Tanzania tusipoacha siasa tutaendelea kuwa wajinga

mzalendo iq1

JF-Expert Member
Mar 10, 2020
1,258
1,541
Habari Watanzania poleni na majukumu.

Kuna kitu kimeniuma leo na kufanya nijiskie vibaya sana juu ya elimu yetu ya Tanzania.

Wasomi wetu kwa namna moja au nyingine wamekua hawaoneshi matunda yao kwetu kama wasomi wa nchi zingine wanavyo fanya japo kwa kiwango kidogo wameweza kujaribu.

Na labda niseme tu, vijana wengi hasa wasom wa Tanzania anapofika chuo tu husahau malengo yake na kuanza kujiingiza kwenye siasa mara atakua BAVICHA au UVCCM. Na kuacha kufatilia taalum yake. Na hata kama msomi wa Tanzania akiamua kusimamia elimu na kuimaliza masomo yake vizuri ataishia kuwa muuza madawa pharmacy au kukaa na vyeti vyake ndani au kama ni ijinia ataishia kufa na stress sababu nchi hii haiongoz na wasomi Ila wanasiasa ndio maana vijana wengi wanajiingiza kwenye siasa sababu serekali wamejaa UVCCM na imeshakuwa ngumu mtu kama sio mwanasiasa kuajiriwa serikalini.

Na Sio CCM tu, hata CHADEMA tayari wana watu wao wanaojua kabisa wakipata nchi wanafahamu nani na nani wanatakiwa wakae sehemu fulani.

Ni aibu kwa nchi kubwa kama Tanzania kushindwa uthubutu na nchi kama Rwanda na Kenya yaani leo wenzetu wanatengeneza mashine za kupumulia wagonjwa sisi tunatengeneza ndoo za kunawia mikono. Kenya wametengeneza sanitizer. Sisi hatujachukua hata hatua moja, yaani Tanzania japo kuna janga ila ni siasa tu ndio zinafanya kazi, yaani hatusikii wataalam wetu wanafanya nini ila tunasikia wanasiasa wakirumbana tu.

Mimi ningependekeza ajira zote za kisiasa mishahara ishuke, pia viongozi wote wa kiserikali wawe maprofesa waliostaafu. sio waandishi wa habari waliosomea Macmillan na Kilimanjaro wakistaafu ndio wanapewa uongozi mzito. Nimesema waajiriwe maprofesa, hiyo itasaidia vijana wengi kujua ili utoboe lazima usome sana na sio kuwa CCM na CHADEMA. Pia ubunge iwe kama ualimu tu, mshahara ukiwa hata laki 7 itakuwa poa na watu hawatokimbilia siasa ila watakimbilia u profesa.

Unamkuta mbunge anajisifu mimi ni darasa la Saba halafu anapokea mshahara Mara mbill au Tatu ya profesa na ruzuku kibao Serikali ijitathmini.

Bila hivi tutaendelea kuwa wajinga wa kutupwa watu wamesha ona elimu bongo hailipi wengi wanakimbilia kwenye siasa tu wakati ilitakiwa tunavyozalisha wanasiasa ndio iwe hivyo hivyo wakati wa kuzalisha wasom wenye tija na taifa
 
Naunga mkono Hoja..Siasa inatumaliza nchi hii kada za kitaaluma haziheshimiwi,Siasa imegeuzwa njia ya mkato kujipatia fedha,utajiri,mali nk badala ya kuwa ni sehem ya mageuzi ya kiuchumi kama taifa..Elimu haina thaman,haina impact ya moja kwa moja kwa taifa kutoa wataalam wa ugunduzi,ubunifu nk imekuwa ya kUjitafutia maslahi binafsi si nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na Sio CCM tu, hata CHADEMA tayari wana watu wao wanaojua kabisa wakipata nchi wanafahamu nani na nani wanatakiwa wakae sehemu fulani.
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom