Tanzania tunahitaji dictator

Felixonfellix

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
1,672
182
Tanzania tunahitaji dictator, mwenye nia ya maendeleo, ili wote tuingie kazini tuache malumbano na hoja ambazo kwa ujumla ni za kupoteza muda.

Tumpate wapi kiongozi dictator asiye na huruma hata kidogo kwa kiumbe yeyote wa Tanzania mwenye uwezo wa kufanya kazi anazembea. Asiye fanya kazi ahukumiwe kwenda jeshi la mafunzo akafanye kazi kwa lazima.

Mfumo wa Jeshi la mafunzo uwe na msisitizo wa kufanya kazi zote za maendeleo. Kila mtu ajitathimini ana mchango kiasi gani katika maendeleo yake na ya jamii inayomzunguka.

Huku kwenye JF yameandikwa mengi sana, hebu tuamue kufanya kazi kwa bidii na sio maneno mengi yanachosha.
 
Wala haina haja ya dikteta, ni kupata mzalendo atakayehakikisha sheria tunazojiwekea zinazingatiwa.

Wa kuvipa vyombo/idara husika mamlaka ya kufanya kazi bila kuingiliwa wala yeye kuziingilia.

Asiye na tamaa ya yeye na jamaa zake kujirundikia mali, ahakikishe mali za watanzania zinatumika kwa ajili ya Tanzania.

Mwenye kutambua majukumu yake, asiye na simile kwa yeyote anayebainika kuliingiza taifa katika hasara na fedheha ya aina yoyote ile.

Mwenye kutambua kuwa Tanzania ni zaidi ya chama chake na dini/imani yake. Asiwabague watanzania kwa imani/itikadi zao bali awe tayari kuwasikiliza wanaomkosoa na kuyatafutia ufumbuzi yanayoongelewa na wanaomkosoa (kama kuna ulazima) bila kuwapuuza kwa maneno rejareja.

Mwenye kuhakikisha nchi inakuwa na miiko yake, aisimamie na kuhakikisha tunapata heshima ndani na nje ya taifa letu.

Mwenye kuwajibika, awe tayari kufa kwa ajili ya watu wake.

Mwenye kumbukumbu ya aliyowahi kuahidi/ongea kwa wananchi yake na kuyatekeleza.

Mwenye uchungu na nchi yake, ailinde dhidi ya kashfa zozote za kifisadi, ailinde nchi dhidi ya maadui 'maradhi, ujinga na umasikini'.

Na mengine mengi mengiiiiii.

Udikteta si wa kuombwa, tukimpata dikteta tutaanza kuomba 'wahisani' kumwondoa!
 
tunahitaji chama cha kikomunist kama cha china! nyonga mafisadi wote + wala rushwa...
 
BTW: Rais huyo tumwandae sisi! Wakati ni huu!

Tukiamua tunaweza, hatuna sababu ya kutaka kutawaliwa, tunaweza kumwandaa mtu tunayemtaka, tunaweza kumkataa yeyote wanayetaka kutulazimishia na tukawakata ngebe 2015 (hata kabla ya 2015).

Tusikubali kupangiwa na 'yeyote' juu ya nani awe rais wetu. Tusikubali kulazimishiwa wa kuongoza taifa.

YES, wananchi ni zaidi ya mahakama, katiba na sheria! Kama vyombo hivi na sheria haviwasaidii wanaweza kuchukua maamuzi sahihi
 
Ni kweli Invisible, lakini taifa letu halina watu jasiri kiasi hicho. Wananchi wengi hatujajengewa uthubutu huo wa kufanya maamuzi magumu.

Ndiyo walewale hata wakishika madaraka makubwa wanashindwa kufanya maamuzi magumu ingawa madaraka wanayo. Binafsi nisingetegemea kiongozi kama Waziri Mkuu awe naye katika watu wanaolalamika tu eti mambo hayaendi. Bado tuna safari ndefu kwa wananchi (kwa maana ya Umma) kutambua nafasi yao katika uongozi wa nchi.

Anyway, tunashukuru CDM iliyoanza kuwapa watu ujasiri wa kudai haki zao. Ngoja tuone mwisho wake.
 
Nchi karibu zote zilizotawaliwa na Madikteta mwisho wake ziliishia katika Vita, mfano rahisi ni jirani zetu Uganda kipindi cha Dikteta Nduli Fashisti Idd Amin Dadaa, n.k,n.k

Hatuhitaji kuongozwa na Dikteta, Nchi hii mimi bado naamini inao Viongozi wazuri, wazalendo, wanaochukia Ufisadi na Rushwa, wacha Mungu, Wenye kuchukizwa na Umaskini tulionao ilihali tunazo Rasilimali lukuki, Wenye Dira na Dhima.

