Tanzania tulivyotekeleza Azimio la Beijing la 1995

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Miaka 25 ya Ulingo wa Beijing

MIAKA 25 nyuma, wajumbe 17,000 kutoka mataifa yote ulimwenguni, na wanaharakati 30,000 kutoka mataifa yote ulimwenguni, walikutana Beijing, Uchina, kwenye Mkutano Mkuu wa Wanawake, ulimwenguni.

Mkutano huo, ambao Katibu Mkuu alikuwa Mtanzania, Mama Gertrude Mongella, ulitoa Azimio la Beijing ambalo limejikita kwenye masuala muhimu yafuatayo:

■ Usawa wa Jinsia
■ Afya ya uzazi
■ Kutokomeza mila potofu kama ukeketaji
■ Usalama wa wanawake na watoto
■ Fursa za kuinua hali ya kiuchumi kwa wanawake
■ Kuwa na Sera Shirikishi zitakazowaingiza wanawake wote, hata waliopo pembezoni, kwenye wigo wa-
Nafasi za maamuzi na uongozi
Fursa za mikopo yenye riba nafuu
Uwakilishi Bungeni na kwenye Udiwani, hadi kupelekea Viti Maalum Bungeni/Affirmative Action
Fursa za Masoko
Fursa za kuwa na maamuzi juu ya maisha
■ Afya kwa wote
■ Elimu kwa watoto wa kike
■ Ajira kwa wanawake wenye stadi stahiki
■ Kutokomeza ukatili wa kijinsia
■ Ulinzi wa wanawake na watoto dhidi ya ukatili
■ Utetezi wa wanawake wanaponyanyaswa kijinsia
■ kuvunja mfumo dume unaokandamiza maendeleo ya wanawake na watoto wa kike
NK

Tanzania ilipeleka wajumbe wapatao 1,200 kwenye Mkutano wa Wanawake Beijing mwaka 1995, wakiwemo wanaharakati.
Tanzania ilikuwa miongoni mwa mataifa ya kwanza kusaini Makubaliano ya Beijing na kama Taifa, haya yametimizwa:

■ Kupitisha Sheria ya Makosa ya Kujamiiana SOSPA 1998, kama njia ya ulinzi wa wanawake na watoto, dhidi ya ukatili wa kijinsia.

● Kuptisha Sheria 2 muhimu:
Sheria ya Ardhi 1999
Sheria ya Ardhi ya Vijijini 1999
Hizi Sheria 2 zimeainisha haki ya mwanamke ya kumiliki-
︎ Ardhi
︎ Jengo/majengo
Na, haki ya mwanamke kumiliki shamba, ambayo kimila kwenye baadhi ya makabila, wanawake hawakuruhusiwa kumiliki ardhi, wala jengo, wala mifugo.
Kwa sasa, baada ya Serikali kusaini Azimio la Beijing la 1995, wanawake wamepata haki hizo.

● Sera ya Jinsia 2000- Hii imeainisha ni maeneo yepi yapewe kipaumbele kwenye mustakabala wa haki jinsia, na imeweka bayana mbinu za kufikia malengo hayo.

● Sera ya Taifa ya VVU/UKIMWI 2001.
Sera hii imeweka bayana uwepo wa unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya WAVIU, wanaoishi na VVU/UKIMWI, na imeweka misingi na mbinu ya kutokomeza unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya WAVIU.

● Sheria ya kutokomeza uuzaji wa Binadamu/Anti Persons Trafficking Act 2008.
Sheria hii inapinga-
Uuzaji wa wanawake na watoto kwenye biashara haramu ya ngono
Ajira ya watoto kwenye migodi; mashamba makubwa; na kwingineko
Kufanyisha kazi za nyumbani watu bila ya kuwalipa ujira
Kusafirisha binadamu kwenda mataifa mengine ambapo wanakuwa watumwa mamboleo

● Sheria ya UKIMWI 2008.
Hii imeweka bayana haki kwa WAVIU ya-
• Kuwa na ajira
• Kutobaguliwa
• Kupata bima ya afya, ambayo kabla yake wakinyimwa
• Kuoa au kuolewa
• Kuzaa, hii hasa baada ya tiba ya MCTP, Mother to Child Prevention, ambayo mwanamke mwenye VVU akiwa mjamzito hupewa tiba hii ili kuzuia maambukizi kwa kiumbe aliye tumboni
• Kuambukiza VVU kwa makusudi
• Waajiri wanaoachisha waajiriwa kazi wanapogundulika wanaishi na VVU, kuchukuliwa hatua za kisheria

● Kuanzishwa elimu jamii juu ya haki jinsia.
Hii inafanywa na serikali, na AZAKI kupitia mikutano elekezi; vyombo vya habari; viongozi.

● Kuongezwa wanawake kwenye Uwakilishi Bungeni, Serikalini, kwenye AZAKI, na kwenye sekta binafsi.

● Dawati la Jinsia kwenye vituo vya polisi kusaidia wanawake

● Matusi ya nguoni na lugha za kashfa wanawake wanapopita barabarani kwa kweli, yamepungua mno.
Kabla yake, wanawake wakiitwa Wo Wo Wo au Nungayembe
Tukawaambia Shikeni adabu zenu. Na mukome

Yanayotakiwa kutekelezwa ili kufikia Lengo la Tamko la Beijing


¤ Tunahitaji Sera ya Afya ya Uzazi SRH Policy.
Hadi sasa, Wizara ya Afya inatumia Muongozo.
Tunataka Muongozo uwekewe wigo mpana, na kupitishwa kuwa Sera.


