Tanzania tuna ombwe la chama cha kisiasa kinachoendana na matakwa ya Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania tuna ombwe la chama cha kisiasa kinachoendana na matakwa ya Watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kimboka one, Jan 20, 2012.

 1. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Ndugu zangu wanajamvi,niwape pole sana kwa misiba yote miwili ya viongozi wetu iliyotukumba hivi karibuni.

  Nametakafakari sana mwenendo na mwelekeo wa siasa za Tanzania kwa kupitia katiba na ilani ya vyama vyote hususani vile vilivyoweka wagombea uchaguzi uliopita,pamoja na kuangalia mwelekeo ya vyama hivyo.

  kadhalika nimetazama mtazamo wa jamii na mahitaji ya watanzania wasasa,nasisitiza watanzania wasasa. watanzania wameamka sana na kuashiria kutengana na mawazo ya kikoloni tulioishi nayo kwa muda mrefu,watanzania wanataka sasa wapate chama kinacholingana na watanzania wa leo,kwani vyama vilivyopo vinamtazamo ile ile wa kikoloni ya kunyunya na kunufaisha wachache na mbaya zaidi ni vikundi vya watu wanaosaka utajiri na umaarufu kwa udi na uvumba.

  lengo langu kuja na hoja hii ni kutaka kukumbusha wadau hili tufikiri namna ya kupata chama kipya hasa baada ya katiba mpya.
  chama ambacho kitaweka wazi namna ambavyo chama kitaepusha serikali yake na mafisadi na watu wavivu kwa mkakati sahihi na wakudumu.

  aidha kupitia katiba ya chama hicho kibainishe sifa za viongozi watakao ongoza serikali yake na hapa turejee kwenye azimio la arusha na kuchukua zile sifa kama zilivyo,ni imani yangu watanzania wenye uwezo na sifa hizo wapo,mfano kiongozi wa chama asiwe mfanyabihashara,asiwe na mali nyingi na hili linapimika tu,kama azimio la arusha lilitaja nyumba leo tutaje sifa hizo kama vile asiwe na nyuma zaidi ya moja,asiwe na magari zaidi ya mawili na hapa watoto,mke au wake na ndugu wa karibu wanausika katika kuhakiki mali za viongozi,kwa uchache ndiyo njia ya kuziba ombwa hili.wewe unawazaje?
   
 2. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Ondoa upupu wako hapa, Azimio la Arusha liliasisiwa na chama gani? na hicho chama chako kipya kitapata wapi 'mandate' ya kutumia Azimio la Arusha ambalo sio lake?
   
 3. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Sera za JWTZ ndo zinafaa kwa mijitu kama ya Tanzania!
   
 4. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,367
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  Huo ndio mwisho wake wa kufikiri, kaka usimchukie, chukia kupotoka kwake.

  Kwa mtoa maada, katiba mpya Tanzania ni wimbo wenye lugha isiyoeleweka. Kwanza mamlaka ya rais katika mchakato mzima wa kukusanya maoni, ufinyu wa elimu ya uraia ma uelewa wa katiba iliyopo ni vitu ambavyo kwa hakika vinakwaza zoezi zima. Ni nani anayeweza kuelezea radha ya mauti ikiwa yungali hai? Ama ni nani awezae kuiona kesho. Napenda tu kukupa busara kwamba safari moja huanzisha nyingine na kaa ukijua usilolijua litakusumbua. Basi kamz uwezo wa mpumbavu ni kutoelewa mambo, mjinga kamwe hawezi kuwa rafiki wa mshenzi. Kama kipofu anamuongoza kipofu mwenzie nadhani unajua mwisho wake kaka, hatuwezi kukushika mkono kwa kuwa wewe una upofu wa kujitakia basi ni heri kwako kukata pua uunge wajihi.

  Tanzania ya leo inaamka kutoka katika usingizi mzito wa ujinga na ule wa kuona kila siku ni kama jana. Huwezi kuwa kipofu usione juhudi zinazofanywa na wazalendo katika kulikomboa taifa lao leo na useme unamsubiri masihi 'katiba mpya' ndio uchague bega. Hapo kaka hutimizi wajibu wako na naanza kupata wasiwasi wewe sio Mtanzania halisi. Labda nikuulize, mwanao akikukosa leo utamrudi amz utamwambia amsubiri babu yake, yaani baba yako wewe, aje mwakani amuonye mwanao kwa kuwa tu baba yako ni babu yake mwanao na ana busarz kuliko wewe!? Utakuwa ni mpuuzi na kila mtu atakushangaa.

  Wananchi wanataabika na maisha wakitafuta kila namna kuiondoa serikali ya hovyo madarakani kwa kuvijenga vyama makini ili kuuimbia 2015 kwa kishindo halafu na wewe unamsubiri masihi tu? Kweli ndugu yangu wewe hufai kabiaa hata kuwa na familia.

  Sio leo tu, hata kesho nitakuelimisha kwamba mkombozi wa nchi hii ni mimi na wewe na maamuzi yetu, kama hali yenyewe ndio hivyo kama wewe nadhani tunahitaji kurudi nyuma ili kujiandaa kwa silaha nzito.

  Ni mimi,
  Pangu Pakavu,
  Nakusalimia.
   
 5. T

  TUMY JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Azimio la Arusha si mali ya chama chochote cha siasa hapa Tanzania hilo kaa ukilifahamu, yeyote anaweza kuingia madarakani na kama anaona yaliyosemwa katika azimio la arusha yanatekelezeka anayatekeleza hakuna mwenye Interlectual Property Right hapo.
  Kuhusu muamko wa watanzania ni kweli ila binafsi nafikiri muamko wa watanzania katika masuala ya siasa uko zaidi mjini na si vijijini we still have a long way to go.
   
 6. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Kimbokaone, unalosema linaweza kuwa na chembe za ukweli, lakini kiuhalisia haiwezekani kupata chama cha siasa kitakachogusa na kuridhisha Watanzania wote, Watanzania tuna imani, makabila na matabaka tofauti na kila tabaka lina mahitaji tofauti tofauti ambapo imani na matabaka mengine yanakinzana na ya wengine.
  Hivyo maono yako, kiuhalisia hayawezekani.
   
 7. b

  bensonlifua92 Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kimboka one

  Ngoja nikuwekee maneno yako ".......kadhalika nimetazama mtazamo wa jamii na mahitaji ya watanzania wasasa,nasisitiza watanzania wasasa. watanzania wameamka sana na kuashiria kutengana na mawazo ya kikoloni tulioishi nayo kwa muda mrefu,watanzania wanataka sasa wapate chama kinacholingana na watanzania wa leo,kwani vyama vilivyopo vinamtazamo ile ile wa kikoloni ya kunyunya na kunufaisha wachache na mbaya zaidi ni vikundi vya watu wanaosaka utajiri na umaarufu kwa udi na uvumba....."

  Kwanza nakuunga mkono kuwa watanzania wa sasa wameamka sana.... Ila tutofautiane kuwa hawa watanzania hawakujiamsha tu wenyewe...kuna waliojitolea kuwafanya wenzao hawa waamke ambao wewe umeshindwa kuwatambua au kwa makusudi umekataa kuwatambua....na chama cha nmna hiyo tayari kipo.... any way kwa mawazo yangu ambayo si lazima yawe sawa na yako

  Ndugu yangu unachotakiwa ni kuunga mkono juhudi zilizokwisha fanyika hadi kufikia hapo ambapo hata wewe umeona tumepiga hatua, na kisha uje na michango yako wewe... nini zaidi kifanyike ili tusonge mbele zaidi au tuamke zaidi...

  AU...Kama unaona hakuna chama kabisa chenye hali ambayo wewe unataka iwe nacho, badala ya kusema tu maneno... ya kinatakiwa chama kingine bila ya kusema nani akianzishe ushauri wako unakosa maana na ni maneno matupu (empty words...) yasiyo na tija yoyote

  Ushauri wangu kwako: Anzisha CHAMA, weka sera zako sawa na kama kweli sera zako zinamaana basi utapata wafuasi wa kutoshea kufika kule ambako wewe unadhani tunahitaji wafike. Halafu acha vyama vingine viwepo ili vikipe ushindani hicho chama chako kipimwe kama kweli sera zake zina mashiko au ni kelele tu....


  Asante kwa uhuru wa mawazo....
   
 8. knownless

  knownless Senior Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 116
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kama unaona vilivyopo vimeshindwa kulingana na mawazo yako huna budi kuanzisha chama chako ambacho kitafanya kazi kulingana zako. Ukishindwa ungana na HR kwani yupo mbioni kuanzisha chama kipya
   
 9. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Asante, tunashukuru.
  Hapana, chombo pekee kinachoweza kuendana na matakwa ya Watanzania kwa ujumla wao ni katiba na kama katiba iliyopo haikidhi matarajio yao, jibu sahihi ni katiba mpya.
   
Loading...