Tanzania tuna uhuru wa habari, ila media oga! Tungekuwa mbali sana kimaendeleo, rushwa, uhujumu, ufisadi, ubadhirifu vingeibuliwa kabla

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
32,844
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
32,844 2,000
Wanabodi,
wale wenye access angalieni Star TV, kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari kinachorushwa live na Star TV, kila siku za Jumamosi asubuhi, leo Mtangazaji Mahiri, Leonard Mapuli yuko na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Press Clubs, UTPC, Aboubakar Karsan, anamwaga nondo za kufa mtu, kwanza kwa kuwaita baadhi ya viongozi ni "Vichwa Maji".

Aboubakar Karsan, anasema Tanzania tuna sheria nzuri inayotoa uhuru mkubwa wa habari tatizo ni Tanzania hatuna Media zenye uwezo wa kuutumia ipasavyo uhuru tulionao, amesema Tanzania tuna media iliyojaa uoga katokana na kuwaogopa viongozi vichwa maji!.

Karsan anasema, media ya Tanzania, ingeutumia vizuri na kikamilifu uhuru tulionao, Tanzania tungekuwa mbali sana kimaendeleo, kwa sababu vitendo vya rushwa, uhujumu, ufisadi, ubadhirifu na madudu yote yanayoibuliwa kwenye ziara za Mhe. Rais, vingeibuliwa kabla na serious media na sio kusubiri hadi rais afanye ziara ndipo madudu yaibuliwe.

Aboubakar Karsan, anasema ile kauli ya rais, John Pombe Joseph Magufuli kuvionya vyombo vya habari kuwa "Watch out, you are not that free", ilitolewa kwa nia njema, kuwaasa media kuwa hakuna uhuru usio mipaka, na kila haki inaadamana na wajibu. Kupitia kauli hii, baadhi ya wasaidizi wa rais wakiwemo mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya, ambao amewaita "vichwa maji", wakaitafsiri vibaya kauli hiyo, na kuanza kuvibinya vyombo vya habari na kuwabinya waandishi wa habari, ikiwemo kuvifungia vyombo vya habari na kuviadhibu.

Karsan anasema, haungi mkono fungia fungia ya vyombo vyombo vya habari yakiwemo magazeti ni kuwanyima haki haki wananchi wanaotegemea media hiyo kupata habari, ameshauri zitumike adhabu mbadala.

Karsan anasema, uhuru wa kweli wa habari, uanzie ndani ya vyombo vyenyewe vya habari, kwa wamiliki wa vyombo vya habari, kuwalipa vizuri waandishi wao, wawape haki zote za msingi za wanahabari, ikiwemo vitendea kazi bora, mazingira bora ya Kazi, bima ya afya, kinga maalum kwa waandishi wa habari za kiuchunguzi. Baada ya waandishi kupata haki zao na stahiki zao newsroom ndipo sasa tukatafute hiyo haki nje ya newsroom kwa kusisitiza sheria, taratibu, na kanuni zifuatwe.

Karsan anasema kuna waandishi wa kweli wa habari, na wanaharakati wa kihabari, kazi za uandishi wa habari, sio uanaharakapti za kihabari, ila amekiri kwenye media kuna sera za media za kihabari na media za ki propaganda na za kiharakati, akatolea mfano gazeti la Uhuru, tangu usajili wake ni gazeti la propaganda ya Chama cha Mapinduzi, hivyo likiandika propaganda yoyote ndiko kutimiza wajibu wake. Lakini vyombo vya kawaida vya habari, vinatakiwa kuwa impartial kwa kuripoti balanced news. Amelaani magazeti huru kujigeuza vyombo vya propaganda za vyama Fulani akatolea mfano gazeti la Tanzania Daima ni gazeti huru, likifanya propaganda ya Chadema, ni kinyume cha sera ya gazeti hilo.