¤ Tunataka Dawati la Jinsia liwepo sehemu zote za ajira, hata kwenye magulio, ili wanawake wanaopata unyanyasaji wa kijinsia, wawe na sehemu ya kupeleka kilio chao.
Dawati hili liwepo hadi ngazi ya jamii.

¤ Tunataka elimu jamii juu ya madhara ya ndoa za utotoni zifike sehemu zote za Taifa, hadi ngazi ya jamii.

¤ Tunataka wabunge wanaoteula kwenye Viti Maalum watambue kuwa sisi, wanawake wa Tanzania, ndiyo Jimbo lao, siyo vyama vya siasa ambamo wamepitia.
Huwa wanajusahau.

¤ Tunataka tunapoongelea amani, ianze ngazi ya familia.
Tutokomeze ukatili wa ndani ya familia.

¤ Tunataka usafiri utengwe kwa ajili ya wanawake pekee kwenye mabasi, ili pawe sehemu salama, hususan usiku wanapotoka kazini, kama manesi; Mama Lishe; nk.
Mataifa ulimwenguni yametenga usafiri wa abiria kwa ajili ya wanawake pekee.

¤ Tunataka Wazee walindwe dhidi ya ukatili wa ndani ya familia.
Viongozi wa dini badala ya kufunda manyago, watoe mafunzo juu ya umuhimu wa kutunza wazee kwenye familia.
Tumeshuhudia wanaopiga Mama au Baba zao.

¤ Tunataka mabinti wanaopata ujauzito wakiwa shule wapewe-
° Fursa kusoma kwenye shule/vyuo maalum ambapo wataweza kwenda na watoto vichanga vyao
° Wapatiwe ushauri nasaha, kuwa wanaweza kujiendeleza
° Wasibaguliwe kwenye jamii

Haya yote yanawezekana iwapo sote kwa pamoja, tunashiriki kuleta matokeo chanya.

Happy 25 Years of Beijing Declaration,
IMG-20201220-WA0027.jpg

Leila Sheikh
Mwanahabari mwandamizi,
Mtetezi wa Haki Jamii
 
Leila Sheikh,

Ana content nyingi sana ya kihistoria; nyingine ambazo hazina rekodi hata kidogo, ama kama zipo ni zimefichwa katika makavazi. Napenda maandiko/ mawazo yake (yale ambayo ni public na yasiyo public) maana huwa najifunza mengi sana.

Leila mimi kama mdau ambaye huwa nafurahishwa na maudhui, nitafurahi ujisajili JamiiForums na pale upatapo nafasi uka share mawazo/ hoja/ historia ambazo zina umuhimu wa kuwa katika rekodi kwa mustakabali wa the next generation. Ninajitolea kuwa bega kwa bega namna bora ya kufikisha ujumbe kupitia Jukwaa hili na urahisi wa kutumia.

Thank you for this post. It is very useful.
 
Ahsante kwa elimu, ndogo uliyotupa kwenye mandiko lako na Kuhakikisha wanawake wanapata Haki zao stahiki.

Ila kuna Baadhi ya vipengele vinahitaji mabadiliko Kuanzia kwenu nyie.

Wanawake,watoto wa kike/mama zetu wa leo, walio wengi wamekengeuka wanapelekeshwa na utandawazi..Sehemu za Siri zimegeuka kuwa public ( Mavazi) hivyo heshima mnayoitaka hamuwezi ipata msipo jirekebisha nyie wenyewe Kwanza.

Pili, swala la kutengewa Usafiri wenu...hilo hakiwezekani nasisitiza tena haliwezekani, Kwanza ni ubaguzi kibinaadamu, pili Sijaona Shida Katika hilo.

Tatu na mwisho swala la kuruhusu watoto wakike kuendelea na masomo wanapopata ujauzito mashuleni, hamuoni ni kuongeza hamasa kwa watoto hao kuona hakuna madhara makubwa katika kosa hilo hivyo kuendelea Kuharibu jamii katika jambo baya la kukemewa vikali dhidi ya wale watakao shindwa kufuata Sherie Ikiwa ni pamoja na adhabu Kali ili iwe funzo kwa wengine.

Anyways hongera kwa elimu nzuri ya ukombozi kwa wanawaKe.
 
Ahsante kwa elimu, ndogo uliyotupa kwenye mandiko lako...na Kuhakikisha wanawake wanapata Haki zao stahiki.

Ila kuna Baadhi ya vipengele vinahitaji mabadiliko Kuanzia kwenu nyie...
Leila amesema mabinti wanaopata ujauzito wakiwa shule wapewe fursa kusoma kwenye vituo maalum.
Hii itawasaidia wasiwe tegemezi.

Mtoto akikosea anasahihishwa.

Tukiwaacha tu, wataharibikiwa.

Wanaweza kujiingiza kwenye biashara haramu ya uchangu doa.

Hivyo, wasaidiwe tusiwapoteze kabisa.
 
Hata siku moja mwanamke hawezi kuwa sawa na mwanaume!
Hapa tu wanawake ni jeuri je wakiupata usawa huo si itakuwa balaa

Ova
 
Back
Top Bottom