Mlalahoi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2006
- 2,182
- 885
Diwani CCM akiri mbunge wake kutoa rushwa
Na Mwandishi Wetu, Mara
DIWANI wa Chama Cha Mapinduzi, Mary Bandoma, ametoa ushahidi kuwa mbunge wake alitumia rushwa katika kampeni za uchaguzi jimboni humo.
Alitoa ushahidi huo katika Mahakama ya Mkoa wa Mara kwenye kesi ya kupinga matokeo ya Mbunge wa Mwibara (CCM), Charles Kajege, iliyofunguliwa na mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Mutamwega Mugayhwa.
Diwani huyo alisema Desemba 10, 2005, Kajege akiwa mgombea wa CCM kwenye jimbo hilo alifanya kikao cha ndani katika eneo la Bulamba Ginnery, ambapo baada ya mkutano aliwagawia wananchi sh 500 kwa kila aliyehudhuria.
Alidai kuwa siku moja kabla ya Uchaguzi Mkuu kufanyika, mbunge huyo alialika watu kwenda kumsikiliza katika eneo la Kibara, wengi wao wakiwa wanawake na baada ya mkutano alianza kuwagawia kanga, vitenge na sabuni.
Diwani huyo alisema, mbunge huyo aliwataka wananchi hao wampigie kura na kuwaahidi kuwa mambo yao yatanyooka wakimchagua kwa kuwa rais aliahidi kumteua kama waziri.
Shahidi huyo ambaye naye alikiri kupokea mgawo huo, alipoulizwa iwapo aliwahi kumshauri au kumwonya mwana CCM mwenzake juu ya vitendo hivyo, alisema waliwahi kufanya hivyo kupitia kikao cha kamati ya siasa lakini alipingwa na baadhi ya wajumbe.
Alisema hata mbunge mwenyewe alimwambia kuwa yeye haogopi na ametumwa na rais kugombea nafasi hiyo ya ubunge kwenye jimbo hilo.
Diwani huyo alisema ameamua kutoa ushahidi huo ili kulinda masilahi ya chama na kuwa CCM imedhalilishwa kwa vitendo hivyo.
Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa leo katika mahakama hiyo mjini Musoma, ikiwa chini ya Jaji Mchome