Tanzania tunamuhitaji Rais wa aina gani 2025?

Kwanza lazima utambuwe watanzania wengi ni vigeugeu just remember Kabla ya uchaguzi wengi wa watu walipendekeza/walipendelea tupate rais mkali na mwenye msimamo thabiti lakini leo wanakengeuka.
Back to the topic~Tanzania inahitaji rais mwenye msimamo kama jpm lakini awe na mtizamo mbali na jpm.Kuwa na rais mfanyabiashara sio case sana lakini kama hana uzalendo ni kazi bure/debe tupu.
Kwa tulipofikia sasa tunahitaji rais ambaye ni mwana falsafa.
Mkuu umenena vyema,nakumbuka akina Mbowe,Mnyika enzi za JK neno "Rais dhaifu,goigoi" na kejeli kibao vilikuwa ndo wimbo wao.Na walitamka wao pia kwamba nchi hii anatakiwa Rais mkali,pia nakumbuka kuna kiongozi mmoja mkubwa wa dini aliwahi kusema nchi ilipofikia inahitaji kiongozi atakayeongoza kwa Mkono wa chuma,leo hao hao pia wameshageuka.Kwa ufupi nchi hii inahitaji Rais mkali.Hawa wa TZ ukiwaedekeza hautafanya kitu chochote.
 
Unaongea usichokijua.
Kuna kampuni nazijua hazikufanya ukaguzi wa hesabu(Auditing) kwa zaidi ya miaka miwili kinyume na sheria zinavyotaka.

Na zilikuwa hazipeleki hesabu za marejesho ya kodi ya ongezeko la thamani au VAT. ( I mean they did not file VAT returns) na kuzituma TRA.

Zilikuwa zinasuasua kulipa Corporate Tax za limited companies.

Kilichokuwa kinafanyika ni kuwapoza tu wafanyakazi wa TRA kitu kidogo kama milioni 3 au 4 kwa kuchelewesha au kutowachukulua kabisa hatua kutikana na kidi wanazodaiwa zinazoanzia milioni 150.

Jiulize hapo serikali inapoteza 150M kwa ajili ya mtumishi wake anavuta 5M na kisha analipwa stahiki zake kibao zinazofikia 4M au zaidi ni faida hiyo kwa taifa?

Hizo 145M anazobakiwa nazo mfanyabiashara ndio ulikuwa unaona vurugu huku mitaani na maendeleo kwa taifa kama miundombinu na madawa au elimu bora hakuna kwa hao masikini(walaji) ambao wametozwa kodi.

Bank kama CRDB zilikuwa jeuri hazikopeshi watu wa chini. Zinakopesha taasisi kubwa na matajiri ili maafisa wa bank wanaowezesha mkopo upite wapate 10% yao. Mwisho wa siku mikopo halipiki kwa wakati na kupelekea majanga kama ya bank ya wanawake.
Ilikuwa deal kutajatisha fedha za serikali. Sasa waone CRDB wapo kwenye list yenye hali tete wakati hawa walisifiwa sana. Lakini NMB iliyokumbatia wanyonge hadi sasa hawajayumba sana labda pesa za mikopo ya waliotumbuliwa vyeti feki ndio zitawasumbua kidogo.

Ule mfumo Kikwetwe ulikuwa unatajirisha wachache na kuifilisi nchi. Ni uchumi bandia ulikuwa unafaida kwa nchi za magharibi na China waliojipenyeza kwetu.

Mkuu hayo madudu machache nasema kitu nilichokishuhudia kwenye corporate business companies. Na bado nipo nashuhudia huku mitaani wanavyoshindwa sasa kujiendesha na kudhibiti nidhamu yao ya matumizi huku wakilipa madeni ya nyuma.

Hali mbaya ya sasa kifedha huku mtaani sio kosa la Magufuli bali ni la watangulizi wake na yeye anapojaribu kutuepusha yasitukute ya Cyprus, Ugiriki na kwingineko tunamrushia lawama za bure.
Kwahiyo sasa anakusanya kodi ya kutosha.. Maafisa hawakunji tena hizo 5 na kuacha 145, ni sawa!

Swali langu; Kwanini mishahara haijaongezwa? Kwanini wastaafu hawalipwi kwa wakati? Aliwahaidi walimu atatoa billion 200 walipe arrears zao, kwanini kawapiga chenga?

Kwanini tukikosoa serikali tunapotezwa? Kwanini aliyepiga picha za expansion joint alibughudhiwa? Kwanini aliyepiga Iramba yuko ndani?

Kama tunauchungu wa kuirekebisha nchi kwanini makosa hatutaki kuyasikia?
 
Swali lilipaswa kuwa Watanzania tunahitaji Rais wa namna gani 2020 maana ndio kuna uchaguzi mkuu.
Haya mambo ya kufanya kuwa eti kipindi ni miaka 10 hayapo ndio maana uchaguzi ni kila baada ya miaka mitano na kwa muenekano wa huyu wa sasa hana uwezo wa kuongeza mingine mitano kwani hii mitatu tuu tumerudi nyuma miaka saba
 
Rais yeyote ajaye ni mbaya kuliko JPM Kama ambavyo watangaluzi wake walivyokua wabaya kulinganisha na watangaluzi wao.

