SoC04 Tanzania tuitakayo ni ile itakayokuwa na msingi ulio bora katika sekta mama ya elimu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Edgar71

New Member
Nov 9, 2022
2
0
Kwa Tanzania ijayo Kuna marekebisho mengi ambayo yanaweza kufanyika katika sekta mama ya ya elimu hapa nchini Tanzania na ili kuboresha mfumo wa elimu na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu bora na ya hali ya juu kabisa, Baadhi ya maoni au mapendekezo au marekebisho hayo ni pamoja na kama ifuatavyo

Kwanza, serikali ya Tanzania inatakiwa Kuongeza bajeti katika sekta hii ya elimu, Serikali inapaswa au inatakiwa kuongeza bajeti ya elimu ili kuhakikisha kuwa shule zinakuwa na miundombinu iliyo bora, yenye kuvutia katika shughuli za kujifunza,na walimu wanapata mafunzo na vifaa vya kufundishia vinapatikana kwa mwingi mfano vifaa vya maabara, vitabu na nyenzo mbalimbali za kujifunzia mashuleni.

Pili, serikali ya Tanzania inatakiwa Kuboresha mfumo wa mafunzo kwa walimu, Walimu wanapaswa kupata mafunzo yaliyo bora na ya mara kwa mara ili waweze kufundisha wanafunzi kwa ufanisi zaidi na kutengeneza wanafunzi watakao kuwa wana uwezo mkubwa wa kufikiria na kuweza kufanyia kazi kile wanachojifunza darasani kwa vitendo katika maisha yao ya kila siku.

Tatu,natamani kuona serikali ikipanua wigo wa elimu bure katika shule zetu za msingi na sekondari au upili, Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inapaswa kuhakikisha kuwa elimu ya msingi na sekondari ni bure inakuwa endelevu kwa kila mtoto ili kuhakikisha kuwa hakuna mtoto anayeachwa nyuma katika kuhudhuria shuleni ukilinganisha na miaka ya zamani vijana wengi walikuwa hawaendi shule kwa sababu ya uwepo wa ada mashuleni ili Hali ya uchumi katika familia zao hauko vizuri.

Nne, serikali yetu inatakiwa Kukuza elimu ya ufundi kupitia wizara yake tukufu ya elimu, Elimu ya ufundi kwa nchi yetu ya Tanzania inatakiwa na inapaswa kutiliwa mkazo ili kuhakikisha kuwa vijana wanapata ujuzi wa kufanya vitu kwa vitendo na hivo watapata Maarifa ya kutosha kuingia katika soko la ajira ndani na nje ya Tanzania kufikia 2035.

Tano,serikali inatakiwa Kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum katika sekta hii ya elimu mfano wanafunzi wasioona yaani vipofu, viziwi, wasioongea hivo Serikali inapaswa kutoa msaada wa kutosha kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum ili waweze kusoma kwa ufanisi na kufikia malengo yao ya elimu na ukiangalia vijana wengi wenye mahitaji maalum wapo na vipaji maaalumu lakini kukosekana kwa miundombinu inayoruhusu wao kujifunza wanashindwa kufikia ndoto zao kikamilifu .

Sita, serikali inatakiwa kuboresha miundombinu ikiwemo madarasani,vyoo ofisi, maabara na maktaba ili kuwepo na wepesi katika kujifunza hata kwa vitendo mashuleni ifikapo 2035

Saba,
Naishauri serikali kupitia wizara yake ya elimu mishara na ajira kwa walimu ziongeezeke ili kuhakikisha shule mbalimbali zinakuwa na walimu na wataalamu waliobobea katika fani mbalimbali za elimu, lengo ni kuinua kiwango cha ufaulu mashuleni na elimu kwa ujumla

Nane, ili tufukie Tanzania tuitakayo mtaala wa elimu uendelee Kufanyiwa marekebisho mara kwa mara na Kufanyiwa majaribio mashuleni ili kuona faida na hasara zake, napendekeza kufikia 2030 mfumo wa kujifunza kwa vitendo uwe asilimia 80%

Hivo bhasi mimi kama mdau katika sekta ya elimu, Kwa kufanya marekebisho haya na mengine mengi yaliyopo mashuleni , Tanzania inaweza kuboresha mfumo wake katika sekta ya elimu na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu bora ya kiwango cha juu kabisa au ya hali ya juu.
 
kufundisha wanafunzi kwa ufanisi zaidi na kutengeneza wanafunzi watakao kuwa wana uwezo mkubwa wa kufikiria na kuweza kufanyia kazi kile wanachojifunza darasani kwa vitendo katika maisha yao ya kila siku.
Hakika elimu tunayoihitaji kuwa. Tuweze kuyatawala na kuyaishi mazingira yetu kiufanisi. Na ndiyo kipimo cha akili ya Taifa.
,natamani kuona serikali ikipanua wigo wa elimu bure katika shule zetu za msingi na sekondari au upili, Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inapaswa kuhakikisha kuwa elimu ya msingi na sekondari ni bure inakuwa endelevu kwa kila mtoto ili kuhakikisha kuwa hakuna mtoto anayeachwa nyuma katika kuhudhuria shuleni
Linaweza kulipuka kwa kushusha kiwango cha wazazi na watu binafsi kuithamini na kuiheshimu elimu. Je mtoa mada hauhisinkwamba kucjangia gharama kidogo kunaongeza ufanisi zaidi wa elimu??

serikali inatakiwa kuboresha miundombinu ikiwemo madarasani,vyoo ofisi, maabara na maktaba ili kuwepo na wepesi katika kujifunza hata kwa vitendo mashuleni ifikapo 2035
Hivi ndio vitu serikali inapaswa kufanya sasa, vile vya jumlajumla kama majengo na si binafsi kama sare na ada. Kila mmoja awajibike kwa nafasi yake.

Hivo bhasi mimi kama mdau katika sekta ya elimu, Kwa kufanya marekebisho haya na mengine mengi yaliyopo mashuleni , Tanzania inaweza kuboresha mfumo wake katika sekta ya elimu na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu bora ya kiwango cha juu kabisa au ya hali ya juu.
Ahsante sana kwa mchango mwema
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom