TANZANIA: Tunajifunza nini kwa wababe wa kivita?

Juniour K

Member
Mar 8, 2012
54
5
Kila kukicha jumuiya mbalimbali za kimataifa,vyama vya haki za kibinadamu na mashirika ya kutoa misaada wamekuwa katika harakati ya kumaliza tofauti ndani ya baadhi ya nchi za kiafrika.

Migogoro na vita vya wenyewe kwa wenyewe husababishwa na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na KUTOKUWA NA USAWA KATIKA UTAWALA,KUONGEZA MDA KATIKA UTAWALA,UDAGANYIFU KATIKA UCHAGUZI MKUU,Ukabila,udini na kugombania rasilimali za nchi.
Ukanda wa nchi zilizopo Afrika ya magharibi ndio ukanda ulioadhirika zaidi,mfano wa Liberia,watu wamepoteza maisha na zaidi kubaki walemavu wa kudumu kutokana na unyama uliofanywa aidha na jeshi la nchi hiyo na pengine hata WAASI waliopinga serikali,kwa wakati huo ni dhairi kwamba Afrika iliingiliwa na JINAMIZI linaloitwa katili mara tu Baada ya askari MTIIFU kwa serikali,Sajini Samwel Doe kuipindua serikali na kujitangaza kuwa Rais wa Liberia mwaka 1980.

Kuna usemi usemao "Anayeua kwa upanga naye Atauwawa kwa upanga"ndivyo ilivyotokea kwa Sajini Samwel Doe.

Narudi kwetu Tanzania ingawa hatujashudia wababe wa kivita katika nchi yenye amani na utulivu,nyakati za leo tunashudia:
(a)Kuwepo kwa tabaka kubwa kwa walionacho na wasiokuwa nacho.
(b)wala rushwa wakubwa na wanaoiba mali za walipa kodi,na sheria inapowaona hupindisha mgongo.
(c)wababe wa kisiasa ambao hufikia hatua hata kunuia damu za wengine zimwagike ili wapate madaraka.
Nayasema haya kwa wale wote wenye tamaa ya madaraka ndani ya ccm na nje ya ccm,Msije kuitumbukiza nchi yetu kwenye majanga.
 
Back
Top Bottom