Tanzania tujitoe Commonwealth

Rubabi

Senior Member
Nov 30, 2006
170
11
Uingereza waafrika kwa visa.Pesa zinatotumika katika huu mkutano zinaweza kujenga hospitali ngapi?Jee commonwealth inamsaidiaje raia wa kawaida Tanzania?

Mini naona commonwealth ni opportunity ya viongozi wetu hawa kutalii bure.It is a talking shop! A big joke! A patronising institution, yaani tunasherekea kutawaliwa?

Tanzania tujitoe, tuimarishe AU na East African community
 
Labda ujiulize kwanza tunapoteza nini kwa kuwa member wa Commonwealth? Mambo mengine huwezi kuona faida mpaka umehusika.

Kuna watu wengi tu ambao wamefaidika na TZ kuwa commonwealth hasa kwenye nyanja ya elimu, sasa kama cost ya hizo faida hakuna, sioni sababu kwanini tujitoe.

Hivi nani aliyekuambia commonwealth inasherehekea kutawaliwa?

Mtu unajitoa kwenye jumuia fulani kama cost ya kuwa IN ni kubwa sana kulinganisha na faida unayopata. Unless kama mwenzetu una data kuonyesha hasara ni kubwa kuliko faida basi lete hapa tujadili.
 
Inabidi kwanza uchukue muda ujielimisha kidogo kuhusu hii commonwealth kabla ya kutoa ushauri kama. Ukijielimisha vizuri nina uhakika utawaomba moderators waitoe hii mada yako haraka sana. Kwa hakiki commonwealth ni zaidi hako kamkutano unachokaongelea. Pole sana!
 
^Burden of proof iko kwako, nitajie faida ya commonwealth.

Hizo sponsorship mwishoni zinasaidia waingereza zaidi ya watanzania, niambie ni wangapi wamerudi baada ya kusomeshwa?

Ni wajibu wa serikari ya Tanzania kusomesha raia wake ,si wajibu wa uingereza kwa hiyo hizo sponsorship sio sababu ya kutetea commonwealth.

Commonwealth ni uendelezaji tu wa mawazo tegemezi ya viongozi wetu ambao mpaka joho la Bunge wanashoneshea Uingereza.

Tuimarishe kwanza local organisations kama AU na EAC, kwa kuwa hizi zitasaidia kumuinua mtu wa kawaida, kufanya biashara na majirani n.k.Kama commonwealth ina meno kweli mbona bado Uingereza haijaondoa subsidies kutoka kwa wakulima wao ili wakulima wetu waweze kuuza bidhaa zao huko ulaya waondokane na kutegemea misaada, wasomeshe watoto wao n.k?

Ndio maana ninasema wataongea maneno tu, labda watakaopata faida ni machangudoa tu wa kampala, na vipesa vya hapa na palemahotelini.Mkutano ukiisha,hali itabaki palepale.
 
Commonwealth ni uendelezaji tu wa mawazo tegemezi ya viongozi wetu ambao mpaka joho la Bunge wanashoneshea Uingereza.

Ndio maana ninasema wataongea maneno tu, labda watakaopata faida ni machangudoa tu wa kampala, na vipesa vya hapa na palemahotelini.Mkutano ukiisha,hali itabaki palepale.

Naona kidogo uko shalow jaribu kupekenyua kwenye tovuti yao ujue ni mambo gani wanayofanya. Ingekuwa vizuri kama ungejua tumefanya nini kutumia ipasavyo opportunities zinazotolewa na Commonwealth. Ukiangalia kwa undani ni sisi wenyewe tumefukza baadhi ya opportunities, sioni kama kuna haja ya kujitoa huko, labda tujiotoe AU, sio CW.
 
Msumbiji ndo tu wamejiunga- Rwanda ndo wanaomba uanachama- je Tz tujitoe? Kwa sababu zipi kubwa za kimsingi?
 
Hili kila mtu ana mtizamo wake, lakini binafsi sioni umuhimu wa hii CW! zaidi ya kuwa wote tulitawaliwa na mwingereza!
 
Hata siku moja mtu asitegemee jambo moja kuwa na faida kwa kila mtu. Tunapojadili faida ya kitu fulani ni muhimu kuangalia kama faida yake ni kubwa kuliko hasara tunayopata.

Tumeongelea masuala ya uraia wa nchi mbili, masuala ya TIC, masuala ya AU, masuala ya EAC nk.

Tatizo ninaliona hapa JF mara nyingi ni kwa mtu kudhani kwasababu yeye hafaidiki na jambo fulani basi halina maana bila kufanya uchunguzi wa kina kuangalia kama kuna faida au kuna hasara.

Inatosha kwenda website ya CommonWealth kujua faida zake nyingi. Lakini pia inabidi kujiuliza tunapata hasara gani kwa kuwa humo?

Mimi naamini kama jambo linasaidia hata mtu mmoja na halina madhara kwa wengine basi serikali ina wajibu wa kumsaidia huyu mtu mmoja aendelee kufaidika. Tukitegemea jambo lisaidie nchi nzima ndio tuone faida yake, tutasubiri mpaka mwisho wa dunia. Maendeleo ya nchi ni total sum ya vimaendeleo vya individuals.
 
Back
Top Bottom