Kwanza kabisa nianze kwa kumshukuru sana MWENYENZI MUNGU atupaye afya,nguvu,neema na kibali siku hadi siku kwenye majukumu yetu yote.
Pili nitumie uwanja huu kulishukuru jukwaa la Jamiiforums kwa namna yao ya pekee sana wanavyoelimisha jamii katika nyanja zote za maisha.
Tatu na mwisho niwashukuru wapenzi wote wa Jamiiforums pamoja na washiriki wenzangu kwenye msimu huu wa 2024 hakika kila mmoja kwa nafasi ya kujiona wa thamani sana najivunia kila aliyepo na asiyekuwepo lakini anayo Nia ya dhati na nchi yetu Tanzania.
Sasa naomba niende moja kwa moja kwenye kile ambacho nimekiona kwa mawazo yangu kuhusu Tanzania Tuitakayo miaka 5 hadi 25 ijayo.Nitajikita zaidi kwenye mfumo wa utawala,elimu ya msingi pamoja na afya kwa kila mwananchi.
Ni muhimu sana kutafakari na kujadili kuhusu mustakabali wa nchi yetu kwa Leo,kesho,na hata siku zijazo zaidi kwenye utawala.Binafsi ni tamanio la moyo wangu na ndoto yangu kuiona nchi yangu Tanzania ikiwa na utawala unaoheshimu itikadi tofauti za kisiasa,mfumo wa utawala ambao utaruhusu mabadiliko ya mifumo ya utawala bila uwepo wa uroho wa madaraka lakini pia mfumo wa utawala ambao utaweka maslahi ya watu wake mbele kwanza.
1. Utawala Bora na heshima kwa itikadi tofauti za kisiasa,natamani Tanzania Tuitakayo miaka 5 hadi 25 ijayo izingatie kuheshimu itikadi tofauti za kisiasa.Tunaamini katika uhuru wa kujieleza na haki ya kila raia kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia. Tanzania niitakayo ni Ile ambayo vyama vya siasa vitafanya kazi kwa ushirikiano bila vitisho wala ubaguzi,iwe Tanzania ambayo viongozi wataheshimiana na kutambua kwamba tofauti za kisiasa siyo za kutugawa wala sio udhaifu bali iwe nguvu ya kushikamana kuliongoza Taifa katika misingi bora ya utawala. Iwe sehemu ya kujenga mazingira mazuri ya kisiasa ambapo kila sauti itasikika na kila wazo litaheshimika kuanzia Kwa raia wa kawaida hadi kwa kiongozi.
2. Mfumo wa kubadilishana utawala bila kuwepo kwa uroho wa madaraka. Tanzania ninayotamani niione miaka 5 hadi 25 ijayo ni Ile itakayoruhusu mabadiliko ya mifumo ya utawala bila uroho wa madaraka. Binafsi ni muumini wa demokrasia hivyo natamani Tanzania Tuitakayo miaka 5 hadi 25 ijayo iwe na mabadiliko ya utawala Ili kuonja ladha zingine za uongozi,yaani viongozi warithishane kipawa cha uongozi kwani kwa jinsi MUNGU alivyogawa vipawa wapo ambao wanatamani kuonesha vipawa vya uongozi walio nao. Viongozi wabadilishane madaraka kwa amani na kwa kufuata katiba. Lengo kuu la kubadilishana utawala liwe ni kuwahudumia wananchi siyo kung'ang'ania madaraka.
3. Kuwaweka wananchi mbele, natamani Tanzania Tuitakayo miaka 5 hadi 25 ijayo iwe ile ambayo itawaweka watu wake mbele kwanza linapokuja suala la maslahi ya Taifa kwani halipo Taifa bila watu na hakuna kiongozi pasipo watu. Ni muhimu viongozi kutambua kwamba wao ni watumishi wa raia walio wengi hivyo linapokuja suala la maslahi ya Taifa basi ijikite sana katika kuweka mipango inayolenga kuboresha maisha ya Watanzania wote bila kujali hali zao za kijamii na kiuchumi. Iwe Tanzania ambayo viongozi kwa dhati watajitolea kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata fursa ya kuishi maisha yenye heshima na utu.
4. Kukemea uongo na kuwaambia viongozi ukweli. Ndugu zangu ni muhimu tujifunze kusema ukweli. Tanzania Tuitakayo miaka 5 hadi 25 ijayo iwe na viongozi wawajibikaji pale wanapokosea, wanapokosolewa kwa ukweli na uwazi. Lakini kubwa tuwakatae wale ambao wanawapamba viongozi hata pale wanapokosea,wale wanaowatukuza viongozi kwa maneno matamu kwa maslahi yao binafsi pasipo kuwaambia ukweli mchungu ili wajirekebishe,kundi hili lisivumiliwe hata kidogo tena kiongozi atakayepata kupambwa na mtu wa aina hii amweke kando kabisa kwasababu haitakii mema nchi yetu Tanzania. Ni jukumu letu sote kuwa waangalizi wa utawala bora na kuhakikisha kuwa tunawawajibisha viongozi wetu kwa matendo yao. Ukweli ni msingi wa maendeleo na pasipo ukweli hatutaweza kulijenga Taifa lenye haki na usawa.
