Tanzania tunayoitaka kama wana wa Israel chini ya Farao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania tunayoitaka kama wana wa Israel chini ya Farao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tyadcodar, Sep 14, 2011.

 1. t

  tyadcodar Senior Member

  #1
  Sep 14, 2011
  Joined: Aug 16, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wana jf hongera kwa kazi,napenda tu kuwambia kwamba msifadhaike sana ndani ya mioyo yenu na jinsi nchi yetu inavyokwenda kwa sababu ni mpango mzima wa mungu.mungu aliufanya moyo wa farao kuwa mugumu ili neno litimie,yaani wana wa isreal waondoke kwenda nchi yao ya ahadi,laiti kama farao angewatreat vizuri wasingeondoka,vivyo hivyo mungu ameifanya serikali ya ccm na viongozi wake wote kuwa na mioyo mugumu yaani hawajali,wanabeza,wanawadharau wananchi na hata kuwafanya hayawani wakifungua mdomo wanaltewa upupu:,epa,kuuza mbuga za wanyama,na mengine yote bila kujali yote hiyo ni moyo mugumu ambao matokeo yake,tulishaanza kuyaona arusha,mwanza,mbeya,iringa na sasa igunga tunasubiri mioyo yao migumu itende kazi, kwa ujumla huo moyo wao mugumu ndiyo utatuletea tanzania tunayotaka
   
 2. delabuta

  delabuta Senior Member

  #2
  Sep 15, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante naunga mkono hoja ni kweli tunaekea kaanani kwa haya mapito tutafika tu mungu ibariki tanzania tufike salaama
   
 3. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,555
  Likes Received: 485
  Trophy Points: 180
  Ni kweli sasa angalau naweza kuona dalili za mjukuu wa mwisho wa mjukuu wa mjukuu wangu wa mwisho kuishi ndani ya Tanzania yenye neema!
   
 4. H

  HAKI bin AMANI Senior Member

  #4
  Sep 15, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye red: Ndivyo ilivyo kwa Jakaya kuwa na moyo mgumu wa kufanya maamuzi magumu, ili neno litimie kama nilivyonenwa na mojawapo wa maaskofu Kwamba JK ni chaguo la Mungu. Mungu amechagua kupitia JK Tanzania iweze kupona. Asante Mungu kwa kuwapofusha macho wasiweze kuona uovu wanaotenda, asante kwa kuziba masikio yao wasiweze kusikia wanapoambiwa uovu wao, asante kwa kuwaacha wajifanye miungu badala yako uliye Mfalme Mkuu wa HAKI na AMANI kwa kudai kwamba AMANI ni sera yao wakati HAKI haipo.
   
Loading...