Tanzania tuchague lugha ya Kiswahili au ya Kiingereza

Haki

JF-Expert Member
Jan 14, 2009
356
17
Tanzania ni taifa kubwa katika A.Mashariki. Cha kushangaza ni kwamba hatuna ONE OFFICIAL language. Tunatumia Kiswahili mitaani, kwenye mikutano,nk. lakini tunafundishwa Kiingereza mashuleni na text books zote ni za Kiingereza. Sasa kwanini tusifundishwe au tutumie lugha moja tu? ikiwa Kiswahili au Kiingereza. Kuna ushahidi unaonyesha kwamba: Wanafunzi wengi wanafeli kwa sababu hawaelewi vizuri Kiingereza. Hii yote inasababishwa na mchanganyiko wa lugha. Chukulia mfano mwanafunzi wa High School kutoka Uingereza anayetumia Kiingereza afundishwe Kiswahili ktk masomo yake. Je atapasi vizuri?
Nchi nyingi zilizoendelea zinatumia lugha moja tu kama Uingereza, Marekani, Iran, China, Italy, France, Russia, Israel nk. Kwa mfano Nyerere alitaka Kiswahili kiwe lugha ya Taifa na kitumiwe kwenye text book ktk Universities. Kuna umuhimu mkubwa kwa TZ kutumia lugha moja mashuleni, iwe Kiswahili au Kiingereza.
 
Tatizo sio lugha mbili, tatizo kiingereza hakifundishwi vizuri, kama sikosei tulianza kufundishwa kiingereza darasa la tatu, mpaka la saba ni miaka 4, ambayo inatosha kujifunza lugha yoyote . Tena ikiwezekana waanze kufundisha mapema zaidi, hii itaondoa ule woga wa lugha ambao watu wengi wanao.
 
Mfumo mbovu wa elimu wa Tanzania umechangia sana kuwafanya wanafunzi wengi kufeli. Kuna professor mmoja alikuwa anazungumzia kwamba, TZ kuna maingeneer wengi waliohitimu elimu ya juu lakini hawajui hata kutengeza filimbi. Huu ni mfano mkubwa kwamba serikali ichague lugha moja tu kama nchi zingine zilizoendelea.
 
masomo yote yawe kwa kiingereza kuanzia darasa la kwanza thats the answer.na pia tuwajali walimu wetu hili itoe changa moto na kuleta upinzani na kuweza kutoa walimu bora.
 
Mfumo mbovu wa elimu wa Tanzania umechangia sana kuwafanya wanafunzi wengi kufeli. Kuna professor mmoja alikuwa anazungumzia kwamba, TZ kuna maingeneer wengi waliohitimu elimu ya juu lakini hawajui hata kutengeza filimbi. Huu ni mfano mkubwa kwamba serikali ichague lugha moja tu kama nchi zingine zilizoendelea.

Suala la ma-engineer kutoweza kutengeneza hata filimbi ni kwamba elimu zetu zimejaa nadharia kwa wingi kuliko vitendo. Na hii inasababishwa na maabara za vyuo vyetu kutokuwa na vifaa vya kuweza kuwafundisha hawa engineers kutengeneza hivyo vitu. Pia hatuna viwanda vya kuwapeleka kupata ujuzi wa kutengeneza hivyo vitu kwahiyo wanaishia kuvisoma kwenye vitabu na kuchora michoro tu basi. Kwahiyo serikali inabidi iamue kuwekeza katika elimu ili kutoa engineers wenye uwezo wa kutengeneza vitu. Na hili linawezekana tatizo ni kutokuweka kipaumbele katika mambo yenye kuleta maendeleo badala yake maslahi binafsi ndo yametawala kwa viongozi wetu. Chukulia kwa mfano pesa za EPA bilioni 133 robo yake tu ingeweza kuleta mabadiliko makubwa mno katika maabara ya vyuo vikuu vyetu na kuongeza ubora wa elimu yetu.
Kutokana na kukosekana kwa vitendo (practicals) wanafunzi wengi wanasoma kufaulu mitihani tu.
Leo hii tunao engineers wengi tu ambao ni walimu shule za sekondari na wengine ni tellers katika mabenki, tatizo ni nini? Jibu: hawana mahali pa kwenda kufanyakazi za u-engineer.
 
Maoni yangu ni yafuatayo...

1. Primary schools hazitufundishi kiingereza cha kutosha kufanikiwa kuelewa masomo ya shule za sekondari... wengi wanafeli kwa sababu ya kutoelewa masomo ... cramming kukumbuka swali na jibu badala ya kuelewa masomo hufelisha wengi sana, manake swali likibadilishwa lugha kidogo, basi hawajui jibu ni lile walilo cram. Tunajifunza kiswahili tokea tukizaliwa, kwa nini tusifundishwe kutumia kiingereza tokea darasa la kwanza? wengi wataelewa masomo ya sekondari, tukifundishwa ivo. Afu pia, tutaweza kushindana vizuri kimasomo vyuoni popote duniani, na pia kijana alieweza kutengeneza filimbi ya mwanzi atarudi tokea chuoni akijua kutengeneza filimbi babkubwa, ya chuma ama mwanzi.

2. Nchi yetu bado haina uwezo ama vyuo vingi vya kutusomesha vijana wote walio tayari kuingia vyuoni, kwa hiyo, bado tutahitaji kusafiri ng'ambo kusoma... tunahitaji ku-master kiingereza kwa sababu nilizojadili apo juu (#1).

ps: Naipenda lugha yetu, kwa hiyo simaanishi tuitupe... ila kweli, tunazaliwa tukiongea kiswahili, na pia tunaongea kiswahili nje ya madarasa, magazetini, vitabuni, ... na pia shule za sekondari zina darasa la kiswahili kutufundisha kizito...
 
Back
Top Bottom