Lwiva
JF-Expert Member
- Apr 17, 2015
- 12,499
- 17,572
Tatizo ni pesa za mikopo zote hizo alizo ongezaAkiba ya Fedha zetu za kigeni Rais Samia ameiongeza kwa TZS 2.3T sasa imefikia $5.8b toka $4.8b mwezi March 2021 | Pesa hii inaweza kulisha Watanzania wote kwa miezi mitatu mfululizo yaani Wale walale tu hakika Tanzania tuko vizuri Sana kwa sasa.
"Hakuna kama Samia "
Namba hazijawahi kudanganya na hazitadanganya tunaposema Rais Samia Suluhu Hassan rekodi zake hazikamatiki na mwendo wake unatoa matumaini mapya kila uchapo lazima kama taifa tukubaliane hivyo, Akiba hii ya fedha za kigeni ni muhimu sana kwa nchi hasa wakati wa majanga mbalimbali ambapo in EAC kiwango cha chini kwa nchi ni uwezo wa kuagiza bidhaa na huduma nje kwa miezi 4.5 mfukulizo.
Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na kuendekeza ujenzi wa SGR kwa zaidi ya Tshs 10trl, Kujenga JNHPP kwa zaidi ya Tshs 6.55trl, kugharamia elimu bila malipo kwa watoto wetu, kupandisha madaraja|mishahara wafanyakazi wa serikali,kutoa mikopo HESLB ya zaidi ya Tshs 500b, kujenga vituo vya afya 220, kujenga madarasa 18,000, kujenga mabarabara na madaraja kila kona ya nchi na mengine mengi bado amefanikiwa kuongeza akiba yetu ya fedha za kigeni (Gross official foreign reserves) kwa zaidi ya $1BL sawa na Tshs 2.3trl na kufikia jumla ya $5.8BL karibu Tshs 13.34trl kutoka $4.8BL aliyoikuta,Hakika Rais Samia anamwendo mzuri sana,
Fedha hizi zinaweza kuagiza bidhaa na huduma nje kwa zaidi ya miezi 6 mfululizo rekodi ambayo sina hakika kama kuna Rais yeyote tangu tupate Uhuru aliwahi Kuifiki na kwakuwa GDP per Capita yetu ni Tshs 2,653.8 au $1,156.8 basi pesa hii inaweza kumlipa kila Mtanzania kwa kila siku Tshs 2,700 kwa miezi mitatu mfululizo asifanye kazi yeyote ale na alale tu,Hakika Rais Samia ni tumaini jipya linalohitaji kuungwa mkono na kila awaye,
Baadhi ya faida za Gross official foreign reserves kwa nchi ni hizi,
Kwanza,kuiwezesha Serikali kutimiza mahitaji yake ya fedha za kigeni na mahitaji ya kuagiza bidhaa kutoka nje,
Pili,Kutoa imani kwamba Serikali inaweza ikatimiza majukumu yake ya muda mfupi kulipa madeni ya nje,
Tatu, Kusaidia utekelezaji wa sera za fedha na kubadilisha fedha za kigeni pamoja na uwezo wa kuingilia kuhakikisha fedha ya taifa ni imara,
Nne, Kuchangia katika mapato ya Benki Kuu kwa kuhakikisha kuna kiwango cha kutosha cha mapato kulingana na jinsi Benki inavyoweza kuhimili majanga/vihatarishi
VIVA SAMIA VIVA || VIVA TANZANIA VIVA