Wakubwa mpaka sasa hawataki kuamini kuwa Ziwa Tanganyika linaweza kuleta pato kubwa katika Taifa.mizigo ya Rwanda unafikiri ni mingi kiasi hicho? mingi ni ya Congo, Zambia, malawi, Burundi. Rwanda mingine anapitishia kenya. tunatakiwa pia kutafuta alternative ya mizigo inayoenda eastern congo ili isipite kabisa Rwanda au ipite Rwanda kwa alternative, tutafute namna ipitie burundi au ikatishie kwa meli ziwa Tanganyia. hi i ni kwasababu ugomvi ulipotokea kipindi cha Jk walitupandishia tozo za mizigo inayotoka tz, pia, kipindi hiki cha covid wamenyanyasa sana madereva wetu, na tunatakiwa kutafuta ufumbuzi wa kudumu ili akituona njiani atuheshimu.
Upande wa magharibi ya nchi pamesaulika,na fursa nyingi tumemuachia nchi jirani.
Ushauri:
1.Waziri wa Biashara na uwekezaji afungue ofisi Kigoma,na aende Ufaransa ,Uswisi na Ubeligiji na China awafuate wawekezaji na wafanyabiashara watakao wekeza biashara na viwanda Kigoma kwa ajili ya kuhudumia nchi za Maziwa Makuu(DRC,Burundi,Rwanda na zinginezo upande wa Magharibi ya Tanzania.
2.Waziri wa Fedha aende akafungue Kigoma ofisi ya Benki Kuu ili tununue dhahabu na kurahisisha ubadilishaji wa fedha kwa wafanyabiashara wa nchi jirani kwa upande wa magharibi ya Tanzania.
3.Waziri wa Kilimo aende Kigoma afungue Chuo/Taasisi ya utafiti wa Kilimo,tulime mazao aina mbalimbali kibiashara na chakula yanayoweza kustawi katika ukanda wa Maghatibi ili tuuze nchi jirani upande wa Maziwa Makuu.
4.Waziri wa Uchukuzi aende Kigoma,akakikishe kunakuwa na miundo mbinu inayoweza kutumika kufungua fursa upande wa Magharibi ya nchi.mfano uwanja wa ndege Kigoma uwe wa Kimataifa ili kupunguza safari ya mtu aendae Kinshasa,Lumbumbashi hata Afrika ya Kati.
5.Kwa ujumla kila sekta iende ikafungue fursa upande wa Magharibi ya nchi ili kuongeza ukuaji wa uchumi na biashara na hatimaye kuongeza pato la Taifa kwa upande wa Magharibi ya nchi sawa na Mikoa mingine iliyo katika kanda zingine.
6.Ni suala la Viongozi walio na maamuzi kuamua "Kuharakisha Ukuaji uchumi,biashara na fursa" ili kuongeza ajira na pato la Taifa!