The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 19,254
- 42,873
Kama hujui mambo ya ndege kaa kimya. Kila ndege ina jina kama mbwa. utakumbuka tz tulikua na ndege zinaitwa KILIMANJARO...SERENGETI.....NGORONGORO etc. hii yao inaitwa Kilimanjaro. kuna nyingine inaitwa Udzungwa. unajua wakenya wanazo ndege 47 zote kubwa. hata moja kama yao hatuna.
Sawa mkubwa, nimekuelewa unaejua mambo ya ndege, acha nikae kimya japo unaelewa mambo ya ndege lakini umeshindwa kuelewa nilichokiandika hapo.
Maelezo yako yana ukweli lakini haimaanishi wao kutumia Kilimanjaro ni jina tu wanaandika ili mradi jina, ina impact kubwa kwenye biashara ya utalii.
Pili ni aibu sisi kama taifa kuwa na shirika la ndege ambalo aidha limekufa au linalegalega. Hicho ndio kilichokua kimebebwa kwenye hayo maandishi yangu.
Na hapo ndio utaanza kuona kwa nini viongozi wetu wana woga wa kujiingiza moja kwa moja kwenye East Africa kwa kuogopa wenzetu kutumia fursa zilizopo kwetu. Badala ya kupinga, tulitakiwa tufanye kitu ili kuboresha na kuwa tayari kushindana badala ya kuzuia.