Tanzania: Upinzani wajipanga kuungana 2015

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Vyama vya siasa vyenye idadi ndogo ya wanachama nchini vimekubali hatua ya kuungana na kuwa Muungano wa vyama (Alliance) kwa lengo la kupata nguvu ya uwakilishi wa kuingia katika Bunge Jipya la Shirikisho baada ya rasimu mpya kupitishwa kwa ajili ya uchaguzi ujao.

Hatua hiyo imekuja baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya kutangaza rasimu iliyotoa mwelekeo wa kupatikana kwa Katiba Mpya ya Tanzania.

Akizungumza jana na gazeti la Mwananchi, Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR Mageuzi, Samweli Ruhuza amesema hali hiyo inaweza kuleta changamoto kubwa hivyo muda sahihi wa vyama vichanga kuzungumzia hili ni sasa.

Katibu mkuu wa chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muhabi anaunga mkono hatua ya kuunganisha vyama hivyo kwa lengo la kuwakilisha mawazo yao kwa maslahi ya taifa.


Mwananchi
 
wanaweza kuungana sema hawawezi kudumu kwani historia ya vyama kuungana katik afrika inaonyesha hazidumu kamwe.
 
Muungano wa maliberali?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hongereni kwa kuungana labda mtatuwekea wabunge wasio wapiga kelele na wasio waropokaji pale mjengoni kama nani na nani wa nyanda za juu kusini.
 
Hakuna kitu kizuri katika siasa kama vyama kuungana kwani wakati mwingine upunguza msululu wa vyama visivyo na tija na kujenga imani ya kweli kwa watu katika ushindani.Hapa tunaanza kupata picha halisi ya utaifa na kuondoa dhana ya vyama vya siasa kuwa ni miongoni mwa taasisi za watu binafsi.
 
Back
Top Bottom