Kampuni moja tu kuingiza mafuta nchini

Mtanganyika

JF-Expert Member
Jul 18, 2007
1,601
945
Na ITV Habari

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji- EWURA, inaandaa utaratibu mpya wa uagizaji wa bidhaa za mafuta ya petroli kutoka nje ambapo zitakuwa zikiingizwa na kampuni moja tu itakayoshinda zabuni ikiwa ni hatua ya kudhibiti bei na ubora wa mafuta hayo.

Akizungumza katika mahojiano maalum na ITV bw. Masebu amebainisha kuwa chini ya utaratibu mpya, kampuni itakayoshinda zabuni itaagiza mafuta yanayotosheleza mahitaji ya nchi kwa muda usiopungua miezi mitatu.

source IPP Media

Jee tunaweza kuafford msambazaji mmoja wa mafuta? Kama hakuna ushindani nini kitamfanya msambazaji auze bei ya kawaida?

Mtanzania wa kawaida ndio anaumiwa mwisho wa siku kutokana na maamuzi ya kipuuzi kama haya.
 
/rushwa inakaribishwa hapo,unakumbuka kipindi cha TIOT?lets wait and see new scandal
 
Total monopoly...Hivi baada ya hiyo miezi mitatu zabuni nyingine itafunguliwa? Je kampuni hii ikaongeza bei kwa manufaa yao na kufanya isiwe kwa manufaa ya Mtanzania itakuwaje mzabuni mwingine au?
Sijui tunaenda wapi...!
 
Nilijiuliza maswali mengi sana nilipoona hii article. Who decides about import and export agreement? Nilidhani ni bunge la Tanzania. JK can't change anything in this country, too many self interest movement.
 
Just for your inf Haruna Masebu is one of the Untouchables... just check his connections tokea alipokuwa Mwalimu pale ARDHI Institute...then GM NHC then...

Jamaa ni Kichwa Kizuri sana (very intelligent)... lakini hili jambo analotaka ku-impose... somehow something somewhere is not straightforward
 
Back
Top Bottom