Tanzania tuna protocol za ovyo kabisa kwa Viongozi wetu

instagram

JF-Expert Member
May 27, 2014
2,091
4,716
Yaani kiongozi anashuka kwenye gari anazungukwa na minders zaidi ya hamsini wengine wananing'inia kwenye milango, hadi kiongozi anaenda kukaa jukwaani kaambatana na minders zaidi ya 20 wanamzunguka hadi anakaa na bado kuna wanamsimamia kwa nyuma, kwa hatari gani aliyokuwa nayo kiongozi wa nchi masikini kama Tanzania hadi awe na ulinzi mkubwa kuliko kiongozi wa marekani au uingereza aliyekuwa na bifu kubwa na makundi kibao ya ugadi duniani?

Yaani unashangaa Joe Biden anshuka kwenye gari hadi anaenda kukaa jukwaani Yuko peke yake na mke wake na hadi anakaa hakuna jitu lina mpumulia nyuma.

Unashangaa hata malkia wa uingereza anashuka kwenye range rover yuko peke yake na kibegi chake kiwikoni anatembea zake hajazongwa na kundi la wapambe wala ushuzi ila sasa sisi watanzania sijui ni nani alianzisha utaratibu huu wa ajabu kwa viongozi wetu kuandamana na utitiri wa watu Hadi wengine wamevaa magwanda kijeshi na mabunduki nje nje hii kitu haikuwepo enzi za nyerere wala mwinyi.

Sijui ni nani aliingiza utaratibu wa kuonesha kana kwamba kiongozi ana maadui wengi kiasi cha kuhitaji idadi kubwa ya kutisha ya wapambe na mibunduki hadharani ambapo zamani silaha ulikua huzioni hadhara kwa viongozi ila unahadithiwa zipo viunoni.

Nahisi kuna watu wanaohusika walianzisha utaratibu wa kuajili ndugu zao kwa kuwajaza kwa viongozi mpaka ikaja kuwa normal kwa viongozi kuzungukwa na wapambe wengi kupita uhitaji.
 
Wazungu huwa wanatucheka Sana , tupo bado Zama za WW2 , kuna mtu alijitengenezea ulinzi wa mabunduki kila angle , lakni Wana wakamtupia kirusi cha COVID huku wanakula 🍿kirusi kikamaliza mchezo ...... Now day biological weapon ndo imeshamiri
 
Tanzania tunafanya kazi kwa kutumia nguvu

Rais Magufuli aliyelindwa kama Mungu yuko wapi? Tulinde afya, tumlinde rais kwa ndani sio kwa nje.

Hatuna mifumo wa taasisi imara

Tukiwaambia tunahitaji katiba mnabisha nchi inahitaji katiba itakayoweka miongozo ya kila jambo linalofanyika katika nchi na kutengeneza mifumo imara ya kiuongozi.
 
Yaani kiingozi na msafara wa magari mia anasimama kijijini ambapo watu hawana hata manati ila sasa kazungukwa na mabunduki ya kivita zaidi ya hamsini anahutubia wanyonge unajiuliza anawaogopea nini wanyonge hawa? Angalau basi angewaamuru jamaa wafiche silaha ndani aongee na wanyonge wake kwanza duh?
 
Tatizo vyombo vya ulinzi na Usalama vinapenda sana kuwatisha Wanasiasa,hata kama sehemu kuna amani tele wao watajifanya kuna hatari eti wamepata taarifa za kiintelejensia,na hapo Mwana Siasa lazima aongeze fungu la ulinzi wa ziada! Bila kuwatisha na Hali ya Usalama, Wanasiasa ni wagumu sana kutoa pesa!!
 
Watu wanapeana kazi, wata justify vipi hayo matumizi ya bajeti za usalama sijui utumishi sijui madudu gani!

Kazi za kupeana na kulindana.

Everyday is Saturday................................😎
 
Hao wakina Biden na Eliza wanalindwa na zaidi ya hao watu wanaowalinda viongozi wa Africa.

Nadhani tunakurupuka sana, anapokuwepo raisi wa US au malkia, mzingo mkubwa unakuwa kwenye rada ya kiulinzi, thermal image inafanya kazi muda wote, snipers, SS, CIA, MI6, FBI, NSA, na technology za hali ya juu kulikagua eneo lote.

Hatuna hiyo teknology, hatuna huo uwezo, angalau basi apate ulinzi wa bodyshield.
 
Back
Top Bottom