Tanzania tuitumie historia ya John Okello na Che Guevera kama alama ya Utu na Uzalendo kwa nchi yetu

Deogratias Mutungi

Senior Member
Oct 1, 2019
137
179
Salaam Wana JF,

Leo ni tarehe 12, January siku ambayo tunakumbuka historia ya Mapinduzi Matukufu yaliyofanyika huko visiwani Zanzibar mwaka 1964, kuna historia ndefu Juu ya mapinduzi haya, Andiko hili fupi litajikita kuelezea moyo na utashi wa kizalendo kwa wanaharakati hawa wawili waliopigania mataifa yasiyo ya kwao kuhakikisha haki na dhuluma inakomeshwa kutoka kwenye utawala wa kiimla chini ya Sultani.

Mantiki kuu kaika andiko hili ni kusihi vijana kutanguliza maslahi ya umma kwanza kama ilivyokuwa kwa Field Marshal John Okello aliyeipenda Zanzibar na kujitoa kadri awezavyo ili aweze kuikomboa licha ya kwamba yeye hakuwa Mzanzibar bali mzaliwa wa Uganda Kijiji cha Lang'o mwaka 1937, Aidha ni mzalendo na alama ya kuigwa kutokana na utu aliouonyesha kwa Karume baada Mapinduzi ya Mwaka 1964.

Kama ilivyokuwa kwa Field Marshal Okello kuonyesha uzalendo kwa watu wa Zanzibar, ndivyo ilivyokuwa kwa Ernesto " Che Guevera" mzaliwa wa Argentina aliyesimama kidete kuwa tetea watu Cuba dhidi ya utawala wa kikatili wa Fulgencio Batista na hatimaye kukabidhi nchi kwa Fidel Castro, kwa ufupi unaweza ukaona utu na uzalendo wa watu hawa katika kuhakikisha haki na uhuru wa kidemokrasia unapatikana miongoni mwa mataifa ya Zanzibar na Cuba.

Swali la msingi kwa sasa je bado tunao wanaharakati, wasomi na wapambanaji dhidi ya uzalendo wa nchi au wengi wao ni "Vibaraka wanaotumiwa kuihujumu nchi" na kuibua agenda chonganishi dhidi ya watu wetu na serikali yao badala ya kujenga umoja kwa mantiki ya maendeleo endelevu?

Wakati tunasherehekea miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar ni Rai ya andiko hili kuwaomba vijana wa Kitanzania kutanguliza uzalendo kwa mataifa yao, Mantiki ya uzalendo ni pana kinadharia na kifalsafa ndani ya ukombozi wa nchi kuanzia uchumi, utamaduni, kisiasa na kijamii hivyo basi tutumie nyao za Okello na Che Guevera kuzikomboa kimawazo na falsafa jamii zetu tunazoishi badala ya kujenga hoja hasi kila siku dhidi ya mamlaka.

Natambua upo uhuru wa kikatiba katika kujieleza lakini ni vema tukajieleza kutoa maoni na kukosoa kwa misingi ya utu na uzalendo wenye fikra za kimaendeleo katika kulikomboa taifa letu, Jamii yenye vijana wengi wenye hila za kisiasa ni nadra kuwa na uzalendo wa kweli kama ilivyokuwa kwa akina Okello na Che Guevera, tunahitaji kutumia historia ya wanaharakati awa katika kuyapenda mataifa yetu kuliko kitu chochote kile kwanza.

Vijana tuwe na Mori ya Kimapinduzi katika kupigania nchi kwa mambo yenye falsafa za msingi, tutumie elimu zetu kuikomboa nchi na si kufitinishwa na mataifa ya Magharibi ambayo uifitinisha Africa kupitia tundu la "Ombwe la Demokrasia" na hatimaye kutuingiza kwenye tundu la kuzimu "Civil wars" rejea Liberia, Sierra leone, Angola na kwingineko.

Je, tumewai kuyatafakri haya, ni vema tukatambua kuwa kila taifa lina utaratibu wake wa kidemokrasia katika kuendesha shughuli zake za ndani, kinacho tugharimu Afrika ni ukosefu wa vijana wenye fikra za kizalendo kama ilivyokuwa kwa Okello na Che Guevera, Wakati tunasherehekea miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanziabar tutafakri upya falsafa za maisha yetu katika kuusimamia uzalendo wa nchi zetu.

Sikukuu njema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Deogratias Mutungi.
 
Ni kweli John Okello alikuwa na mtazamo wa Ernesto Guevara au John Okelo aliiteka Zanzibar na kuitawala kinguvu?
 
Back
Top Bottom