Tanzania tumewahi kutuhumiwa tunaficha data za Ebola

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Hili liko wazi jamii za kimataifa zimewahi kuituhumu serikali ya Tanzania kuwa wanaficha data za ugonjwa wa Ebola kitu ambacho kilipingwa na serikali ya Rais Magufuli

Serikali ya Magufuli ilisema ni wivu tu unawasumbua kuhusu hatua tunazopiga kuhusu maendeleo ya wananchi kwa kuibua miradi mikubwa

Baadae hali ilitulia na maisha yakaendelea na punde limeibuka gonjwa la Covid 19 ambalo awali serikali ilikuwa wazi kwa wananchi na jamii za kimataifa

Lakini sasa data za Corona zimeanza kusua sua hasa baada ya hotuba ya mheshimiwa pale Chato hasa kwa upande wa Tanzania bara ambapo ana mamlaka ya moja kwa moja

Je jamii ya kimataifa inaanzaje kuitazama Tanzania kuhusu Covid 19 na Ebola hasa suala la data na transparency?

Hatuoni kwamba jumuiya za kimataifa zitaanza kuamini kuwa Tanzania tumewahi kukumbwa na Ebola na kuficha data?

Ni maswali magumu sana kujibiwa kipindi hiki na tunajenga mazingira magumu ya kuaminika kwenye jamii na jumuiaya za Kimataifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dada na jamaa wa JF, kuna muda sio kila ukweli lazima usemwe.
Mwisho kujua vitu vingi sana inaweza isiwe vizuri sana kwako.

Uwe na wakati mwema.
 
Mkuu umesahau walianzia kwenye ZIKA, wakamtumia dada ake LEMUTUZ akishiwa kuliwa kichwa wakamwajiri wao.
Wakaja kwenye EBOLA wakagonga mwamba.

Wakaja kwenye kuchapisha nyaraka za kuaminisha kwamba Tzie itashambuliwa na Vikundi vya Kigaidi watalii wajiadhari.
Kimbembe sasa ni COVID 19 hapo hatuchomoki.
 
Sijui kwanini viongozi wa Tanzania waliopewa dhamana ya kuongoza wananchi wanaficha habari mbalimbali zinazohusu wananchi na nchi yao. Mficha uchi hazai.
 
Mkuu umesahau walianzia kwenye ZIKA, wakamtumia dada ake LEMUTUZ akishiwa kuliwa kichwa wakamwajiri wao.
Wakaja kwenye EBOLA wakagonga mwamba.
Wakaja kwenye kuchapisha nyaraka za kuaminisha kwamba Tzie itashambuliwa na Vikundi vya Kigaidi watalii wajiadhari.
Kimbembe sasa ni COVID 19 hapo hatuchomoki.
Mbona tayari tumechomoka! Marekeniv ndiyo hawachomoki wanalia na kusaga meno.
 
Mkuu umesahau walianzia kwenye ZIKA, wakamtumia dada ake LEMUTUZ akishiwa kuliwa kichwa wakamwajiri wao.
Wakaja kwenye EBOLA wakagonga mwamba.
Wakaja kwenye kuchapisha nyaraka za kuaminisha kwamba Tzie itashambuliwa na Vikundi vya Kigaidi watalii wajiadhari.
Kimbembe sasa ni COVID 19 hapo hatuchomoki.
Kweli mkuu,nimekumbuka Zika ilimtumbua yule mama ambaye sasa yupo UN

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom