Tanzania: The Best Democracy.

Mwanafalsafa

Senior Member
Jun 24, 2007
158
225
Ni habari nzuri lakini angalia kama ni kaforum kapya kasije kakawa kanatafuta "Page Rank" kupitia forum hii ambayo tayari iko juu.

"Page Rank" ni kupanda chati za Google ambapo ikiwa website yako imebandikwa kwenye website yenye Rank ya juu zaidi pasipo reciprocal link basi unapata point nyingi zaidi na kupiga hatua kubwa kuelekea juu ya chati za Google.
 

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,700
1,250
Ni kweli tunayo Demokrasia yenye uhafadhali kuliko ndugu zetu wa Kenya na Uganda.

Kama Mkenya alivyodai, tunaweza tusiwe na uchumi mzuri kama wao, lakini baadhi ya Taasisi zetu zinajitahidi kufanya vizuri.

Lakini kuna kitu ambacho Tanzania inacho ambacho nchi nyingi za kiafrika hazina - Umoja na Undugu wetu. Na kwa hili napenda kumsifu sana Mwl. JK Nyerere . . . .

Kwa nini tusiwe ndugu na kwa nini tusiwe na umoja? Mwalimu alihakikisha anajenga mfumo ambao leo hii ndiyo tunajivunia. Kivipi?

Mathalani . . . .

Umezaliwa Mbeya . . . Primary Umesesoma Mbeya kwa Wanyakyusa (Miaka 7). . . ukafaulu

Secondary unaenda Old Moshi (Na Warranty ya TRC wakati huo) unaenda kukutana na wachaga na wengine kutoka mikoa mbalimbali (Miaka 4).

High School unaenda Kibaha Secondary, huko unakutana na Watu vwa Pwani na wengine toka mikoa Mingine (Miaka 2)

Jeshini JKT Ruvu miezi 6 - Mnakutana makabila mbalimbali na matabaka mbalimbali

Service - Buhemba Miezi 6 - Unakutana na wakulya na makabila mengine.

Kisha - Chuo Kikuu - unakutana na watu tofauti na makabila tofauti (Miaka 3 hadi 5)

Kisha kazi unaanza Rukwa - Sumbawanga unafanya miaka 3, kisha unahamishiwa Dodoma n.k.

Hebu niambie Ukabila utatoka wapi? Ukifika wakati wa kuoa au kuolewa unamchagua myu unayemfahamu aliye karibu na wewe bila kujali kabila wala dini (to some extent).

Haya ndio maombo yaliyotuunganisha kwa kiasi kikubwa na tujione ndugu. Mtaji mabao ndugu zetu wa CCM wanautumia wao wakiuita - AMANi, UMOJA, NA MSHIKAMANO. Ni kutokana na hilo ndiyo maana siasa za Tanzania hazina vurugu za watu kuuwawa au kutoana ngeu.

Mwalimu JKN anaweza akawa alituacha masikini, lakini leo hii tunaishi kwa amani na upendo tofauti na ndugu zetu amabo uchumi wao ni mkubwa lakini kila election ikifika lazima watu wafe na isitoshe vurugu za ukabila zimeota mizizi.
 
Top Bottom