Tanzania: Tatizo la ajira kwa vijana ni kubwa sana, lisifanyiwe masihara!

Habari wana Bodi

Tunapozungumzia tatizo la ajira kwa vijana, sio tu wale ambao hawana kazi kabisa, ila inajumuisha mpaka wale ambao wapo kwenye ajira, lakini wanapata ubaguzi au manyanyaso flani flani, bila kuwa na njia ya kujikwamua.

Ni muda mrefu sasa, hili swala limekua likijadiliwa na kuendelea kujadiliwa bila kupata ufumbuzi, hadi imefika paala, sisi vijana ambao tuko kwenye hili tatizo tunaonekana kama bomu linalotaka kulipuka (tunafananishwa na bomu).

Kwa hapa tulipofikia, Serikali hii ina-ajiri kwa kiwango kidogo sana na kupelekea vijana wengi kutegemea ajira kwenye sekta binafsi (kuajiriwa au kujiari)

Kwe upande wa ajira za kuajiriwa kwenye sekta binafsi, kwa sasa, WA-INDI ndio wamekua wakipewa kipaumbele kana kwamba wao ni waTanzania huku mTanzania mimi na wewe tukiachwa. Makampuni makubwa yamekua yakiajiri waIndi na kuwalipa mishaara minono kwa kazi ambazo zinaweza kufanywa na waTanzania wenye elimu hiyo.

Tukija kwenye hizi biashara ndogo ndogo, WACHINA ndio wamejazana huko. Hizi biashara ndogo ndogo zilitakiwa ziachwe zifanywe na wazawa, ili kuweza kukuza, middle income. Kusingekua na mafuliko ya hawa wachina, leo hii vijana wengi wangekuwa wanamoyo wa kuingia mtaani na kujiajiri au kwa wale walioajiliwa, kutumia akiba yao kidogo kufungua hizi biashara ndogo ndogo. Kwa kufanya hivi kungesaidia kwa kiasi fulani tatizo hili

Sio kwamba Serikali haioni au haijui haya matatizo, wanaona na wanajua, ila wameamua kutuacha ili KUTUKOMESHA. Imefika wakati sasa, ingawa upo nchini mwako, unakuwa kama mtumwa vile na hii ni kwa sababu ya hii serikali kuwathamini hawa waHindi na wachina.

HITIMISHO

Vijana, umefika wakati inatupasa tutambue sasa hivi sisi ni kama watoto yatima, inatupasa tutambue kwa hali ilipofikia hata ukiwa na Masters utaishia kuwa-frustrated, na hii ni kutokana na mfumo uliopo. Tutambue kuwa serikali hii haina tena msaada na sisi, kwani kama wangekua wanafanya juhudi za kutatua hili tatozo, tokea 2010 hadi leo 2013, angalau dalili za unafuu tungeanza kuziona. Tutambue kuwa hawa watu hawana huruma nasi.

Vijana, inatupasa tujifunze kutoka hata kwa nchi jirani ya Kenya, walivyo wakali kuhusu ajira zao za ndani, hawataki maskhara kabisa.

Vijana, inatupasa tuwe na kauli moja kuwa hii serikali sasa inatosha, wanatakiwa watoke madaraki (IWE KWA HIARI AU KWA NGUVU YA UMMA), ili kupisha serikali nyingine ambayo itakuwa sikivu na kuweza kuona hili tatizo la vijana kuwa sio bomu. Lakini tukiendelea kulalamika, haitatusaidia na tutaendelea kuumia tu
 
Nchi zilizoendela na zinazoendele zimekuwa na takwimu za mara kwa mara za watu ambao hawana ajira.Kwa mfano,kwa mwaka huu Marekani unemployment rate inaonyesha ni 7.3% na UK ni 7.8 nakadhalika.

Swali:Unemployment rate ya Tanzania ni aslimia ngapi kwa mwaka huu na mwaka jana?Serikali inazo takwimu za uhakika kweli?Hata hizo za uongo zipo?Au ni kama ile ishu ya mitaala ya Mbatia mpaka leo haionekani?

NB:Support hoja zako kwa data..acha porojo za uchama na kama data hakuna sema wazi..hakuna!
 
nadhan hata takwimu hakuna... hakuna pesa za kufanya huu utafiti ila taasisi kama REDET ya wasomi uchwara wachache pale mlimani zina pesa za kufanya utafiti wa kupima umaarufu wa rais Kikwete baada ya miaka mitano ya uongozi wake!!!
 
Na huu ndo ulofa tulo nao.Sasa kama takwimu muhimu kama hizi hakuna tatizo la ajira kwa vijana litatatuliwaje?si bure watu wameamua kuwa "punda" wabeba sembe.REDET nao ni wachumia tumbo tu...
 
Nchi zilizoendela na zinazoendele zimekuwa na takwimu za mara kwa mara za watu ambao hawana ajira.Kwa mfano,kwa mwaka huu Marekani unemployment rate inaonyesha ni 7.3% na UK ni 7.8 nakadhalika.Swali:Unemployment rate ya Tanzania ni aslimia ngapi kwa mwaka huu na mwaka jana?Serikali inazo takwimu za uhakika kweli?Hata hizo za uongo zipo?Au ni kama ile ishu ya mitaala ya Mbatia mpaka leo haionekani?
NB:Support hoja zako kwa data..acha porojo za uchama na kama data hakuna sema wazi..hakuna!

Siwezi kukupa data na wala hatupewa. Taarifa ya idadi ya Watanzania kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2012 ina walakini kwani baadhi ya watu walithibitisha wakati ule kwamba taarifa zao hazikuandikwa. Unachotaka kukijua ni kitu kigumu sana na wala hilo halipo katika vipaumbele vya nchi hii. serikali ya nchi hii ipo likizo katika mambo ya msingi yahusuyo nchi. Kwa mbali viongozi wa serikali wapo kwenye dili za madawa ya kulevya, biashara zingine (kwa kukwepa kodi), wizi wa fedha za umma na kuidhibiti Chadema. Zaidi ya hayo kwa mbali sasa hivi kuna single mpya hapo serikalini ya Big Result Now. Hiyo Big Result Now waalimu wamesema haitawezekana bila Big Salary Now. Huo mziku sijui kama tutauweza.
 
mimi mpaka leo huwa sielewi hata kufahamu kazaiya National
Bureau of Statistics.
I have never seen any seen any single helpful and informative piece of info toka kwao.
mniwie radhi mnaopata ugali hapo..povu lisiwatike but sijui hata kazi yenu..very sad
Am out..
 
NASHUKURU KWA MAELEZO MKUU...Big Result now bila data ni usanii mtupu!
 
Kwa hapa kwetu wala hakuitaji pesa nyingi ku fanya hiyo research... Waende pale kwa wale vichaa wanaojiita "Tume ya Ajira" watapata statistics za ma-barua ya maombi, then watapata majibu ni kwa kiasi gani vijana (bomu linalosubiri kulipuka) wanavyotaabika mtaani....
 
Kuna data humu eti wamesema as it stands unmemployment rate 10.7% huu si uongo wa wazi kabisa huu?Leo hii ukitangaza kazi ya mshahara wa laki 3.5 utaletewa barua mpaka za watu wenye masters zao!
 
Nimesoma hii link...source yake ni Tanzania Bureau of Statistics.My take...well cooked data to say the least.Eti mpaka January 2012 unemplyoment rate ni 10.7%?really?In maana ktk kila watu 100 at least 10 hawana kazi?Nooop!The problem is bigger than the data suggests!

The government is playing makida makida with Tanzanians on this critical issue. Inatumia nguvu nyingi katika kuidhibiti CHADEMA wanashindwa kujua kuwa majority wanakipenda hiki chama kwasababu hawaoni juhudi zozote za serikali katika kutatua haya matatizo likiwa hili la ajira Tanzania. La msingi ni kutambua kuwa CCM haina jipya, haina mkakati wowote madhubuti wa kuitoa hii nchi hapa ilipokwama kwenye hili janga la umasikini.
 
