Tanzania upole na unafiki wetu ndiyo sababu ya Umaskini wetu

Thailand

JF-Expert Member
Nov 15, 2019
263
778
Ndugu zangu miaka ya 1960s kipindi tunapata uhuru wetu, Uchumi wetu in terms of GNP tulikuwa sawa kabisa na nchi kama Vietnam, Thailand, Singapore, Malysia, Uchina na Korea Kusini.

Kwa kipindi chote hicho hakuna chama chochote cha upinzani kilichoingia madarakani na either tukakitupia lawama kwa kutuletea Umaskini huu wa kutupa.

Lawama zote hizi za Umaskini na poor democracy in Tanzania msingi wake mkubwa ni kwa CCM kwa maana ndicho chama kilichomadarakani tangu tunapata uhuru 1961 hadi leo 2020.

Inasikitisha kuona CCM inashindwa kuruhusu uhuru wa Watanzania kuwa-challenge kwa hoja na wao kukimbilia kutumia vyombo vya ulinzi na usalama kama kinga yao dhidi ya kuambiwa ukweli.

CCM jibu swali, kwanini Tanzania ni Maskini imepitwa na nchi ambazo mwanzoni tulikuwa tunalingana nazo Uchumi sasa wapo mbali maradufu kutupita sisi tulipo na rasilimali nyingi kuwapita?

Uelewa wa watanzania unaongezeka sana kiasi kwamba wengi hawataki na wamechoka kudaganywa kwa nini serikali inatumia nguvu kubwa kudhibiti wingi wa Watanzania wanaoufuta sera za upinzani?

Kuna asali gani hapo Ikulu ambayo mnaona Watanzania wengine hasa wa sera mbadala hamtaki wao waiguse kwa ajili ya kusaidia watanzania wengine kufikia ndoto zao kwa sera zenye uwazi kwa Kila hatua Tanzania tunayolenga kuifikia?

Mawazo yananipeleka kusema kwamba sababu ya hiki cha chama cha kijani kubaki madarakani ni upole na unafiki tulionao Watanzania.

Watanzania tupo kwa ajili ya matumbo yetu kwenda choo hatuna hatua yoyote tunayopiga kwa ajili ya make a legency (a big influential history) kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Ndio maana Kitila yule ambaye akiwa upinzani aliona Mdahalo ni kipimo tosha kwa wagombea wetu wa uraisi Ila leo ukimwambia amuombe mwenyekiti wake wa chama atokelezee kwenye Mdahalo hatakubali. Wapinzani wengi waliohamia chama tawala ni Tamaa na hofu ya kuendelea kupata kujipendekeza kwa jiwe ili wapate vyeo wapo kwa ajili ya matumbo yao. Fake! Vyama vya siasa si vipo vingi kwa Nini hawakuona haja ya kwenda hata ADA-TADEA nacho si no chama cha siasa!

Halafu wakishafika huko kwenye chama tawala akili zinawaruka kusapoti hata vitu vya kijinga hutazania hawana reasoning ability.

Watanzania tusingekuwa waoga, wapole na wanafiki leo hii tungekuwa na KATIBA mpya ambayo asilimia 💯 Ni naomi na mapendezo ya watanzania namna watakavyo nchi yao iongozwe. Lakini kwa ukorofi wa CCM wakakataa yale naomi na Warioba mwenyekiti wa tume Ile kudhalilishwa huku Watanzania tunacheka kinafiki?

CCM jitokezeni mseme Ile KATIBA mpya yenye naomi ya watanzania na iliyotumia Pesa nyingi kukamilisha kwa nini mliitelekeza? Mnadhani mtaendelea kutawala kwa msingi wa kufinya mienendo yenye kwa kuikataa KATIBA mpya?

Tukio la LISSU kupigwa risasi mchana kweupe kama watanzania tusingekuwa waoga wapole na wanafiki wakutupwa tungeshawajua wauwaji wale kwa sababu sio suala la upinzani tu bali ni suala la undugu na utu wa mwanadamu. Watanzania tungeshinikiza jensi la police litutajie askali walinzi waliotakiwa kulinda nyumba Ile ya Tundu ila muda huo walikuwa wapi na kwanini watoke wote muda wa tukio nani aliyewapa order hiyo tungeanzia hapo kwanza kuwawajibisha wahuni hao ambayo kwa uoga na UPOLE wetu mpaka leo serikali haijaangaika kuwatafuta watu hao. Lakini serikali inajisahau kwamba ukipandacho ndicho ukivunacho, yametokea mauaji Iringa kwa kiongozi wa UVCCM rais ametoa tamko la kutafuta watu hao haraka anasahau hakuongea polite kwa wale walioutesa utu wa TUNDU LISSU kwa kumpiga risasi.

Leo hii mkurugenzi wa NEC anaisaidia CCM kukipigia kampeni kwa kutoka makalipio makali vyama vya upinzani vilivyo na nguvu Tanzania ili tu kuipa CCM uhalali wa kuchukua ushindi wa uchaguzi mkuu wa October 28. Anasema eti hataki chama ambacho kitauza MADINi yetu nje kwa wazangu!

Hivi ndugu zangu Acacia na BARICK north Mara wanaomiliki migodi yetu ya dhahabu Ni ' Wazaramo!? halafu huyu nae anajiona Ni msomi wa PHD. ujinga wa watanzania ndo inaufanyia chama hiki kiendelee kuwa madarakani lakini watanzania tungekuwa tunajitambua mpaka Sasa hivi huyo mkurugenzi tungeshamchomoa hapo ofisini maana hayupo kwa ajili ya watanzania Kama ameshayaonesha haya mapema hivyo kweli atakuwa na moyo mwepesi kutangaza matokeo ya chama Cha upinzani kushinda endapo kitashinda?

Watanzania wenzangu, tujadili namna tunavyoweza kuondokana na uwoga na unafiki tulionao kufanya mabadiliko yanayoweza kuleta neema kwa taifa hili na kuweka historia kwa vizazi vijavyo.
 
Kesho tunasubiri barua ya NEC kwenda kwa magu kumuomba afike kwenye tume ya uchaguzi ajieleze Ni kwa Nini anawatishia wananchi kwamba wakichagua wapinzani hata wapelekea MAENDELEO huku kodi kutoka kwao anakusanya
 
Tunapaswa kuingia mtaani kukataa yanayoendelea mara moja la sivyo nchii itaangamizwa na washenzi fulani.
 
Kina mwanasiasa mmoja wa upinzani akiwa Arusha aliwahi kusema "Nchi hii ina wanawake wajinga na wanaume wapumbavu".

Elimu tunayopewa kwenye shule za kata haituongezei chochote bali ujinga na upumbavu.

Adui ujinga anaendelea kukua kwa kasi sana.
 
What I know for sure is , this october i’m voting for TUNDU LISSUu for so many reasons. but the biggest of all is that i don’t want to see some insecure, paranoid man in the highest office in the country who cares very little about laws and constitution. i also ask you to vote for TUNDU LISSU.

Babymama cariha , pls join me
 
What I know for sure is , this october i’m voting for TUNDU LISSUu for so many reasons. but the biggest of all is that i don’t want to see some insecure, paranoid man in the highest office in the country who cares very little about laws and constitution. i also ask you to vote for TUNDU LISSU.

Babymama cariha , pls join me
Nakuunga mkono
 
Back
Top Bottom