Tanzania tulifanya mzaha kwenye sekta ya ubinafsishaji...!

Tanzaniaist

Senior Member
Nov 29, 2011
161
156
Habari wana JF..,ni muda mrefu nilipotea nilikuwa kifungoni..,lakini nimerudi tena!

Leo napenda kuiongelea nchi yangu Tanzania, Ambayo imejaaliwa kuwa na rasilimali za kutosha kuweza kuijenga nchi na kuinua maisha ya kila siku ya Mtanzania...! Namwonea Huruma sana JK raisi wetu mpendwa na ninahisi saa nyingine anajilaumu kwanini anabeba mzigo ambao ulisababishwa na aliyemtangulia Ben Mkapa!

Kwenye mada hii sina nia mbaya ya kumsema Ben Mkapa rais wa awamu ya tatu.,ila madudu yaliyofanywa katika serikali yake hasa kwenye sekta ya ubinafsishaji ndio inaligharimu taifa sasa hivi..,kwaaanzia kuongezeka gharama za serikali,ajira,kufa kwa viwanda na mashirikia ya umma,umeme,mikataba mibovu ya madini ambayo hainufaishi taifa..!
Haya ndio matunda ya awamu ya tatu..!

Hebu tucheki Air Tanzania, shirika la ndege la Taifa..,ambalo liliuzwa kwa South african airways kipindi cha Mkapa sasa hivi ni kama limekufa huku kukiwa na utata ambao haueleweki..,KENYA AIRWAYS tulikuwa nao sawa baada ya east airways kufa.,lakini hii leo KENYA AIRWAYS WANA NDEGE KARIBIA 34, wakati AIR TANZANIA wana NDEGE MOJA TU, ambako moja ilianguka juzi.., wenzetu wakenya kwenye suala la ubinafsishaji au kwenye masuala la kitaifa hawana mzaha..!

Tuje TTCL, mbona hakuna kinachoeleweka, leo hii kampuni ya simu ya kenya SAFARICOM ndio kampuni kubwa ya simu Nchini kenya, tuje RELI ina maana tulishindwa kupata mwekezaji wa maana kwenye hii sekta paka tukumbatie wahindi ambao hawana hata uwezo wa kununua mabehewa na kuleta mabehewa feki, Tuje TANESCO mm nadhani kama BEN MKAPA angekuwa SERIOUS angewezesha uwekezaji kwenye kituo cha umeme wa makaa ya mawe pale KIWIRA nadhani leo hii kusingekuwa na matatizo ya umeme na hata kumpungizi mzigo JK, Lakini tukasikia alijimilikisha kwa bei chee..,na leo hii Taifa linazizima kwa matatizo ya umeme

Tuje kwenye sekta ya Viwanda, kipindi cha BEN MKAPA tulishuhudia utitiri wa Viwanda vikifa..,VIWANDA ambavyo vilijengwa na MWALIMU JK NYERERE..,sio kwamba vilifilisika ni kwamba serikali ilishindwa kutafuta wawekezaji potential..,mfano.Moroshoe ambako kiliuzwa na kisha baadae kuchomwa moto, moro leatherbags,urafiki,kili tex,machame machine tools na viwanda mbali mbali ambavyo baadhi viliuzwa na leo hii yamebakia Magodown na wamiliki kuuza mashine Au mengine kugeuzwa zizi la mifugo mfano.Canvas Morogoro..,leo hii Taifa hakina kitu cha kujivunia kwenye suala la Uzalishaji kila kitu tunaingiza toka nnje..,tumshukuru BAKHRESSA kwa kutufutia aibu kwa bidhaa zake za AZAM zinazotangaza tanzania..!

Tuje kwenye suala la Ardhi, MWALIMU JULIUS K.NYERERE alipokonya ardhi walowezi na kutaifisha mashamba baada ya ARUSHA DECLARATION 1977..,kama yale Mashamba ya NARFCO Babati,Katesh, na Arumeru..,lakini BEN MKAPA Akayarudisha tena hayo mashamba kwa wageni badala ya kurudisha kwa wananchi..,mfano babati mashamba yaliyokuwa ya serikali yameeuzwa kwa Wahindi toka nnje, Arumeru na hata baadhi ya viongozi wa serikali kuhodhi Ardhi kubwa maeneo ya Mvomero hadi vijiji kuamishwa..!

Tuje kwenye kuongezeka Gharama za Serikali, Leo hii serikali inalia watumishi wake kukosa nyumba kwenye sehemu ambako wanapopangiwa vituo vya kazi..,hii ni baada nyumba za serikali kuuzwa na kukosa mipango ya kujenga nyumba nyingine za kuishi..,na kuipa serikali mzigo mkubwa..!

Jamani wana JF ni mengi sana ambayo nashindwa kuendelea kutokana na Uchungu, ninachoweza kusema Poleni Watanzania, Pole Rais Kikwete
 
Tanzania bado hatujapata viongozi,mm nazan katiba mpya iweke kipengele cha kuwachukulia hatua kama china
 
Back
Top Bottom