Hitimisho.
Karsan anasisitiza, Tanzania tuna Uluru mkubwa wa habari kwa mujibu wa sheria, unakwamishwa na viongozi vichwa maji, na media zenye uoga, hivyo amesisitiza media tutimize wajibu wetu bila uoga kwa mujibu wa sheria, tukiacha uoga, tutaisaidia sana serikali, tutaisaidia jamii na kulisaidia Taifa.
Asanteni kufuatilia.
Paskali
Rejea 

mulwanaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Messages
3,490
Points
2,000

mulwanaka

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2017
3,490 2,000
Uhuru wa kutowa habari upo ila very 'selective' sana unaweza kua huru kusema lolote kama humgusi raia number one na kazi zake, tuwe wa kweli hamna mtu anaweza kuthubutu kuhoji jumba jeupe, kama utaratibu na ununuzi wa ndege, pesa inayo tumika kununua wapinzani ujezi wa Airport ya chato na Bandari yake, nk....
 

Castr

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Messages
15,508
Points
2,000

Castr

JF-Expert Member
Joined Apr 5, 2014
15,508 2,000
Aulizwe kama anaijua Jamii Forums. Aulizwe kama anajua kua JF inaripoti mahakamani ikishinikizwe ifanikishe kutambulika kwa member aliyeonyesha madudu ya Oil Com bandarini.

Aulizwe kama anajua kua ili uweze kuripoti habari kwa njia ya mtandao, blog au vlog, unahitajika uwalipe TCRA? Kinyume na nchi zingine.

Anajua kua kuna muswada ukisimamiwa na Nape ulitaka vyombo vyote vya habari viwe vinapokea matangazo ya habari kutokea Televisheni ya Taifa?

Kama hayo yote anayajua na bado atasema Tz tuna uhuru wa habari basi ni kweli tuna uhuru wa habari.

NB. Wakati mwingine naona unaandika neno Gandhi samahani naomba nijue maana yake. Mfano leo umeandika '... Gandhi ya viongozi..:
 

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
12,654
Points
2,000

Mystery

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
12,654 2,000
Yaani Rais alipowaambia wakuu wa vyombo vya habari kuwa "watch out you are not free to that extent" eti hakuwa na nia ya kuviminya vyombo vya habari kweli??

Nimeamini katika awamu hii kila mtu Tanzania analazimika kujiunga na "praise and worship team for Magufuli" ili mradi tu mkono uende kinywani......

Anaweza,kutuambia ni kwanini magazeti ya uchunguzi ya Mwanahalisi na Mawio yalipata kifungo cha maisha??

Je anayafahamu masahibu yanayomkabili Max Mello, mmiliki wa Jamii Forum, huko mahakamani??

Utawezaje kuita tuna Uhuru wa vyombo vya habari, wakati juzi tu Amnesty International na Human Rights Watch wametoa ripoti yao kuwa Tanzania kuna uminyaji mkubwa sana wa vyombo vya habari??

Nchi hii tuna vyombo vya habari vingi vilivyojiunga na "praise and worship team for Magufuli" na chombo cha habari ambacho kitafanya "kiburi" cha kutojiunga kumsifu na kumwabudu Mheshimiwa, hakika kinajitia kitanzi........

Huyo jamaa ategemee kupewa uteuzi na Mheshimiwa kwa nafasi ya uDC au uDED
 

VAPS

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2012
Messages
3,169
Points
2,000

VAPS

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2012
3,169 2,000
Tatizo kubwa kwetu bado tuna utawala wa Kifalme kiuhalisia. Wapambe wa mfalme hawawezi mwacha salama mwanahabari anaetoa taarifa sahihi isiyosifia juhudi.Rejea misukosuko mfano reporter Itv njaa Kagera.Wanahabari pia wanapenda bahasha kwa njaa zao.
 

LIKE

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2013
Messages
3,404
Points
2,000

LIKE

JF-Expert Member
Joined Dec 17, 2013
3,404 2,000
Karsan anasema, Uluru wa kweli wa habari, uanzie ndani ya vyombo vyenyewe vya habari, kwa wamiliki wa vyombo vya habari, kuwalipa vizuri waandishi wao, wawape haki zote za msingi za wanahabari, ikiwemo vitendea kazi bora, mazingira bora ya Kazi, bima ya afya, king malum kwa waandishi wa habari za kiuchunguzi. Baada ya waandishi kupata haki zao newsroom indigo sasa tukatafute hiyo haki ya née ya newsroom.
P

Mzee kanywe supu ya kondoo..bill nitalipa jioni,pindi nikitoka kwenye mishemishe

full kuchapia.!

au ndio mambo ya Autobots/robot.?
 

