kama vile, India na China ambazo zimetokea kuwa washirika wakuu wa kibiashara na uchumi wa nchi za Afrika, ripoti ya shirika hilo la kimataifa la kupambana na rushwa inafichua na kueleza kwamba mikataba mingi ya kibiashara baina ya makampuni ya nchi hizo na nyinginezo imeoza kwa rushwa.

Wakati hali ikiwa ni hivyo, takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), zinaonyesha kwamba baadhi ya nchi zilizotajwa ndani ya ripoti ya TI kwa kuchochea ufisadi zimo katika nchi kumi bora zinaoongoza kwa kuwekeza vitegauchumi vyao katika sekta mbalimbali nchini.

Nchi hizo ambazo zinaongozwa na Uingereza nyingine ni pamoja na India, China, Italia, Ujerumani, Marekani, Uholanzi, Canada, Afrika Kusini na Kenya.

Kati ya nchi hizo, Uingereza imewekeza nchini katika miradi 527 ambayo ni pamoja na sekta ya kilimo, India miradi 120 na China 123.TI, kwa upande mwingine inaeleza wasiwasi wake kuhusu rushwa hii ya kiwango cha kimataifa, inayozihusu sekta mbalimbali zikiwamo za uwekezaji, biashara inavyozidi kuongezeka na hata kutishia uhai wa nchi hizo kiuchumi.

Orodha hiyo ya nchi 30 zinazoongoza, hasa kwa makampuni yake kuhonga ili kupata zabuni au kazi nyinginezo, TI inasema inaonyesha kukiukwa kwa sheria na taratibu za kimataifa.

Taarifa hiyo inayoitwa Transparency International 2006 Bribe Payers Index (BPI), inaelezwa kuwa ni ya utafiti na uchunguzi wa aina yake ambayo haijawahi kufanyika.Ripoti hiyo ya Oktoba 4, inaeleza kuwa imeyachunguza makampuni zaidi ya 400 kutoka nchi 30 zikiwamo zenye viwanda au zile zinazoongoza kwa usafirishaji na uuzaji nje bidhaa.

Kwa bahati mbaya, nchi tajiri kama vile, Uingereza, Marekani, nazo zimeorodheshwa kwamba makampuni yake ni miongoni mwa yale yenye rekodi mbaya."Imekuwa kawaida kwa makampuni kutoka nchi hizi tajiri kutoa hongo, hasa kwa nchi zinazoendelea ili kupata kazi," inaeleza TI ambayo imetoa alama 10 zikiwa ni za juu kwa makampuni ya nchi hizo 30. Licha ya mataifa tajiri, lakini TI inaeleza pia wasiwasi wake kuhusu kujiingiza kwa makampuni kutoka mataifa yanayokuja juu kibiashara kwa ngazi ya kimataifa, yaani India, China na Russia.

Lakini kwa upande wa China na nchi hizo zinazoitwa 'wafalme wajao' kibiashara, shirika hilo linaeleza kuwa hata juhudi za kupambana na rushwa na ufisadi zimeshindikana kiasi cha kuwa mzigo wakati vitendo hivyo vinapohamishiwa nje ya mipaka ya nchi hizo.

“Makampuni hayo yanahonga na hivyo kukwamisha juhudi za serikali za nchi maskini katika kupambana na maovu kama rushwa, kujenga misingi ya utawala bora, matokeo yake nchi hizo zinazama zaidi katika lindi la umaskini,” anaeleza Mwenyekiti wa TI, Huguette Labelle.Walengwa wakuu wa mtego, TI inaeleza kuwa ni pamoja na maofisa wa serikali, makampuni na wengineo ambao kwa namna oja au nyingine wanahusika katika kufanikisha miradi.

Katika uchunguzi wake ambao ulihusisha wafanyabiashara zaidi ya 11,000 kutoka nchi 125 kuhusu mtazamo huu wa hongo na rushwa katika kupata zabuni, wengi walionyesha wasiwasi wao kuhusu jinsi makampuni kutoka India yanavyohusika katika mtego huu.Katika hatua ya kushangaza, TI inaeleza kuwa wafanyabiashara wengi kutoka Afrika waliohojiwa wakati wameyataja akampuni kutoka Ufaransa, Italia kama ambayo yamebobea kwa kuchochea vitendo hivyo.

“Ni unafiki mkubwa kuona makampuni kutoka nchi zilizoendelea yakiendelea kutembeza hongo karibu katika nchi zote ulimwenguni, huku serikali za nchi zao zikiyafumbia macho au kuendelea kutoa mashinikizo kwa nchi maskini zijenge utawala bora," anaeleza mwenyekiti huyo. Ripoti hiyo, pia inazituhumu nchi zote ambazo makampuni yake yanatuhumiwa katika kushiriki maovu hayo kwa kushindwa uchukua hatua thabiti na za kutosha kuzuia rushwa hiyo ya kimataifa,” anaeleza Mtendaji Mkuu wa TI, David Nussbaum.

