Tanzania, Uganda kuzalisha umeme wa MW 16 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania, Uganda kuzalisha umeme wa MW 16

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Sep 18, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280  [​IMG]
  Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta


  Serikali za Tanzania na Uganda zimetiliana saini hati ya makubaliano ya kuanzisha mradi wa pamoja wa nishati ya umeme utokanao na maji katika maporomoko yaliyo katika eneo la Murongo mkoani Kagera nchini, ambao utazalisha megawati 16 zitakazotumika katika nchi hizi mbili za Afrika Mashariki.
  Taarifa hii ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mikutano miwili ya mawaziri wanaoshughulika na jumuiya hiyo, iliyofanyika hivi karibuni jijini Arusha na katika nchi ya Rwanda.
  Sitta alisema mradi huu utakaojulikana kwa jina la ‘Mradi wa Murongo –Kigagati utagharimu kiasi cha Dola za Kimarekani milioni nane (Sh. billioni 20),unatarajiwa kuchukua kipindi cha miezi 12 hadi kukamilika mwakani.
  “Kigagati ni eneo ambalo liko katika nchi ya Uganda. Mradi huu utakapokamilika utamaliza matatizo yote ya umeme katika maeneo yaliyo katika mpaka wa nchi hizi mbili na kwamba kila nchi itachukua nusu ya megawati zitakazozalishwa.Fedha za kuugaharimia mradi huu, tumezikopa toka katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB),” alisema.
  Alifafanua kwamba mradi huu ni mfano wa kile ambacho kimekuwa kikisisitizwa katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) ambapo nchi zimekuwa zikihimizwa kushirikiana kuanzisha miradi ya maendeleo ambayo itakuwa na tija kwa wananchi wa nchi za EAC.
  Wakati huo huo Sitta alisema Bunge la Afrika Mashariki limepitisha sheria ya kuanzishwa kwa Taasisi ya mafunzo ya Mabunge ya EA, ambayo itatumika kutoa mafunzo kwa wabunge na wafanyakazi wa Mabunge badala ya kuendelea kutumia fedha nyingi kuwapeleka nje ya ukanda huu kupata mafunzo hayo.
  “Hatukuwa na taasisi ya aina hiyo katika ukanda wetu, na kwa hiyo tulipohitaji kutoa mafunzo kwa wabunge au watumishi wa bunge kwa kozi mbalimbali, ziwe fupi au ndefu tulikuwa tunawapeleka katika mataifa ya nje. Sasa kwa kuanzisha taasisi ya aina hii, itatusaidia sana katika kutujengea mfumo unaofanana katika mabunge yetu,” alisema.

  SOURCE: NIPASHE

   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Duh! mkuu hiyo Mg ni kipimo kipya nini????? anywayz waombe mods wakubadilishie iwe MW
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Mimi huwa sizidishi wala kupunguza nime kopi na ku paste hiyo habari wewe ukitaka nenda kawalaumu Gazete la IPPMedia bonyza hapa utapata hiyo habari Home
   
Loading...