Tanzania: Utajiri wa gesi waanza kunufaisha vigogo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania: Utajiri wa gesi waanza kunufaisha vigogo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Informer, Sep 22, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Informer

  Informer JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2012
  Joined: Jul 29, 2006
  Messages: 1,224
  Likes Received: 2,438
  Trophy Points: 280
  UTAJIRI wa gesi asilia Tanzania, unatishiwa na ufisadi ndani ya mfumo wa utawala na kuna taarifa za uhamishaji wa fedha zinazohofiwa kutokana na uwekezaji katika sekta hiyo.

  Uchunguzi umeonyesha kwamba, kwa miaka kadhaa, baadhi ya watu ndani ya mfumo wamekua wakitumia mbinu chafu kujinufaisha na rasilimali ya gesi nchini.

  Tanzania inatarajiwa kuongeza makisio ya kiwango cha utajiri wake wa gesi asilia hadi kufikia takriban futi za ujazo trilioni 30.

  Pamoja na marekebisho hayo, kuna mashaka kama mapato mengi yatakayotokana na gesi hiyo yatatumika vema bila kuathiriwa na ufisadi.

  ------- Nimeruka mistari kadhaa-------

  Hata hivyo ni uwezekano mkubwa wa ufisadi wa kutisha katika kutoa leseni mpya za utafutaji gesi baharini unakowaogofya wachambuzi wa mambo katika tasnia hiyo.

  Hata hivyo Kabwe amekuwa akijumuisha pamoja ufisadi mdogona mkubwa ili kulitohoa suala la ufisadi na kuishinikiza serikali.

  Agosti 15, 2012 Zitto alitangaza kwamba taarifa ya mwezi Juni ya benki kuu ya Uswisi, Swiss National Bank (SNB), ilionyesha kwamba viongozi serikalini pamoja na wafanyabiashara wakubwa walikuwa wameficha fedha katika akaunti zao nchini humo zinazofikia 315.5bilioni/- (USD 200million).

  Kila mwaka Benki Kuu ya Uswisi huchapisha jumla ya fedha na mikopo zinazomilikiwa na wageni, ingawaje taarifa hiyo haichambui kiasi ambacho kila mwenye akaunti anamiliki.

  Kabwe aliliambia bunge, "Kambi rasmi ya upinzani imepata taarifa kwamba kiongozi mmoja mwandamizi na mawaziri kadhaa katika utawala uliopita wamo katika orodha ya watu wenye mapesa hayo.

  Sehemu kubwa ya pesa hizo zililipwa na makampuni yanayotafuta mafuta na gesi katika pwani ya Mtwara yaliyopewa leseni kati ya mwaka 2004 na 2006.

  "Kambi rasmi ya upinzani inaitaka serikali kutoa tamko rasmi kuhusu hatua ilizochukua tangu tangu ripoti hiyo ya Benki Kuu ya Uswisi ilipotoka. Tunaitaka serikali iliambie taifa hatua itakazochukua ili kuzirejesha fedha hizi pamoja na nyingine ambazo zimefichwa katika nchi nyingine za nje. Kambi rasmi ya upinzani itayatangaza majina ya wanaomiliki fedha hizi katika mabenki nchini Uswisi kama serikali haitotoa taarifa rasmi juu ya suala hili."

  Kampuni ya Kiingereza ya Ophir Energy, ambayo inamilikiwa kwa ubia na kigogo mmoja katika chama tawala nchini Afrika ya Kusini cha African National Council, Waziri wa Makazi Tokyo Sexwale, kilipewa Kitalu 1 katika pwani ya Mtwara katika duru ya tatu ya utoaji leseni mwaka 2005.

  Ophir ilipewa vitalu viwili zaidi, Kitalu 3 na 4, bila kushindanishwa mwaka uliofuata. Hii si kutoa hisia kwamba rushwa ilihusika. BG, zamani ikiitwa British Gas, baadaye ilinunua hisa katika vitalu hivyo na ndiyo inayoviendesha wakati Ophir ni mbia mwenye hisa chache.

  Mtu wa kati ambaye ni mfanyabiashara raia wa Afrika ya Kusini na mwenye mahusiano ya karibu na ANC, Moto Mabanga, alisaidia Ophir kupata vitalu hivyo. Alifungua kesi jijini London mwezi Juni 2012 dhidi ya Ophir kuhusiana na mgao wake wa asilimia tano (5%) ya faida kwa mujibu wa mkataba wa kuchangia uzalishaji uliofikiwa.

  Mabanga pia aliliingia katika mgogoro na kampuni ya nchini Afrika ya Kusini ya Vodacom juu ya ada kwa huduma zake baada ya kufanisha matatizo yaliyokuwa yanaitatiza kampuni hiyo nchi Kongo-Kinshasa.


  CHANZO - Fikra Pevu
   
 2. t

  tenende JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kamanda Zitto bado kazi nzito iko mbele yako! Ni vema vigogo hawa tuwajue kwa majina. Usivunjike moyo na shutuma piga kazi.
   
 3. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Okay,

  Napata picha ya chanzo cha accounts za Uswiss (2004-2006)
   
 4. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,578
  Likes Received: 1,674
  Trophy Points: 280
  Duh! yani wa south washa anza kufaidi sisi bado?
   
 5. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mimi naona ngoma bado mbichi! Tunataka jinsi hao wamiliki wa hizo kampuni walivyoziweka pesa kwenye hizo akaunti. Kusema Tokyo Sekwale ana hisa Ophir haisaidii. Kila mtu Afrika Kusini anajua Tokyo Sekwale ni mfanyabiashara mashuhuri

  Kama ZZK ataweza kumnanga Tokyo Sekwale kwenye hii shutuma basi atakuwa amemsaidia sana Zuma.

