Tanzania tutumie gesi yetu kukwepa vikwazo vya Urusi na Ukraine

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,301
12,600
Athari za vita ya Urusi na Ukraine haitatukosa na inaweza kudumu kwa muda mrefu sana.

Tanzania tumejaliwa kuwa na gesi asilia inayoweza kutumika kwenye magari, machine, na kutoa nishati ya umeme. Sio juhudi wala mikakati ya gesi yetu hii kutumika kushusha presha ya madhara ya vita hivi. Nilitarajia serekali na private sector kufanya yafuatayo:

1. Kutoa msukumo wa kuyafanya magari yote yanayotumia petrol kutumia gesi yetu ili kuepuka gharama za upandaji wa bei za mafuta ya petrol.
2. Kushusha gharama za kufunga vifaa vinavyotumika kwenye ufungaji wa mfumo wa kutumia gesi kwenye magari
3. Kusambaza haraka vituo vya kujaza gesi kwenye magari
4. Kuongeza speed kwenye kubadilisha gesi asilia iweze kutumika kama nishati majumbani/jikoni
5. kununua na kuhifadhi mafuta mengi sana kabla bei hazijapanda juu zaidi.
6, Kuimarisha na kuboresha huduma za usafiri wa umma ili watu wengi zaidi waache kutumia magari yao binafsi
barabarani. Magari haya ya usafiri wa umma yanaweza kupangwa na kuratibiwa vizuri ili kuhakikisha kuwa yanakuwa route, safi na ratiba zinazoeleweka kwa abiria.

Jamani kupanga ni kuchagua, ni heri tusimamishe baadhi ya miradi na kazi ili kupata fedha za kuokoa fedha nyingine sasa.
 
Hatuna gesi yetu!! Gesi iko kwetu lakini siyo yetu! Tulishaiuza kitambo kwa Bei ya mbuzi!! Sana Sana sisi nasi ni wateja!!
 
Back
Top Bottom