Hakuna kinachinisikitisha kama kuona zero effort kutoka serikalini kukabiliana na tatizo la ajira.Infact as we speak kuna wageni kibao tu kwenye sekta za utalii ,elimu na madini.Yaani hata kulinda hivi viajira vichache bado tunashindwa.Wakenya na waganda wamejaa kwenye shule za English-medium,hoteli za kitalii zimejaa waajiriwa wageni sasa kuna sababu gani ya kuanzisha vyuo kama UDOM nia vingine?......tungoje bomu lilipuke!
 
Nchi zilizoendela na zinazoendele zimekuwa na takwimu za mara kwa mara za watu ambao hawana ajira.Kwa mfano,kwa mwaka huu Marekani unemployment rate inaonyesha ni 7.3% na UK ni 7.8 nakadhalika.Swali:Unemployment rate ya Tanzania ni aslimia ngapi kwa mwaka huu na mwaka jana?Serikali inazo takwimu za uhakika kweli?Hata hizo za uongo zipo?Au ni kama ile ishu ya mitaala ya Mbatia mpaka leo haionekani?
NB:Support hoja zako kwa data..acha porojo za uchama na kama data hakuna sema wazi..hakuna!

Acha kuzunguka mbuyu, sema tu unafanya research
 
Kuna data humu eti wamesema as it stands unmemployment rate 10.7% huu si uongo wa wazi kabisa huu?Leo hii ukitangaza kazi ya mshahara wa laki 3.5 utaletewa barua mpaka za watu wenye masters zao!

Mkuu hii serikali haipo serious kwenye swala la ajira. Ajira ni ngumu sana kupata, watu wanazunguka na bahasha zao mpaka bahasha zimepata fungus... Ndio maana siku hizi vijana wameamua kulelewa na mashugamami, ili maisha yasonge mbele...

Lakini na sisi vijana ukimya wetu ni tatizo, we need to rise our voice...
 
Sisi watanzania wapole sana mkuu....labda mpaka tubanwe saaaana na maisha na tuanze kula nyasi...we might rise our voices!Hii ishu ni ngumu mno kaka as you said.Kuna mdada namjua na Masters yake anauza kaduka ka vinyago...mind you sii lake,kaajiriwa...shame!
 
mimi mpaka leo huwa sielewi hata kufahamu kazaiya National
Bureau of Statistics.
I have never seen any seen any single helpful and informative piece of info toka kwao.
mniwie radhi mnaopata ugali hapo..povu lisiwatike but sijui hata kazi yenu..very sad
Am out..

Uwepo tu wa ofisi ya namna hii katika nchi yetu na wewe kuitambua kwamba ipo tena pale Kivukoni front jirani na ofisi ya bw. Membe na Wizara ya Fedha ni hatua nzuri sana ya kuanza kuitambua ofisi hiyo na majukumu yake na kile ambacho inafanya na imekuwa ikifanya. Nakupongeza sana maana ni wadanganyika wachache wanaoifahamu ofisi hii hata kuweza uitaja kama ulivyofanya!!
 
Nchi zilizoendela na zinazoendele zimekuwa na takwimu za mara kwa mara za watu ambao hawana ajira.Kwa mfano,kwa mwaka huu Marekani unemployment rate inaonyesha ni 7.3% na UK ni 7.8 nakadhalika.

Swali:Unemployment rate ya Tanzania ni aslimia ngapi kwa mwaka huu na mwaka jana?Serikali inazo takwimu za uhakika kweli?Hata hizo za uongo zipo?Au ni kama ile ishu ya mitaala ya Mbatia mpaka leo haionekani?

NB:Support hoja zako kwa data..acha porojo za uchama na kama data hakuna sema wazi..hakuna!

Mashavu yako unataka kutugeuza sample ya research yako eeh? Vilaza mnatusumbua sana.
 
Back
Top Bottom