Tanzania tunahitaji mjadala wa kitaifa kuhusu maana ya ndoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania tunahitaji mjadala wa kitaifa kuhusu maana ya ndoa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andindile, Jul 20, 2009.

 1. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ndugu wana JF Tanzania kama taifa linahitaji mwongozo. Hivi sasa imefika wakati viongozi wetu watukalishe chini watanzania wote ili tutatafute maana ya neno NDOA na tukilipata na na kura ya maoni ipitishwe ili kukubaliana na maana hiyo au la, na wengi wakakubaliana nayo, iingizwe kwenye katiba ya nchi kama sehemu ya mwongozo wa jamii yetu ya Tanzania. Na vijana wafundishwe maana hiyo mashuleni na majumbani. Nasema hivi kwa sababu ipo hatari ya kuipelekesha puta nchi yetu kiasi kwamba itapoteza mwelekeo. Si mmesikia kuwa vikundi vya kutetea mashoga wameishtaki serikali kwa kuwanyanyasa mashoga na wasagaji?

  Kumbukuka bila kuwa na misingi imara ya kuliongoza Taifa tutayumbishwa mpaka basi na 'haki' wanazobuni wenzetu kila kukicha. Pia sio kila kinachoanzia Ulaya au marekani ni sahihi kwa jamii zetu.

  Nawasilisha
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Jul 20, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mjadala wa kitaifa wa nini wakati Sheria ya Ndoa imetoa maana ya ndoa? Na kwa nini unafikiri kiwekwe kwenye Katiba? Maana siku hizi viongozi wetu hawaiogopi hata hiyo Katiba wanajihusisha na kutangaza dini hata bungeni, ukidefine upya ndoa na kuweka kwenye katiba ndio itasaidia nini? Au unataka kuchomekea mambo ya kadhi kiaina kwenye thread hii?
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hakika hayo yamebainishwa wazi katika Katiba ya Tanzania na ile ya Zanzibar katika sheria za Ndoa.

  Na ndoa imefasiriwa vizuri sana humo. Ingawa kidigo ina mapungufu kidogo hususan umri wa mtoto wa kike kuolewa lakini inakidhi kwa jamii ya sasa
   
Loading...