Tanzania: Tukitaka maendeleo ni lazima tufanye maamuzi haya mepesi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania: Tukitaka maendeleo ni lazima tufanye maamuzi haya mepesi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bundewe, Jul 21, 2011.

 1. Bundewe

  Bundewe JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Watanzania kama tunataka maendeleo ni lazima tuwe na utamaduni wa kufanya maamuzi bila woga. Maamuzi muhimu sana kuyafanya ni kuondoa serikali iliyopo madarakani endapo tunaona haina tija kwetu. Kwa sasa hali ilivyo katika nchi yetu ni wazi kwamba viongozi waliopo madarakani wamebweteka kiasi kwamba wanajua hata wakiboronga kiasi gani, watashinda uchaguzi unaofuata, hivyo hawaoni umuhimu wa kuwajibika kwa wananchi. Na wale wanaowania nafasi hujipendekeza kwa viongozi wao wa chama ili wapitishwe kugombea nafasi za uongozi hasa urais ambao wanaona wakishapitishwa na chama tu tayari wameingia ikulu, wananchi hatuna sauti.

  Nchi nyingi zilizopiga hatua hazina msalie mtume!! ukiboronga unang'olewa kwenye uchaguzi unaofuata. Angalia Marekani, Ghana, nk. Njia muhimu na pengine ya pekee kufikia maendeleo tunayoyataka ni kukiondoa chama kilichopo madarakani na kuweka kingine, nacho kikiboronga tunakiadhibu vile vile kwa kukiondoa. Baada ya miaka 10 tu ya kufanya hivyo atakayeingia madarakani ataelewa umuhimu wa falsafa ya Nguvu ya Umma. Haiwezekani mtu anaingia madarakani ujambazi unaongezeka, shilingi inashuka thamani, umeme unapanda bei/mgao, gesi inapanda bei, mafuta bei juu, elimu inashuka, analeta ambulance za bajaj, anaingia mikataba ya kifisadi, anateua maswahiba zake, serikali yake inagawanyika, nk. halafu wananchi tusichukue hatua. Ni lazima atatudharau. Umma hauna nguvu.

  Nashauri kwa sasa tuache ushabiki wa vyama ila tujiulize serikali iliyopo madarakani imeweza kwa kiasi gani kutatua kero za wananchi? Imetimiza ahadi ya "maisha bora kwa kila mtanzania?' Tusiingie kwenye mtego wa kutetea kila kinachofanywa na serikali eti kwa sababu chama chetu ndo kilichopo madarakani. Kaa pembeni ya chama kwa muda na uone je, tangu serikali hii ya awamu ya nne imeingia madarakani imeweza kujibu kero za wananchi? Tusirejee kwenye falsafa ya 'zidumu fikra za mwenyekiti'. Let us be critical for once.
   
Loading...