Masiya

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
6,181
Points
2,000

Masiya

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
6,181 2,000
Aboubakar Karsan, anasema Tanzania tuna sheria nzuri inayotoa uhuru mkubwa wa habari tatizo ni Tanzania hatuna Media zenye uwezo wa kuutumia ipasavyo uhuru tulionao, amesema Tanzania tuna media iliyojaa uoga katokana na kuwaogopa viongozi vichwa maji!.
Kuna sheria, kuna utekelezaji wa sheria, kuna kutafsiri sheria, na kuna vitendo ambavyo badala ya kuvishughulikia kisherai watu (hao vichwa maji) wanajitungia sheria zao na kutekeleza. Tumuulize Mwangosi huko aliko, check na Kibanda, ongea na Kubenea, Azory Gwanda yu wapi, magazeti mangapi yamefungiwa hata bila kesi. Ukipenda pia muulize Paskalli Mayalla hatujui yaliyomsibu mbele ya Ndugai (ni siri yake sidhani kama atakuja kutujuza). Sheria za habari na cybercrime zote zinawahusu. JF chini ya Mello isingekuwa ngangari saa hizi tungetafutana (wee acha tu). Si mwana habari lakini sidhani kama wanahabari wetu ni mapopoma waogope kivuli chao, wanajua nini chaweza kuwafika na bado hawajaona nani wa kuwatetea. Pia tusisahau wapo ambao kwa hiari yao au ajira zao wao ni kuimba mapambio na hawa pia huwakatisha tamaa wale ambao wangetaka kujaribu.
 

ForeverMore

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2014
Messages
509
Points
1,000

ForeverMore

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2014
509 1,000
Hivi Max mmiliki wa JF alishinda kesi yake mahakamani?

Kama alishinda ina maana tuna sheria za kuwalinda waandishi wa habari.

Tatizo ni kama mtoa mada alivyosema, kuna viongozi wanazingua kitu ambacho kina changanyika na uoga wa waandishi wa habari na kuto lindwa na wamiliki wa hivyo vyombo vya habari.

Kwa wenzetu, mlinzi wa kwanza wa mwandishi wa habari ni shirika la habari analolifanyia kazi. Lipo tayari kusimama na mwandishi wake hata mahakamani.

Pia umoja wao unawalinda, ukimgusa mwandishi wa habari mmoja hata kama ni wa media pinzani, wengine wote wana shambulia.

Tatizo letu, tunataka tupewe haki, yaani tuna bembeleza na kulilia. Ni sawa na kumbembeleza mdeni wako akulipe.

Uwezi kukaa kutarajia mwanasiasa akusaidie bila kuangalia masilahi yake kwanza, hakuna kitu kama hicho.

Kwa asilimia kubwa siasa na uandishi wa habari haupatani, ni wapinzani. Sasa hivi siasa inaidharau uandishi wa habari. Bila waandishi wa habari kutengeza heshima mtabaki mnalia milele. Lazima ifike mahali siasa iwaheshimu, iwaogope. Na hiyo haiji kwa kuwalilia na kuwaangukia chini ya miguu yao.

Tangu lini Arsenal ikaiomba Man u isiwafunge wagoli mengi? Ni kupambana.

We unakaa unatarajia bosi wako ipo siku tu ataamua kukuongeza mshahara? Lazima umtikise.

Waandishi wa habari angalieni ni jinsi gani mnaweza fanya muogopwe na wana siasa. Mmoja wenu akikamatwa msinyamaze, ongezeni sauti. Hii ni vita sio mchezo wa kutekenyana.
 

Siwamilele

Member
Joined
Oct 22, 2019
Messages
38
Points
125

Siwamilele

Member
Joined Oct 22, 2019
38 125
Yaani we Paskali, unashikiwa akili na huyo Karsani kirahisi hivyo? Bado ninaimani na hoja zako nyingi Lakini ktk hili hapana buana. Huyo katumwa tu na kitengo cha propaganda cha jiwe ili kutuliza hali ya mambo kufuatia mvua ya mashambulizi ya Amnesty..... na Human.......!
 

Forum statistics

Threads 1,379,902
Members 525,619
Posts 33,760,608
Top