  Tokyo Sekwale ni hasimu mkubwa wa Zuma katika kinyang'anyiro cha ugombea urais kwa tiketi ya ANC Mangaung mwezi Desemba.

  Tokyo Sekwale ndiye aliyekuwa akimfadhili MALEMA afanye kazi chafu ya kumfitini Zuma ili aondolewe Mbeki style
   
 6. Mkali Tozz

  Mkali Tozz JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Siku hizi kipofu hazuiiwi kula kwa kushikwa mkono, Huporwa kilichopo mdomoni!

  Tunawaombea majambazi wote wa rasilimali za nchi hii mungu awape magonjwa ya MOYO, TB, PRESSURE, VISUKARI na UKWIMWI na Wasionje hata kidogo. WAFE mapema then wakajibu makosa yao kwenye mahakama za haki kwa mungu. Maana mahakama zao hizi kwenye tawala zao hazitendi haki!
   
 7. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Mjumbe siku hizi anauwawa kama unabisha mpigie simu Mwangosi atakwambia; ila kwa ujumbe tumeusikia ngoja tuuingize katika mlolongo wa sababu za kuitoa CCM madarakani.
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  kidumu chama cha mapinduzi.....

  Chukueni Chenu Mapema wasiwazintue wala nini
   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  kidumu chama cha mapinduzi.....

  Chukueni Chenu Mapema wasiwazingue wala nini
   
 10. m

  mharakati JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  nani alikua nishati 2004-2005 au ni ile kitchen cabinet ya bw mkapa ya akina yona,mramba,kigoda
   
 11. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mi naamini zitto ni mtu mwenye uwezo wa kuongoza nchi kama rais wa Tz lakini siamini kama anaweza kuwakilisha maslahi na mahitaji ya watazania waliokaliwa kimabavu na Ccm kutokana na tamaa zilitookithiri za uroho wa madaraka alionao na kimsingi hawezi kupambana kizalendo anapooneshwa fedha!

  Hii ni tabia ya viongozi vijana waliotoka kwenye familia duni kiuchumi!

  Ila kama angetumia busara kidogo na uvumilivu ili kwanza ajijenge kisaikolojia na kizalendo ktk nafasi yake ya ubunge angekuwa kiongozi mzuri siku zijazo kwa nafasi ya uraisi!Jinsi alivokaa kimya wakai viongozi wenzie wanatetea maslahi wa Tz waziwazi na ushahidi kwamba anapata maslahi makubwa ktk ukimya huo kutoka kwa wakandamizaji wa demokrasia na uchumi wa nchi ambao ni Ccm...

  Nimtahadharishe kwamba hapa anajifuta kwenye mioyo ya Tz wote hata hao ccm na anajiua kisiasa hivyo nimtolee mwito wa kushituka na kurudi kwenye siasa za kiharakati na ukombozi ACHANA NA CCM utaadhirika sana zito Acha njaa
   
 12. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  hii balala. natafuta kazi ya kukata mafisadi vichwa na kuwachoma moto sijui itatangazwa lini
  nawashauri wachangiaji msiwe mna reply with quote kama mada ni ndefu
  watu wanaotumia simu wanapata shida sana kusoma.
   
 13. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Linaloniuma zaidi ni kuwa mtz wa kawaida haoni huu ujinga ndani ya mfumo huu na kuamua kuendelea kuukumbatia. We are really cynics!!!!
   
 14. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Eeeh mungu ipokee dua hii ya Mkali Tozz na mimi na wazalendo wooote wanauguswa kwa uchungu na wizi huu na ubakaji wa rasilimali za nchi yetu.
   
 15. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #15
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Miaka ya nyuma mabenki ya Uswisi yalikuwa na usiri mkubwa sana na haikuwa rahisi kupata taarifa za pesa chafu km ilivyo sasa. Ndio maana kina Mobutu walificha nyingi tu huko.
  Kwa mtindo huu wa sasa,unasaidia sana nchi maskini zilizokuwa zinaporwa kila kukicha. Tungejuaje kwamba kuna zaidi ya 300bo zimefichwa huko?
  Yote kwa yote Mh Zitto tunasubiri hyo list ikiwa ni chachu ya kufanya maamuzi sahihi 2015.
   
 16. J

  Joachim Morgan Member

  #16
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mbona uzi wenye kuhusisha uporaji wa rasilimali za nchi hawa jamaa hawaonekani wao wanachangia kuhusu CDM tu tatizo ni nini? Ritz, Mdizi, Rejao, Majebere, Zawadi Ngoda na wenzao au wao ni sawa tu rasilimali zikiibwa naomba majibu.
   
 17. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #17
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Very Strong accusations can only win hearts if supported with empirical evidence.
   
 18. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #18
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,480
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  Zitto ni mwanasiasa makini sana katika ufuatiliaji wa uporwaji wa raslimali za nchi, lakini kwa mtazamo wangu naona ni sehemu ya yeye kujipatia fedha kwa hao wanaohusika na kashfa hizo, hapa tunaona anachelewa kutaja hayo majina inawezekana ili hao wahusika wamwagie mafedha na issue ndo hiishie hapo.

  Sitegemei kwa muda unavyochelewa hivyo kama huyu jamaa atataja hayo majina.
   
 19. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #19
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Wale ambao hawana kazi na wenye fikra finyu ndo wanajadiliana nao hao. Wenzako kila wakiandika hapa wanalipwa na CCM.

  Wewe changia kujenga nchi achana na vyama
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...