Tanzania tuwe makini na Rais Paul Kagame, siyo mtu wa kuaminika

chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
6,300
15,018
Mzee Mstaafu Kikwete tafadhali mtahadharishe Rais Samia juu ya unafiki wa Kagame maana unamfahamu vizuri.

Kagame ni mtu mbaya sana na yuko radhi kufanya lolote ilimradi apore mali, leo hii taifa lijifunze hatutaki influence ya watu aina ya Kagame tena kwenye nchi yetu.

Kama nchi hatutaki kabisa Kagame na habari zake tena hapa yeye aendelee kuunda waasi wake huko DRC , aendelee kushirikiana na mabebebru kuiba rasilimali za Congo lakini hatutaki yajirudie kwetu hapa.

Hayati Magufuli alifanya kosa kubwa kumwamini.
 
Kwa hiyo milango mnafungua kwa baadhi ya majirani tu? Mizigo yake mnataka ipitie bandari ya dar es salaam hili mpate pesa. Mbona pesa yake hamuikatai? Acheni Rais afanye kazi yake kwa sababu halazimishwi kukubali ushauri /urafiki na nchi yeyote. Mbali na madhaifu yao majirani zetu ni muhimu sana kwa mambo mengi tu.
 
Sio kwamba haaminiki, ni mtu mwenye roho mbaya na hana faida kwa Tanzania. six years ago tz tulikuwa tunaishi kwa furaha, tangu mwendazake atue kwa PK tumeishi maisha ya huzuni na kuweweseka sawasawa na yale wanayoishi wanyarwanda hadi leo. bora sisi tunaye mama hapa ameturudishia furaha kidogo.
 
Magufuli alitapeliwa? Mbona ndo nasikia leo?
Umeitoa wapi hii??
Rwanda ndio nchi inalipa road toll ya dola 152 kwa truck kutoka Rusumo hadi Dar es salaam some good 1200 plus km,
Kwa kawaida Road toll hulipwa kutokana na umbali na kwa 1200 km halali ilitakiwa iwe region ya 500 plus usd,lakini kwa Rwanda protocals zilibadilishwa. Ni kama walipewa exemption ya kutumia barabara zetu bila malipo
 
Kwa hiyo milango mnafungua kwa baadhi ya majirani tu? Mizigo yake mnataka ipitie bandari ya dar es salaam hili mpate pesa. Mbona pesa yake hamuikatai? Acheni Rais afanye kazi yake kwa sababu halazimishwi kukubali ushauri /urafiki na nchi yeyote. Mbali na madhaifu yao majirani zetu ni muhimu sana kwa mambo mengi tu.
mizigo ya Rwanda unafikiri ni mingi kiasi hicho? mingi ni ya Congo, Zambia, malawi, Burundi. Rwanda mingine anapitishia kenya. tunatakiwa pia kutafuta alternative ya mizigo inayoenda eastern congo ili isipite kabisa Rwanda au ipite Rwanda kwa alternative, tutafute namna ipitie burundi au ikatishie kwa meli ziwa Tanganyia. hi i ni kwasababu ugomvi ulipotokea kipindi cha Jk walitupandishia tozo za mizigo inayotoka tz, pia, kipindi hiki cha covid wamenyanyasa sana madereva wetu, na tunatakiwa kutafuta ufumbuzi wa kudumu ili akituona njiani atuheshimu.
 
Rwanda ndio nchi inalipa road toll ya dola 152 kwa truck kutoka Rusumo hadi Dar es salaam some good 1200 plus km,
Kwa kawaida Road toll hulipwa kutokana na umbali na kwa 1200 km halali ilitakiwa iwe region ya 500 plus usd,lakini kwa Rwanda protocals zilibadilishwa. Ni kama walipewa exemption ya kutumia barabara zetu bila malipo
hii kitu ni kwasababu gani? inatakiwa kubadilika haraka iwezekanavyo.
 
Rwanda alifanya nini cha kuiathiri Tanzania?
Magufuli alikosea nini exactly kwenye mahusiano na jirani yake Kagame. Wapi tulipigwa?
 
hii kitu ni kwasababu gani? inatakiwa kubadilika haraka iwezekanavyo.
Mkuu wewe acha tu

Unakumbuka mwendazake alipokuwa waziri wa ujenzi , aliwachukia sana transporters wa Kitanzania kuwa wanaharibu barabara.? Na hii ndo ilikuwa fimbo madubuti ya kuwaadhibu transporters.

Kwa roadtoll ya 152 manake ni kuwa transporters wa Tanzania walionekana ni ghali kupeleka mizigo rwanda . na ndo huu utitiri wa gari za rwanda unauona leo.

Tra wanakosa mapato pia kwa sababu gari ya Rwanda huezi idai , Efd receipt , sumatra etc na wala hawalipi mapato
 
Mkuu ww acha tu
Unakumbuka mwendazake alipokuwa waziri wa ujenzi , aliwachukia sana transporters wa Kitanzania kuwa wanaharibu barabara.? Na hii ndo ilikuwa fimbo madubuti ya kuwaadhibu transporters
Kwa roadtoll ya 152 manake ni kuwa transporters wa Tanzania walionekana ni ghali kupeleka mizigo rwanda . na ndo huu utitiri wa gari za rwanda unauona leo ,

Tra wanakosa mapato pia kwa sababu gari ya Rwanda huezi idai , Efd receipt , sumatra etc na wala hawalipi mapato
Rwanda walitupandishia sisi mizigo tulipie laki tano tunapopitisha kwenda congo, ni baada ya Jk kugombana naye kipindi kile. Mh Samia suluhu anatakiwa apandishe haraka hii kitu kwasababu tunajenga barabara kufaidisha wanyarwanda na pia madereva wetu wanaumia/kosa ajira. Rwanda wenyewe wana faida gani kwetu ya kuwapa exemption? alimshikaje masikio mwendazake huyu jamaa? tuamke.
 
29 Reactions
Reply
Back
Top Bottom