Anaongeza: “Kwa hakika rekodi ya mataifa hayo kuhusu vita dhidi ya rushwa na ufisadi katika sekta ya biashara kimataifa inasikitisha kuisoma.”“Sote tunajua kwamba sheria na kanuni zipo, lakini ama hazitumiki au haziheshimiki kabisa,” anaeleza.”Sheria za kitaifa zimetungwa ili kupambana na rushwa na ufisadi kwa nchi moja moja, kutokana na kubuniwa na Umoja wa Mataifa (UN)na zimeridhiwa, lakini ugumu ni kwenye utekelezaji wake,” anaongeza.Nchi nyingine ambazo zinatajwa kubobea bali ya China na Russia ni Uturuki na Taiwan.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TI kwa Kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati, Casey Kelso, anaeleza kuwa rushwa imekuwa ikitumiwa kama kishawishi cha kupata zabuni na nafasi za kibiashara.Kelso anayatetea makampuni hayo kuwa hayatoi tu rushwa au hongo au kuichochea rushwa, isipokuwa kwa kushindwakuvifichua au kuvikemea vitendo vya rushwa katika nchi zao vinapofanyika. TI Bripe Payers Index 2006: the rankings
Katika hatua nyingine, wakati TI ikieleza msimamo huo, mchumi kutoka Benki ya Dunia analionya bara la Afrika ikiwamoTanzania kuhusu ongezeko la makampuni ya India na China yanayowezeka katika ardhi yao.

Mchumi huyo, Harry Broadman, katika kitabu chake: Africa's Silk Road: China and India's New Economic Frontier, anaeleza kuwa licha ya ongezeko la makampuni ya nchi hizo kuwekeza katika sekta mbalimbali katika Afrika, lakini kukosekana kwa uwiano ulio sawa kibiashara, Afrika inaumia zaidi.

Kitabu hicho alichokitoa mwezi uliopita, mchumi huyo anazieleza China na India kuwa zinaelekea kuzipokonya nafasi ya kibiashara Ulaya na Marekani katika kuwekeza na kufanya biashara Afrika.Hata hivyo, anaonya mchumi huyo kuwa nchi hizo zinakabiliwa na changamoto zaidi kutokana na kufanya biashara namataifa hayo ambazo baadhi yake kodi ziko juu, hasa kwa bidhaa zinazoingizwa katika masoko yake.

Broadman anaeleza kuwa ingawa kumekuwako na ongezeko la bidhaa kutoka Afrika kwenda Asia katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, hali iliyofanya bara la Asia kuwa mshirika mkubwa wa tatu kibiashara na Afrika hadi kufikia asilimia 27 na kuziacha Ulaya yenye asilimia 32 na Marekani asilimia 29, bado hali si shwari.Anaeleza kuwa kwa kipindi hicho, rasilmali kutoka India na China zilizowekezwa Afrika ziliongezeka kwa China uwekezazenye thamani ya dola 1.18 bilioni hadi Juni mwaka huu.

Uchunguzi katika makampuni 450 ya Kichina na India katika nchi za Afrika Kusini, Tanzania, Ghana na Senegal, mchumi huyo anaeleza kuwa yamewekeza katika sekta mbalimbali, ikiwamo za mafuta, maliasili, ujenzi, viwanda na kadhalika.
spacer.gif ¨"Lakini, ukifanya uchunguzi kwa sasa, inachouza Afrika huko India na China ni malighafi au maliasili tu," anaelezaBroadman.

Katika kitabu hicho ambacho mchumi huyo alikizindua wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia uliofanyika Singapore, ambao ulizungumzia pia jinsi ya kuwasaidia watu 300 milioni wanaokabiliwa na umaskini katika Afrika, anaeleza pia bara hilo linahitaji miujiza ili kujinasua katika umaskini kama ilivyofanyika kwa watu milioni 400 barani Asia miaka 25 iliyopita.Wasiwasi wake ni kuhusu uwekezaji kama njia ya kuleta matumaini kwa Afrika hasa kwa kuendelea kuwapo kwa vikwazokama vile uhusiano usio sawa wa kibiashara baina ya maeneo hayo mawili.

Kwa mfano, anaeleza mchumi huyo kwamba China na India zinazotoza viwango vikubwa vya kodi kwa bidhaa kutoka Afrika, jambo linalozizuia nchi hizo kupenya katika soko hilo.Kwa mujibu wa mchumi huyo, biashara ya nje ya Afrika kuelekea Asia ni asilimia 1.6 ya biashara ya bara hilo (Asia) ulimwenguni.

Hata hivyo, mchumi huyo anaeleza kuwa dhana ya ushirikiano wa kusini-kusini, kupitia uwekezaji katika Afrika, huenda ikabadili hali hiyo.

Mchumi huyo anaona kuwa kuendelea kuzalishwa kwa bidhaa katika nchi hizo za India na China ambazo zina soko kubwa Afrika, kutokana na kuwa za bei ya chini, machoni mwa wachumi wa Afrika zinaonekana kuwa zinadumaza soko la ndani.

Anaeleza wasiwasi ambao unakubaliwa na wafanyabiashara wazawa, kwamba bidhaa hizo zinashindana na zile zinazozalishwa katika nchi hizo, ikiwamo Afrika Kusini.
 
Mzee Mlalahoi,

Huyu jamaa pamoja na kitabu kupanda hivyo, bado hajawahi kupewa "NAFASI", kwa sababu ya kuwa mkweli, na asiyependa unafiki wala mchezo na kazi!
 
Back
Top Bottom