Tanzania tunahitaji Waziri wa Kilimo makini vinginevyo hata hivyo viwanda vitatushinda!

Sera makini za kilimo tunazo!

Watunga sera za kilimo siku ukiwaona mashambani ujue wameenda kwenye mazishi. Na wakijitahidi wanatembelea green house huko goba kwa ajili ya kujiselfie. Sera zitungwe na wakulima maana ndio wanajua changamoto za kilimo na sio hao wauza sura huko maofisini.
 
Bajet ya wizara ya kilimo ni kiasi gani? Msitafute mchawi wakati inaeleweka maamuzi ya mkulu ndio tatizo. Mambo ya viwanda wala usiongelee maana huko ni juu ya uwezo wenu. Kitu mnaweza kufanya kwa usahihi ni kukimbiza mwenge na kulinda muungano kwa gharama yoyote.
Ufipa muungano hamuutaki?
 
Kwa hiyo kilimo chetu ni duni kwa sababu mimea mingi yenye uwezo wa kuua wadudu waharibifu havitumiki? Akili kama hizi ndiyo humaliza nchi hii kabisa.
Nimejibu suala la wataalam; sasa suala la akili limekujaje hapa? Wataalamu tunaowategemea ndo wanashindwa kutumika ili kuinua ubora wa kilimo chetu.
Back to hoja!
Hujui kuwa madawa ya kilimo yanayotengenezwa viwandani yanachangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma ubora wa mazao ya kilimo?
Rejea machapisho ya kilimo hai kuna kitu utajifunza.
 
Kilimo bado ni uti wa mgongo wa taifa letu pamoja na ukweli kwamba mambo mengi yamebadilika huko Duniani kutokana na uwepo wa teknolojia mpya. Hivyo basi kama taifa tunahitaji Waziri makini atakayesimamia sekta hii.Haiwezekani bei ya korosho inachakachuliwa na wizara ya kilimo yenye mawaziri watatu imekaa kimya hadi Waziri mkuu aingilie kati.
USHAURI:
Waziri wa mifugo Mpina Luhaga ahamishiwe Wizara ya Kilimo na Naibu wake apandishwe kuwa Waziri kamili pale Mifugo. Ahsante!
Usiseme hivyo. Mkuu anahitaji kuendeleza kule kuliko sahauliwa. Hahitaji watu wenye uelewa wa kutumikia wananchi
 
Unajichanganya kule Kenya na Uganda sera za kilimo ni tofauti na za kwetu,ndio maana bei za mazao yao ambayo nasisi tunalima tunakimbilia kutafuta masoko huko.Mfano mzuri ni kahawa inalimwa kwa wingi Uganda lakini sisi tunaivusha ya kwetu.Hata Raisi Magufuli amekili kwa hilo.
Nimejichanganya wapi? au wewe ndo hujanielewa?
 
Back
Top Bottom