Tanzania tuwe na vituo vya kupimia Coronavirus ili kuokoa utalii

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,578
4,255
Wengi tunajua kuwa Utalii umekuwa na Mchango mkubwa sana kwa ukuaji wa Uchumi wetu na ajira kwa Watanzania

Kutokana na hili Janga la Corona kumekuwa na changamoto kubwa tunayopata kwa mashirika ya ndege na Nchi nyingi za Ulaya na Marekani kuhitaji wageni wawe wamepima nakupata majibu negative ndio wasafiri kurudi kwao.

NASHAURI
Serikali ifungue Kituo (Lab) ya kupima na kutoa majibu ARUSHA ndani ya masaa 12 na pia kuwe na kituo kimojawapo karibu na Dar Airport (Amana?) kipewe uwezo huo.

Naamini kwa kufanya hivyo kunaweza kutuongezea wageni kwa kama 50% kwa kipindi hiki cha mpito

ie: Kwa sasa tunapoteza wageni wengi kwani wanashindwa kuja Tanzania kwa kukosa connection ya namna ya kupima na kupata majibu kwa wakati.

mf: Mgeni yupo Serengeti unamuambia aje Arusha mjini asubiri siku tatu ndio apate matokeo kutoka dar?
 
Back
Top Bottom