Kutokuridhika ni hulka ya mwanadamu.
Umejib kifalsafa sana ambapo ni akil kubwa inaweza kuelewa
 
Swali lilipaswa kuwa Watanzania tunahitaji Rais wa namna gani 2020 maana ndio kuna uchaguzi mkuu.
Haya mambo ya kufanya kuwa eti kipindi ni miaka 10 hayapo ndio maana uchaguzi ni kila baada ya miaka mitano na kwa muenekano wa huyu wa sasa hana uwezo wa kuongeza mingine mitano kwani hii mitatu tuu tumerudi nyuma miaka saba
Labda kama atatoa kwa njia nyingine lakini si ile ya kura..

Ingawa roho inauma kuyasema hayo..
 
KAMA HUYU WA SASA WATU WANAPIGWA RISASI KILA SIKU HIYO 2025 TUNAOMBA WA AINA YA MABOMU SASA... WATU WAUAWE KWA MABOMU
 
Habarini za Asubuhi wanabodi..

Uzi huu niuandika baada ya kusikiliza kupindi cha Straight Talk Afrika cha Shaka. Jana walikuwa wanaongelea siasa za Afrika Kusini na Cyril Ramaphosa. Binafsi sikuwa namjua Cyril vizuri mpaka alipokwaa madaraka kutoka kwa Zuma. Hapo ndipo nilishawishika kutafuta na kuusoma wasifu wake. Ukiacha mengine mengi, he is a purely businessman.

Tanzania tuna mipango na matazamio mengi mbeleni, tunaitaka Tanzania ya viwanda na ifikapo 2025 tunatazamiwa kuwa nchi yenye uchumi wa kati (Second world country).

Binafsi siamini kama hawa walioko madarakani sasahivi watatufikisha kwenye hata moja kati ya hayo mawili. Kufika huko hatuhitaji kauli za kibabe, sera zisizoeleweka za kuwakandamiza wawekezaji, kujifungia ndani tukiwasubiri mpaka wao waje.

Serikali yetu ya sasa labda inafanya mazuri kwenye baadhi ya mambo ambayo kiukweli ni machache na yanahesabika. Serikali ya sasa imejaa wanataaluma ambao kiukweli hawana background yeyote kiuongozi hasahasa kibiashara zaidi ya kuwa wakufunzi tu.

Mambo mengi yanakwama, viwanda tulivyohaidiwa hatuvioni vinavyofunguliwa vingi kama sio vyote vilikuwa initiated wakati wa Kikwete, wakati huo ilikuwa rahisi kushawishi wawekezaji sababu purchasing power ilikuwepo, hali ya fedha kwenye mzunguko ilikuwa nzuri. Ila sasa, ni wenyewe tu ndio wanajua wanachofanya.

Tukirudi kwenye mada kuu, Je, kwa hapa tulipo na huu mkwamo tunaoupitia bila shaka kwanza tunahitaji Rais msomi lakini pia Rais ambaye amebobea kwenye masuala ya kibiashara.

Hapa haraka lilinijia jina la ALI MAFURUKI. Kwa kiasi kikubwa naona Mtanzania huyu anaweza kutupeleka kule tunakotaka kwenda. Huyu amekulia kwenye buashara na anajua biashara haitaki ubabe, biashara yeyote duniani inataka NEGOTIATIONS, biashara haitaki two faced people. Kwamba leo tunaongea hiki alafu kesho tunageuka.

Kwa mtizamo wako; nani unaona atafaa kuwa mrithi wa JPM?
Why 2025 na siyo sasa!!!? We are tired.
 
Hatujadili mihemko na hearsay.. Tujadili content mkuu. Ni rais gani atatufaa tunapoitafuta Tanzania ya viwanda na nchi ya kupato cha kati?

Kipato cha kati hakiletwi kwa kelele, tunahitaji biashara zishamiri. Sasa kama tunaua biashara, makusanyo ya kodi ni hadithi tunawezaje kufika huko?
Ajae awe Bashe. Naona anafaa sana na hakawa rais, zamuu hii tumpe ni mwenzetu. Anaweza hata kusaidia jinsi ya kupatikana Alshabab wakatuondolea mateso.
Kuna wapiga debe wake wapo, wanalipiga kwa mbali
 
Bashite awe Rais,makamu wa Rais awe mnyeti,waziri wa habari jerry muro,waziri wa maendeleo ya vijana watoto le mutuz jingaz,waziri wa mambo ya ndani salumu hapi bila kuwasahu kina kibajaji,goodluck na wengineo huku chakubanga polepole akiwa mshauri mkuu wa Rais daud bashite
 
Atakaye tuwezesha kuwa na stock kubwa zaidi ya tani million ya dhahabu, na almasi kwenye national vaults (dollar,UK paund, Euro zinalekea kupigwa chini vibaya). Huku akiendeleza na kuongeza idadi ya viwanda vya uzalishaji mali vichakatavyo malighafi za kilimo, uvuvi, ufugaji, uwindaji, kuboresha zaidi miundombinu, za afya, usafiri, elimu. Kuimarisha Vikosi vyetu vya ulinzi kitekenolojia. Kuanzisha kituo maalumu cha masuala ya Sayansi, Uhandisi na Teknolojia (ambacho hakitaingiliwa na wanasiasa na kifanye kazi chini ya 'special branch').

Nina mengi sana ya kueleza kwa uchache naishia hapa.
 
atakayeendeleza mauaji na utekaji ili kupunguza idadi ya watu inayotishia kuleta uhaba wa ardhi
 
Nani alikuambia sisi tunataka Rais sema Ccm 25 -50 watatupa marais wa Aina gani tutakupa majibu
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom