Tanzania tunahitaji uhuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania tunahitaji uhuru

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Emma M., May 16, 2009.

 1. E

  Emma M. JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi binafsi naona kwamba:-
  Tanzania hakuna uhuru halisi.
  - UHURU unaosemekana kuwa upo ni uhuru wa Viongozi wa ngazi za juu.
  - Viongozi hawa wako huru KUINGIA hadi HAZINA kujichotea mapesa.
  - Viongozi hawa wako huru kutoshitakiwa hata kama uovu wa inajulikana.
  - Viongozi hawa wako huru kutuandikwa mauza uza yao magazetini.
  - Viongozi hawa wako huru kutibiwa hospitali yoyote watakayo duniani.
  - Viongozi hawa wako huru kuwachagua wapambe wao ili kula nchi kilaini.
  - Viongozi hawa wako huru kulindwa na vyombo vya habari.
  - Viongozi hawa wako huru kuuza raslimali za nchi kwa wageni.
  Nini kifanyike wana jamii?

  Emma.
   
 2. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Can I ask? What's ur proposal madam?
   
 3. E

  Emma M. JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaniki,
  Tunahitaji uhuru wa kuwaondolea Viongozi wetu huo uhuru mbaya waliojiwekea.

  Nahitaji mawazo yako pia.
   
 4. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #4
  May 16, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  I see your point. Watu wengi hawaelewi maana ya uhuru. Serikali ndo iko huru. Maana wao ndo wanatunga sheria zinazotubana sisi. Na hivyo sisi tunakuwa kama makondoo, kazi kuburuzwa tu. Ukikaa na kuwa philosophical about it, unaweza ukaanza kulia. Lakini ndo tulichoaamua, kuishi under the rule of law...au sio?
  The argument goes like this:
  Ukipenda maendeleo, lazima muishi binabamu wengi pamoja. Na mkiwa wengi lazima kuwe na sheria za kulindana. Na kukiwa na sheria lazima awepo wa kutunga sheria (bunge), na wa kusimamia sheria(serikali through the polisi, na mahakama). Pia lazima kuwepo wa kusimamia huduma mbalimbali zitolewazo kwa hiyo jamii(serikali). Mwisho, wewe (as an individual) unafuata tu mkumbo, na kuongozwa tu siku zote. Sheria zitatungwa za kuwalinda watawala, wewe utabaki kulipia huduma zako. Usipotaka, basi itakubidi uende kuishi katikati ya mbuga, peke yako bila huduma zozote za jamii kama hospitali, maji safi, umeme, nk. Hii ndio the price of development. Labda upate watawala watakaojali watawaliwa, which is nearly impossible. Ndo maana wanasema POWER IS CORRUPTIVE.

  Wengine wanasema uhuru wako uko katika uchaguzi. But then again...kura zitaibiwa. Sasa sijui uhuru wa mwananchi uko wapi kweli? Good question!
   
 5. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #5
  May 16, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kuiondoa CCM madarakani ni jambo la mmsingi kwanza...it is very manipulative and corrupt...ila kazi ipo..
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  May 16, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mbona uhuru huo tunao? Si tunachagua tena hao viongozi mwakani...au?
   
 7. L

  LaVerite Member

  #7
  May 16, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Emma umetoa chachu kubwa sana, na mjadala kama huu nadhani ndio muafaka kabisa kwa forum hii. Suala kubwa watanzania, na waafrika kwa ujumla tulilotakiwa kulijua ni kuwa viongozi wetu walitusaliti wakati wa uhuru. walikubali uhuru wa bendera uchumi ukabaki mikononi mwa wageni. Kwa maneno mengine uhuru wa kweli haukupatikana. Wakoloni walituchezea ka-mchezo. Walitu-manipulate. Wakawapa viongozi wetu uhuru huku waki warubuni direclty au indirectly kuwa maslhai yao (ya viongozi wetu) yatalindwa. Na viongozi either wakarubunika au wakakubali hivyo. Uhuru wa kweli ulitakiwa kuleta mabadiliko ya kweli ya kiuchumi, kijamii, kisiasa nk. Lakini tangu uhuru mambo yamebadilika kidogo sana na ni hasa hasa mijini. Lakini vijijini kwenye 80% ya watanzania wote hakuna lolote. Ndugu zangu wanaoishi huko ukonongo, Tabora ndanindani hawaoni tofauti kati ya ukoloni na uhuru kwa sbb tangu uhuru hawajafikiwa na umeme wala maji wala huduma za afya, ni juzi tu secondari ya kata imejengwa lkn haina waalimu.

  Kwa ufupi wakoloni weupe walikuwa replaced na wakoloni weusi. Tunachotakiwa kufanya ni kuanza upya jitihada za kudai uhuru kutoka kwa hawa wakoloni weusi. Si lazima tuingie msituni. Lkn lazima tudai haki yetu ya kufaidika na rasilmali zetu. Na tutaweza kufanya hivyo kwanza kwa kuiamsha jamii nzima ya kitanzania, tujue haki zetu na wajibu wa wetu wakufaidika na rasilmali, pili kwa kuuondoa uongozi huu (wa ccm) madarakani kupitia ballot, au civil disobidience, na kuweka watu ambao wataongoza kwa matakwa ya walio wengi na sio wachache. Yote haya yatawezekana ila kama tu watanzania wataamka. Bila watu wengi kuamka itakuwa ngumu. Na media, hasa wakati huu wa media huru (free press) inaweza kusaidia sana. Forum kama hii kama ingewafikia watu wengi ingesaidia kuwaamsha.
   
  Last edited: May 16, 2009
 8. E

  Emma M. JF-Expert Member

  #8
  May 16, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni vema tukajihoji kama kweli tuko huru.
   
 9. E

  Emma M. JF-Expert Member

  #9
  May 16, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyani,
  Uchaguzi wa Tanzania ni kama MAZINGAOMBWE tu.
  Ambao hatuwapigii kura ndio huwa wanashinda.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  May 16, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,649
  Likes Received: 82,379
  Trophy Points: 280
  Karibu sana ukumbini. Nimefurahia kuona hukuchelewa kuanzisha mada hapa jamvini tena hapa kwenye jukwaa ambao labda ndiyo lina umaarufu mkubwa hapa JF. Wengi tutafurahia michango yako ya kuikomboa nchi yetu toka mikononi mwa mapapa mafisadi na Viongozi mafisadi waliowekwa katika mifuko ya mapapa mafisadi na siku zote hawawezi kusema lolote lile baya dhidi ya mapapa mafisadi hao kutokana na kukirimiwa na mabilioni ya pesa za kifisadi baada ya kuifisadi nchi yetu. Karibu sana.
   
 11. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #11
  May 16, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Nadhani Uhuru tunao na umekamilika, lakini kwa unyonge wetu tunashindwa kuutumia ipasavyo.
  Unyonge huu umo miongoni mwetu tulio soma na miongoni mwa wasio soma.

  Unyonge ni pamoja na pamoja na kuamini kwa akili zetu zote kwamba uwingi wa noti mifukoni mwetu ni suluhisha la matatizo yetu.

  Unyonge wa kuthamini sinia la wali, kofia khanga na pishi ya mchele na Thst10,000 kuliko uwezo wako juu ya hati yako ya kupigia kura.

  Unyonge wa kuamini kwamba unyonge wetu ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku.

  Unyonge wa kushindwa kufikiri.

  Uhuru ulipatikana siku nyingi sana lakini tumeshindwa kuuenzi na kuulinda kwa Damu na akili zetu.

  Tukidai Uhuru leo tutadai toka kwa nani?

  Sisi ni koloni la nani?

  Nadhani wa kulaumiwa na kubebeshwa kila kitu ni rafiki na kipenzi chetu tusiyependa kuachana naye hata siku moja, mpenzi wetu UNYONGE.
   
 12. E

  Emma M. JF-Expert Member

  #12
  May 16, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MADELA,
  Huo unaouita unyonge ulitupataje?
  Au tulizaliwa nao?
  Basi tunahitaji uhuru utakaotuondolea unyonge.
   
 13. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #13
  May 16, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Uhuru wa kwanza tunaouhitaji ni uhuru wa mawazo. Wantuendesha kwa kutu chezea akili. Once we are independent thinkers they can't corrupt our minds and when that happens then they can't control us as sheep following the shepherd anywhere he'she leads us.
   
 14. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #14
  May 16, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kumbe hatukupata UHURU mwaka 1961?
  Changamoto kweli kweli.
   
 15. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #15
  May 17, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Unaongea kinyume chake.

  Mwalimu Nyerere aliondoa unyonge wake binafsi kwanza kama mtanganyika, akakubali lolote liwalo na liwe akajiingiza katika siasa na kaamua kutoa mapendekezo ya kubadili maazimio ya TAA ya kudai mambo madogo madogo ya kutaka kujifananisha au kuwa equated sawa na wazungu na kudai uhuru kamili.
  Uhuru jambo kubwa kuliko mambo yote.
  Futa unyonge kwanza kisha Dai Uhuru.

  Aliondoa unyonge kwa kujielimisha.
  Aliondoa unyonge wake kwa kuwaambia watu wengine haki zao kama binadamu.
  Aliondoa unyonge wake kwa kukubali kuacha kazi ya ualimu pale Pugu ilo mpa maslahi makubwa katika mazingira ya unyonge ili kuunganisha nguvu za wanyonge wengi nakudai Uhuru.

  Mtu mnyonge hawezi kusimama mbele ya bwana wake mkoloni na kudai Uhuru, hawezi kufanya hivyo kwa sababu pingu za unyonge wake hazitomwacha.
  Mtu mnyonge hana muda wa kupambana na unyonge wake, ila ana muda wa kufikiria machungu yatakayo mpata, au kile atakacho kosa kwa kuingiza jeuri yake na kujikweza juu ya unyonge.

  Unyonge tumeuvaa kama nguo, wakituambia unyonge wetu unatupendeza tunakubali na tunazidi kuuwekea matarizi juu yake na hata kujivunia.
  Hata hapa JF ukisoma maandiko ya watu wengi tu utaona wazi jinsi wajivuniavyo unyonge wao kwa nguvu zao zote na akili zao zote.

  Ukisikia watu wa kawaida kabisa Tanzania wanapiga stori nakusema kwamba Tanzania ni nchi ya Amani huku wana njaa hawajala tangu jana jioni na sasa ni saa 6 au 7 ya mchana wako nje ya baraza wanapiga stori na mekoni hakuna msosi unajua hawa ni watu waliovaa unyonge na wanajivunia hali yao ya unyonge kwa kujidanganya.

  Ukisha jua kwamba wewe ni mnyonge kazi kubwa uliyo nayo ni kupambanua mambo yakufanyayo kuwa mnyonge.
  kujua tu kwamba wewe ni mnyonge si suluhisho.
  Kuorodhesha mambo yakufanyayo kuwa mnyonge ni hatua muhimu.
  Kujenga mkakati wa kupambana na kila kikupacho unyonge ni muihimu zaidi.
  Muhimu kuliko vyote ni kujitolea muhanga kuingia katika mapambano ya kujitoa katika unyonge kwa kuvunjilia mbali yale yakufanyayo kuwa mnyonge biala kuogopa wala kujali matokeo.

  "Wale jamaa wa vizazi na vifo hawakupi cheti cha kuzaliwa mtoto wako mpaka uwape kitu kidogo"

  Chukua hatua, andika barua kwa kingunge mwenyewe wa vizazi na vifo, toa malalamiko yako rasmi peleka kopi kwa mbunge wako na kwenye gazeti unalo liamini na kama unamwanasheria mtumie.
  Ukikubali kutoa kitu kidogo unadumisha unyonge.

  Mara nyingi tunazidiwa na mchecheto wa hofu ya kuchukuliwa hatua kwa ujeuri wetu wa kudai haki na kukubali hali halisi hata kama kwa namna zote hali ile haturidhiki nayo.
  Haki ni haki yako, lakini mara ngapi katika maisha ya kila siku yasiyohusisha viongozi wa serikali umepata kunyimwa haki??
  Unaweza kunyimwa haki yako kwakupambikwa sifa isiyo yako.
  Mwoga yule.
  Atatufanya nini yule?
  Hebu tumfanyizie tuone atafanya nini!
  Atathubuti ana roho ya kuku yule.
  Wakati mwingine ni lazima sauti yako isisike ili uweze kupata kilicho haki yako.
  Mtu anaweza kumwita mkeo chemba na kuanza kumtongoza huku wewe unasikia wazi wazi, kwa sababu shati la unyonge lime kukaa vyema unajifanya hujui kinachoendelea.
  Fedha yake, Msuli na ukubwa wa kifua chake wala cheo chake kamwe visitumike kuendeleza unyonge wako.

  Kule Busanda wananchi wanazomea viongozi wa CCM.
  jiulize kwa nini?
  Watu wale wametambua kwamba kila siku wanadanganywa kwa ahadi za uongo kwa sababu wao ni wanyonge. Ili kukomesha aina yote ya uongo, mara kiongozi akianza kusema uongo watu wanazomea.
  Zamani tuliamini kabisa kwamba tukimzomea kiongozi wa kitaifa nguvu zote za serikali zitatuangukia kma wimbi la Sunami.
  Kwa kutambua kwamba unyonge wetu ni vazi la manyasi tuwezalo kulivua tukitaka, tumeanza kujenga utamaduni wa kuwapa majibu yao viongozi wote wanaothubutu kuendelea kututia katika unyonge.

  Tuna wabunge wengi sana pale Bungeni ni wanyonge kuliko Bibi yangu kule Malinyi.
  Wametumwa kwenda kuwasemea wananchi ili kuharakisha maendeleo yao, lakini wamefika kule, wamegawiwa au kuvishwa majoho yaunyonge na kushindwa kujenga hoja nzito dhidi ya ujuha mwingi ufanywao na watendaji wa serikali na mashirika yake.

  Mbunge mara zote anafanywa mjinga kwa kupewa nafasi za hapa na ple katika vyombo fulani iliaendelee kupata per DM na sitting allowance.
  Wabunge jeuri hunyimwa nafasi za kuwapa kipato cha ziada, ukiwa jeuri sana wanakupa nafasi ili wapate kukumaliza kama wanavyo jaribu kummaliza bwana mdogo Zitto.
  ( Zitto bado nakuamini endeleza moto)

  Unaweza kuvaa suti pande tatu lakini bado u mnyonge.
  Unaweza endesha VX na GX za nguvu lakini bado u mnyonge.
  Kile kikuzuiacho kutumia nafasi yako uwezo wako kama mtu kama mwakirishi kama sheikh kama padri kusema ukweli hadharani ndicho kikupacho unyonge.

  Kile kitupacho unyonge mara nyingi tumedhani ndicho kitupacho shibe na raha kidogo tuliyo nayo. Kwa kudhani hivyo mara zote nafsi na hisia zetu zimeshindwa kuturuhusu kupambana na unyonge wetu kwa sababu kupambana na unyonge wetu ni kama kupambana na kile kitupacho na kilindacho uhai na utu wetu.

  Amen
   
  Last edited: May 17, 2009
 16. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #16
  May 17, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  MADELA WA MADILU,
  Nakupongeza kwa jinsi ulivyo yawakilisha mawazo yako.
  Hata kama sikubaliani nayo yote, umeyawakilisha kiufundi sana.
  Ningeweza ningekushawishi uandike KITABU kuhusu UHURU na UNYONGE.
   
 17. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #17
  May 18, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,592
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280

  supported;

  unyonge, kutokujali, kutakufikiria vizazi vijavyo, kuridhika ma kukosa uzalendo, uhuru hupo, ndio maana watu wanaokula rushwa wanwatumia tunaosema hawana uhuru, wana uhuru wa kukataa na tukawa nyuma yao!
   
 18. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Unyonge ni hatari kweli kweli.
   
 19. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tukiweza kufika mahali ambapo nafsi ya ndani inaweza kuwakilishwa na maneno na matendo ya ubinadamu wetu, tukifika ambapo mawazo yetu yanaweza kushabiana na vitendo vyetu, tukifika mahali ambapo imani zetu zinaweza kubebwa na uhalisia wetu, tutakuwa tumeanza kuishi katika uhuru wetu.
   
 20. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  PETU,
  Falsafa yako ni kali.
  Tutafika lini?
  Ni ngumu kama ngamia kupenya katika tundu la sindano.
   
Loading...