Tanzania tunajifunza nini na machafuko yanayotokea kenya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania tunajifunza nini na machafuko yanayotokea kenya?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by HGYTXK, Aug 30, 2012.

 1. HGYTXK

  HGYTXK Senior Member

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hbr zenu wadau,siku za hivi karibuni kumeripotiwa machafuko yaliyosababisha vifo vya polisi na raia kadhaa nchini Kenya.Machafuko haya yalitokea baada ya kuuwawa kwa mwanaharakati wa kiislam ktk mazingira ambayo wananchi wanayashabihisha na mkono wa serikali.tayari yule mwanaharakati alishawahi kutoa dukuduku lake juu ya wasiwasi alionao juu ya maisha yake na tayari alinusulika kutekwa huko nyuma.
  Vitendo vya aina hii vimekuwa vikijitokeza hapa kwetu na vinaonekana kuwa ni jambo la kawaida kwani vifo vya utata vinatokea na kuzimwa kwa kuundiwa tume ambazo hazileti tija yeyote.Sijui ni kutokana na huruma tulonayo waTZ kiasi cha kuchezewa na kuanzishiwa vitu ambavyo wenyewe huviita upepo wa msimu?.Nachelea ipo siku haya yanayowatokea wenzetu yatakuja kutupata pale nyoyo zitakapoota miba za chuki dhidi ya udharimu wa baadhi ya wenye madaraka.
   
 2. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hakuna anayejifunza.watu wamelewa madaraka, ndio kwanza wanazidi kujiimarisha na yeyote anayewapinga anapotea.lakini amini usiamini siku yao yaja, ndipo kutakapokuwa kilio na kusaga meno.Ijapokua wao wanaona hayatawakuta wao.
   
 3. mangikule

  mangikule JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 3,180
  Likes Received: 1,261
  Trophy Points: 280
  Mbegu ya chuki inapandwa pole pole na inamea!! Kenya kuna matukio mawili makubwa!! Hilo la IMAM wa mombasa ni kama la ULIMBOKA!! hapa kwetu lakini hawa wa KENYA walikuwa smart siyo vilaza kama IGHONDU na wenzake.
  Hapa wanasiasa wakitafuta maskini wachache kwenye kabila lao wanawahonga na kuwachonganisha na mauaji yanaendelea. Tanzariver huko trukana wameuawa watu 52 kwa mtindo huu.
  Hii ndiyo style inayoingia TZ kwa kasi. Uchochezi wa kidini unaenda kasi ya ajabu!! usipokomeshwa maafa ni lazima. Wakikabila upo na kama ilivyo huku chuki dhidi ya wakikuyu inaenezwa kwa nguvu zote!! Huku TZ vita dhidi ya wachaga haiwezi kufanikiwa kwa sababu bado haijawa na mashiko ya kihistoria. ILA DINI Mungu apishie mbali............
   
 4. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,785
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Kwa watawala wetu wa sasa hawajifunzi chochote. Kwa maoni yangu serikali zetu ktk eneo hili zinapaswa kupambana na makundi yenye kueneza chuki za kidini na ugaidi. Watawala wa nchi karibu zote za Kiarabu na Kiislamu wanapambana vikali na makundi haya,kwanini sisi tunawachekea hawa jamaa?!
   
 5. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hayo unayosema HGYTXK Mkuu, ni suala la muda tu, lakini tumo njiani na karibu tutafika huko. Viongozi wa Tanzania hawana utamaduni wa kukinga kabla ya kutibu, bila ya kujali kuwa Kutibu kuna gharama kubwa kuliko Kukinga.

  Na kuhusu machafuko hayo hayo ya Kenya ambayo chanzo chake ni Wanaharakati wa Kiislamu, hasa Muslim Youth Centre (naomba wenye nafasi wapitie makala hii: Kituo cha Vijana wa Kiislamu kinalenga kusababisha mapigano ya kidini Kenya, wachambuzi wasema. Sabahionline.com), haya mambo yamekuwa yakijitokeza kwa nguvu Tanzania na serikali ama kwa woga, udhaifu na ulegelege au kwa sababu inafaidika na kugawanyika kwa Wananchi, bado inayafumbia macho.

  Imefika wakati kwa Tanzania kujifunza kutokana na haya yanayotokea Kenya, Sudan, Somalia, Mali Nigeria, Burma na kwengine kote ulimwenguni ambako Waislamu wamekuwa tatizo. Sisemi kama ni tatizo la Waislamu hasa, bali chuki zilizojengwa na Wamarekani kutangaza vita vya wazi na Waislamu wenye siasa kali na mbinu wanazotumia kufanya hivyo. Kwani badala ya kuwashughulikia wahusika (hawa wenye msimamo mkali), wanawaingiza Waislamu wote katika kapu moja na ndio maana kumekuwepo na uadui wa wazi na unaoendelea kukua kiasi ya kugeuka vita vya Waislamu na Wakristo.

  Watanzania, busara zisipotumika na kama hatua za haraka hazikuchukuliwa, tutakuja kujuta. Tusiwafumbie macho watu hawa, lakini nasisitiza busara zitumike tusirejee makosa ya Wamarekani, anagalau katika nchi yetu. Tusibweteke na wimbo wa "Tanzania kisiwa cha amani" ambao sasa hauna kiitikio tena. Kinga ni bora kuliko Tiba.
   
 6. C

  Careboy wamuntere Senior Member

  #6
  Aug 30, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri kuhusu suala la dini naomba niwaombe wakatolic kutokuingilia issues za waislam hasa pale wanapodai mambo fulani kutoka kwa serikali, na kujitangazia kwamba eti wapo wengi kuliko wenzao, sasa kama mmejihesabu ninyi makanisani, na huko misikitini mlipita lini kuwahesabu waislam hadi mkajua wako wachache,? mimi hizi ndo naziona chanzo cha chuki na mitafaruku ktk jamii yetu ya kitanzania, otherwise kama hayo hayatakuwepo basi tutakuwa salama. lkn mkizidi kuwabeza waislam hata kwenye madai yao na serikali ninyi mnakaa kati basi amani tunaiweka rehani. huu ni ushauri kwa serikali, wakatoliki na waislamu. na hakuna haja ya kuleteana chokochoko, kwani binaadam ni huyox2 tu. na ss ni wamoja why tufarakane eti kwa sababu wewe wataka kupata sana kuliko mwenzie hata pale mwenzie anapodai pia hutaki. hii ni tatizo tuiangalie kwa makini. tuwaaachie wanaodaiana wakishindwana basi suluhu itapatikana kwa njia salama zaidi. nawasilisha. na mubarikiwe wote.
   
Loading...