Mkuu umenena vyema,nakumbuka akina Mbowe,Mnyika enzi za JK neno "Rais dhaifu,goigoi" na kejeli kibao vilikuwa ndo wimbo wao.Na walitamka wao pia kwamba nchi hii anatakiwa Rais mkali,pia nakumbuka kuna kiongozi mmoja mkubwa wa dini aliwahi kusema nchi ilipofikia inahitaji kiongozi atakayeongoza kwa Mkono wa chuma,leo hao hao pia wameshageuka.Kwa ufupi nchi hii inahitaji Rais mkali.Hawa wa TZ ukiwaedekeza hautafanya kitu chochote.Kwanza lazima utambuwe watanzania wengi ni vigeugeu just remember Kabla ya uchaguzi wengi wa watu walipendekeza/walipendelea tupate rais mkali na mwenye msimamo thabiti lakini leo wanakengeuka.
Back to the topic~Tanzania inahitaji rais mwenye msimamo kama jpm lakini awe na mtizamo mbali na jpm.Kuwa na rais mfanyabiashara sio case sana lakini kama hana uzalendo ni kazi bure/debe tupu.
Kwa tulipofikia sasa tunahitaji rais ambaye ni mwana falsafa.