Viongozi wa namna hio hapo juu, ongezea na alioandika Invisible hapo juu, mimi naamini Tunao. Uchaguzi ukija tena tuwachague hao, na Si vinginevyo.

Mungu ibariki Tanzania
 
Siyo awe dictator, hata kwa demokrasia tunaweza kumpata rais makini, mwenye nia ya maendeleo, asiyebabaishwa wala kuhongwa kwa dhahabu, mavazi, pesa, mwenye uzalendo wa kweli kwa nchi yake na asiyetoa nafasi ya upendeleo kwa marafiki na wapenzi!!

TUKIAMUA INAWEZEKANA!!!NCHI NI YETU SOTE
 
Tanzania ni mali ya watanzania,tukithubutu tunaweza fanya sisi,kweli tunawatuwengi sana wenye nia ya maendeleo,ambao wanachukia ufisadi ndani ya mioyo yao!

Kuwa na rais dictator siyo suluhisho, maana wengi nao ni mafisadi!!! Tutumie demokrasia ili kupata kiongozi makini kwa maendeleo ya nchi yetu
 
Wala haina haja ya dikteta, ni kupata mzalendo atakayehakikisha sheria tunazojiwekea zinazingatiwa.

Wa kuvipa vyombo/idara husika mamlaka ya kufanya kazi bila kuingiliwa wala yeye kuziingilia.

Asiye na tamaa ya yeye na jamaa zake kujirundikia mali, ahakikishe mali za watanzania zinatumika kwa ajili ya Tanzania.

Mwenye kutambua majukumu yake, asiye na simile kwa yeyote anayebainika kuliingiza taifa katika hasara na fedheha ya aina yoyote ile.

Mwenye kutambua kuwa Tanzania ni zaidi ya chama chake na dini/imani yake. Asiwabague watanzania kwa imani/itikadi zao bali awe tayari kuwasikiliza wanaomkosoa na kuyatafutia ufumbuzi yanayoongelewa na wanaomkosoa (kama kuna ulazima) bila kuwapuuza kwa maneno rejareja.

Mwenye kuhakikisha nchi inakuwa na miiko yake, aisimamie na kuhakikisha tunapata heshima ndani na nje ya taifa letu.

Mwenye kuwajibika, awe tayari kufa kwa ajili ya watu wake.

Mwenye kumbukumbu ya aliyowahi kuahidi/ongea kwa wananchi yake na kuyatekeleza.

Mwenye uchungu na nchi yake, ailinde dhidi ya kashfa zozote za kifisadi, ailinde nchi dhidi ya maadui 'maradhi, ujinga na umasikini'.

Na mengine mengi mengiiiiii.

Udikteta si wa kuombwa, tukimpata dikteta tutaanza kuomba 'wahisani' kumwondoa!

Mkuu nchi hii hakika inataka dikteta.

Ukisoma historia utabaini kwamba wenzetu wa Ulaya ambao nchi zao zina maendeleo utakauta lazima walipitia udikteta na kutwangana. Wengine walipitia uharamia kama ilivyo sasa hivi kwa Somalia. Mkishapitia hatua zote hizo mnaketi chini na kuamua jinsi ya kuongozana kidemokrasia kwa kuwa baada ya udikteta ama kutwangana mtakuwa mnaheshimiana na kuogopana. Nchi zetu kwa bahati mbaya hazikupitia udikteta kama ule wa Musolin, Hitler, Mao ama Stalin tulikuw atunasema udikteta wa Chama kimoja lakini si udikteta wa kulazimishana kufanya kazi.

Nchi kama Tanzania haijapitia udikteta kwa hiyo imeruka process moja ya maendeleo inabidi tupate Dikteta atunyooshe kisha tukae chini na kuandaa utaratibu wa kuongozana kwa njia za kidemokrasia na siyo kukimbilia demokrasia ambayo haina tija kwa wananchi!!
 
Huku kwenye JF yameandikwa mengi sana, hebu tuamue kufanya kazi kwa bidii na sio maneno mengi yanachosha.
Mkuu mbona tunafanya kazi sana tu! Kama unaangalia/ unaandika/ unasoma tu Jf bila kufanya kazi au kuyafanyia kazi maoni yetu humu, basi jf haina faida kwako!

Kuhusu Dikteta, mi sidhani kama tumefikia hapo! Tunahitaji viongozi wazalendo wakweli, wenye kutanguliza maslahi ya taifa mbele, not selfish, wenyefikra za kisasa za demokrasia na maendeleo. Na kwa maoni yangu, hapa tunamhitaji Mh. Dr. (Phd) W. P. Slaa.
 
Back
Top Bottom