5. Sekta ya elimu, elimu ndiyo msingi wa maendeleo ya Taifa lolote. Tanzania Tuitakayo miaka 5 hadi 25 ijayo ni ile itakayoweka kipaumbele katika mfumo wa elimu ya msingi kwani hapo ndipo tunapoandaa msingi imara wa maisha ya mtoto wa Kitanzania. Ni vyema kuweka mpango kazi wa muda mrefu kuhusu mitaala ya elimu kwani kumekuwepo na mabadiliko kadha wa kadha ya mitaala kwa muda mfupi mfupi, natamani Tanzania ipate mtaala thabiti ambao utachukua muda mrefu bila mabadiliko ambao utampa mtoto uwezo wa kufikiri kwa kina na kujifunza kwa ubunifu. Tanzania Tuitakayo miaka 5 hadi 25 ijayo iandae mtaala thabiti wa elimu ya msingi ambao utazingatia sio tu maarifa, bali pia maadili mazuri ya watoto, ubunifu na ujuzi wa maisha. Lakini pia Tanzania niitakayo miaka 5 hadi 25 ijayo natamani itoe mafunzo ya kutosha na nyenzo za kufundishia ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Ni muhimu Tanzania Tuitakayo miaka 5 hadi 25 ijayo iwe na dira na mpango wa muda mrefu katika sekta ya elimu ili hata walimu wetu wapate kufundisha kwa utulivu na watoto wapate elimu bora itakayowaanda kwa maisha yao ya baadae.
6. Sekta ya afya ( matibabu kwa wote ), sekta ya afya ni muhimu sana kwa ustawi wa wananchi wa Taifa letu. Naitamani Tanzania Tuitakayo miaka 5 hadi 25 ijayo kila mwananchi apate huduma bora ya afya bila kuhangaika na gharama kubwa za matibabu. Ili kufanikisha jambo hili binafsi ninayo mapendekezo yafuatayo ;
( a ) kuanzishwe utaratibu wa kila raia kuchangia huduma ya afya yake kila mwezi awe ataumwa au hataumwa kwasababu afya ni kitu nyeti sana na mtu anapougua ghafla wanaopata shida ni wale wanaomzunguka kuhangaika kutafuta pesa za kumpeleka kwenye matibabu lakini endapo mtu huyo amewekeza kwenye akaunti ya afya yake ni rahisi sana kupata huduma ya matibabu bila kuwatesa wale watu wake wa karibu.
( b ) pia kama itawezekana itengwe bidhaa moja kitaifa ambayo kila raia ni lazima ainunue yaani ni ile bidhaa muhimu sana kwa kila mwananchi, bidhaa hiyo iwekwe kodi ambayo haitakuumiza mwananchi kodi hiyo iende moja kwa moja kwenye mfuko wa afya lengo ni kuboresha maisha ya kila mwananchi kupata huduma ya afya bila kuhangaika.
Endapo tukiyaboresha mawazo haya ambayo nimeyapendekeza basi Tanzania Tuitakayo miaka 5 hadi 25 ijayo itakuwa sehemu ya furaha sana kwa wananchi wa Kitanzania kwani watakuwa na uhakika wa kupata huduma ya matibabu bila kuwa na pesa.
Ndugu Watanzania wenzangu ndoto hii ya Tanzania Tuitakayo miaka 5 hadi 25 ijayo inaweza kutimia. Ni matumaini yangu kuwa ni ndoto ya kila Taifa kuwa na utawala bora unaosifika na raia wote,pia ni ndoto ya kila Taifa kuona mifumo ya elimu na afya inakuwa thabiti inayowapa watu wake matumaini, furaha na tabasamu la muda wote.
Tuanze sasa hii safari ya kuitengeneza Tanzania Tuitakayo miaka 5 hadi 25 ijayo kuanzia sasa kwa kuhakikisha mifumo ya utawala bora unaoheshimu itikadi tofauti za kisiasa unaanza kutekelezeka kwa vitendo, na mifumo ya elimu na afya inawekwa vyema kwa ajili ya kizazi kijacho kikafurahie wazazi wao kufanya maamuzi mazuri.
Naomba nihitimishe mawazo yangu kwa kunukuu maneno ya Nishan Panwar yasemayo hivi " Naweza nisiwe na uwezo wa kuwapa watoto wangu kila kitu wanachokitaka lakini nitawapa yale mambo muhimu wanayoyahitaji kutoka kwangu ambayo ni upendo, muda na uangalifu " kwa maneno haya ni dhahiri kwamba Tanzania ni kama baba au mama wa familia inaweza isiwe na uwezo wa kufanya yote ambayo Watanzania wanataka lakini ikawapa yale mambo muhimu wanayoyahitaji kama utawala bora, elimu safi na afya njema Kwa Watanzania wote.
MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU BARIKI WATANZANIA WOTE, MUNGU IBARIKI PLATFORM HII YA JAMIIFORUM,AMEN.
Asanteni.