Tanzania tumemkabidhi mbu kazi ya kutibu Malaria?

Kiby

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
6,899
4,623
Wakuu nilikuwa nafuatilia kipindi cha kipima joto ndani ya ITV leo, ambapo swali lililokuwa likijadiliwa ni 'kukithiri kwa ujambazi wa kutumia silaha nchini' Studioni alikuwepo mwenyekiti wa serikali za mitaa kimara B, mhadhiri wa chuo kikuu UDSM na mkurugenzi upelelezi makosa ya jinai Robert Manumba.

Kilichonisukuma kuandika hii thread ni wasiwasi wangu juu ya uwezo wa uelewa wa mambo wa DPP wetu, kweli kwa yeyote aliyemsikiliza anaweza kugundua kasoro nyingi sana kwake na kutilia shaka uwezo wa kielimu wa huyu mtu aliyeshikilia ofisi muhimu nchini.

Pamoja na mambo mengi aliyoshindwa kutolea ufafanuzi mojawapo ni police wachache tulio nao ni mkakati wa serikali wa kuwa na jeshi dogo ama ni serikali kutokuwa na uwezo wa kuajiri police wanaowiana na idadi ya raia. Muda wote aliopewa kuongea alikuwa akizungumza kama mkuu wa kitengo cha propaganda wa chama fulani cha siasa.

Wakuu naomba msaada tusaidiane, je elimu ya mtu huyu ni ya kiwango gani?

Ni vigezo gani vinavyohitajika kwa mtu kuajiriwa katika hii ofisi?

Tatu ofisi hii ipo katika mhimili gani wa dola?

Mwisho ningefurahi kama tungejulishwa ikiwa ofisi hii ni ya kisiasa au kiutendaji na inawajibika kwa nani.
 
Jeshi la POLISI Tanzania mmh!

.
Jibu la kiini cha kesi kubwa hasa zile za kutumia kalamu(computer) kutokuwa na nguvu linaweza kuwa uwezo mdogo wa kuichambua kuiainisha jinai wa mkurugenzi? Na kama ni hivyo, watu walioshikilia ofisi kubwa huku uwezo wa uelewa wao ni mdogo linawezakuwa tatizo la kiufundi kwa yule anaewateua?
 
Back
Top Bottom