Tanzania tujifunze kupitia ukuaji wa uchumi Ethiopia

DAD'S SON

JF-Expert Member
Nov 18, 2015
392
466
Kuna msemo unasema usimdharau mwenye njaa leo maana hata wewe kesho utalia njaa.

Miaka ya 2000 Ethiopia ndio ilikuwa nchi ya 3 kutoka mwisho katika zile nchi maskini duniani(was the third poorest county in the world).Pato la mtu kwa siku was almost $650.Zaidi ya 50% ya watu walikuwa wanaishi below the global poverty line,the highest poverty rate in the world.

What happened since is miraculous.
Kuanzaia mwaka 2000-2016 Ethiopia ikawa nchi ya tatu kwa ukuaji kiuchumi duniani ikuchuana na Myanmar ambayo ni ya pili bila kusahau China ambayo ni ya kwanza huku ikizibwaga Nchi kama India,Kazakhstan na Vietnam.According to IMF Ethiopia's economy has been growing rapidly since 2003.
Mwaka 2011 umaskini wa Ethiopia ulishuka kwa 31%(very interesting)
The outlook for the next 5 years is bright.

Ifike wakati viongozi wetu wajifunze kupitia the incredible economic rise of Ethiopia na sio bla bla za kwenye social media na Tv.
Ukisoma kiundani kuhusiana na historia ya Ethiopia utagu,ndua uchumi wa Ethiopia unategemea sekta kilimo na usafirishaji.Kwa Tanzania Mungu alitubalik kila kitu ikiwemo madini,vyanzo vya maji,misitu,ardhi yenye rutuba,nguvu kazi,gesi yaaani kiufupi Mungu alitupa kila kitu cha kutufanya tuwe one of the richest country in the world lakini leo hii Tanzania ni miongoni mwa nchi maskini duniani,raia wake bado wanaishi chini ya dola miaka na miaka(what a shame).

Kwa kuhitimisha viongozi tuliowapa dhima ya kutuongoza wajue uongozi ni kitu cha kupita na sio kitu cha milele,wasidhani wayafanyayo hatuyaoni japo wanadhani wanafanyia gizani,madaraka mliyonayo isiwe silaha ya kututishia kudai mlicho tupromise kwenye majukwaa,hali ya uchumi mtaani inatisha sana na ule msemo wenu wa kusema pesa mtaani haipo kwa sababu mmeziba machaka ya wapigaji dili ni uongo mkubwa sana kutokea duniani ni kauli ya watu walioshindwa kutimiza walicho ahidi.
 
una subiri nini kum tag jiwe "" aje kuusoma huu ujumbe wake ""..?
 
Serikali hii haitaki kuwekeza kwenye kilimo penye watu wengi na badala yake wameamua kununua ndege ambayo kiuhalisia sio kipa umbele.

Sector hiyo ya usafiri wa anga uwekezaji wake ni mkubwa mno na aghali zaidi kuliko kilimo na ina changamoto nyingi sana kiasi kwamba mashirika mengi ya ndege hata ktk mataifa tajiri hutegemea ruzuku toka serikalini ili zi-survive ushindani.

Hivyo sisi uchumi wetu kukua itakuwa ni ndoto kwa sababu ya "Misplaced Priorities".
 
Ethiopia wana shida kubwa sana kiuchumi na wengi wa viongozi wa afrika hawajui tafsiri ya kukua kiuchumi wanadhani kuwa na majengo marefu ya vioo mjini ndio kukua kwa uchumi bora. Hatimae watu wanaachwa kombo.

Ukiijua definition ya development hutapata shida kujua maendeleo halisi ni nini? Honestly nikusaidie tu development "refers to the improving the standard of living of people" Ethiopia hawana hii mitaa inang'aa ila watu wanavilio vya Hatari kila siku bora wafe kwenye maroli kuliko kuishi Ethiopia. Same applies kwa Rwanda tunaambiwa uchumi wao unakuwa but akilini kila mnyarwanda anatamani kuishi Tanzania.

Nchi za afrika zinapaswa kujifunza na kuwa kama zile za Nordic countries, Norway, Sweden, Denmark e.t.c ambazo zinaamini katika "welfare state" yaani watu wastawi kwanza then hayo ndio maendeleo yenyewe the rest will follow later. Hapa ndio maana hata wamarekani wanatamani kuishi Nordic countries.
 
Sio huko Ethiopia nimesoma juzi wanasema akiba ya fedha za kigeni inaporoka siku hadi siku imefika wakati kuna baadhi ya bidhaa marufuku kuagiza nje ili kulinda kiasi kilichopo.

Kwa maana hiyo biashara haziendi ajira zinakufa na maisha magumu.

Hawa waethiopia mamia kwa maelfu kila siku wanajilipua kwenda SA kutafuta maisha bora...

Tanzania tuwekeze kwenye Kilimo,Utalii na Bandari na mahusiano ya kidiplomasia tutatoboa kila mtu ataona maisha mazuri.
 
Kiuhalisia Ethiopia ni masikini sana ukilinganisha na Tanzania, kama kuna nchi tunayopaswa kujifunza kutoka kwao kwa ukanda wetu wa mashariki na pembe ya Africa basi ni Kenya. Ukweli ni mchungu lakini Kenya ndio mfano bora kabisa kwa ukanda wetu
 
..KILIMO kisipokua kwa asilimia walau asilimia 8% kwa miaka walau 5 mfululizo tutaendelea na hadithi hizihizi.

..na ukizingatia kwamba POPULATION yetu inakua haraka, basi CHALLENGES zinazowapata WAETHIOPIA za kuwa vurugu na malalamiko ya kisiasa, kiuchumi, na kijamii, zitatukabili.

NB.

..mambo haya Dr.Mpango anayafahamu vizuri. Alikuwa akiyahubiri wakati akiwa Tume ya Mipango enzi za JK.

..Namshangaa sana awamu hii Dr.Mpango amekuwa mhubiri wa Uchumi wa mashirika ya ndege. Tz siyo Dubai au Qatar wenye pesa za kuchezea kununua ndege.

Cc Dejavu, Nyanjomigire
 
Kuna msemo unasema usimdharau mwenye njaa leo maana hata wewe kesho utalia njaa.

Miaka ya 2000 Ethiopia ndio ilikuwa nchi ya 3 kutoka mwisho katika zile nchi maskini duniani(was the third poorest county in the world).Pato la mtu kwa siku was almost $650.Zaidi ya 50% ya watu walikuwa wanaishi below the global poverty line,the highest poverty rate in the world.

What happened since is miraculous.
Kuanzaia mwaka 2000-2016 Ethiopia ikawa nchi ya tatu kwa ukuaji kiuchumi duniani ikuchuana na Myanmar ambayo ni ya pili bila kusahau China ambayo ni ya kwanza huku ikizibwaga Nchi kama India,Kazakhstan na Vietnam.According to IMF Ethiopia's economy has been growing rapidly since 2003.
Mwaka 2011 umaskini wa Ethiopia ulishuka kwa 31%(very interesting)
The outlook for the next 5 years is bright.

Ifike wakati viongozi wetu wajifunze kupitia the incredible economic rise of Ethiopia na sio bla bla za kwenye social media na Tv.
Ukisoma kiundani kuhusiana na historia ya Ethiopia utagu,ndua uchumi wa Ethiopia unategemea sekta kilimo na usafirishaji.Kwa Tanzania Mungu alitubalik kila kitu ikiwemo madini,vyanzo vya maji,misitu,ardhi yenye rutuba,nguvu kazi,gesi yaaani kiufupi Mungu alitupa kila kitu cha kutufanya tuwe one of the richest country in the world lakini leo hii Tanzania ni miongoni mwa nchi maskini duniani,raia wake bado wanaishi chini ya dola miaka na miaka(what a shame).

Kwa kuhitimisha viongozi tuliowapa dhima ya kutuongoza wajue uongozi ni kitu cha kupita na sio kitu cha milele,wasidhani wayafanyayo hatuyaoni japo wanadhani wanafanyia gizani,madaraka mliyonayo isiwe silaha ya kututishia kudai mlicho tupromise kwenye majukwaa,hali ya uchumi mtaani inatisha sana na ule msemo wenu wa kusema pesa mtaani haipo kwa sababu mmeziba machaka ya wapigaji dili ni uongo mkubwa sana kutokea duniani ni kauli ya watu walioshindwa kutimiza walicho ahidi.
Asante kwa takwimu zilizoenda shule , lakini je unaweza kutuambia sababu za raia wa ethiopia kukimbia nchi yao maelfu kwa maelfu , tena kwa njia ya makontena ya kubeba mahindi badala ya usafiri halisi wa binadamu ?
 
Ni kweli uchumi wa Ethiopia unakuwa vizuri lakini siyo kwa kiwango cha kubeza rekodi ya bongo kwa kiasi hicho. Ni ajabu hukutoa takwimu katika kujega hoja yako. Unaweza kulingasha takwimu za mataifa mengine ambayo yamekumbwa pia na misukosuko mingi ya kisiasa na kijamii kama Ethiopia.

Kwa mujibu wa takwimu za karibuni za IMF, Ethiopia imewekwa kwenye kundi la nchi 28 masikini zaidi duniani kwa kigezo cha GDP, $909 wakati Sudan $992, Chad $919, Mali $917, na Rwanda $819 haipishani sana na Comoro $869. Nashauri tuwe tunaweka ushahidi wa takwimu katika kujenga hoja zetu katika masuala ya uchumi. Itapendeza.
 
Hivi unaijua Ethiopia kweli mkuu, au unaijulia kwenye hizo makala na report za IMF??

Ethiopia ni nchi yenye maendeleo ya vitu na si maendeleo ya watu. Wana reli,shirika la ndege, barabara n.k lakini watu wamechoka vibaya sana. Wewe huoni kila siku makumi kwa mamia ya waethiopia wanakamatwa Tanzania wakitoroka nchi yao mnayoiita ni ya neema wakielekea South Africa.

Mimi nimefika Ethiopia kiukweli wana shida saaaaana raia wake mpaka nilijiuliza hivi hii nchi ndio ile tunayosikia sifa zake?''....

Bongo ni bonge la nchi sema viongoz wanatutupa chini.

God Bless Tz
 
mkuu nchi hii haiendelei si kwa sababu eti ni wavivu,hatuna elimu,n.k kama ambavyo wanatuaminisha!!
tatizo ni kila baada ya miaka mitano kuna watu wanapokezana,mkuu wa nchi anateua genge lake kutafuna keki ya taifa!!
Viongozi ni wezi sana tena bila wasiwasi,wana anzisha miradi uchwara ili watuzibe macho wao wanapokwapua...!!
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom