Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wotee.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wotee....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 29, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,610
  Likes Received: 82,191
  Trophy Points: 280
  Watanzania wavunja rekodi ya uzalendo Afrika

  Imeandikwa na Na Joseph Lugendo | HabariLeo | Tarehe: 28th November 2009

  TANZANIA imeweka rekodi ya aina yake barani Afrika kwa kuibuka nchi pekee yenye wananchi wenye mapenzi makubwa kwa taifa lao kuliko jambo au mfumo wowote wa kitamaduni, kiuchumi au kijamii unaowagawa katika makundi mbalimbali na matabaka.

  Rekodi hiyo ambayo ni moja ya kigezo cha nchi iliyo na ulinzi imara, imepatikana baada ya wananchi wa nchi za Afrika, wakiwemo Watanzania, kufanyiwa mahojiano maalumu kuhusu jambo la fahari wanalodhani ni muhimu kujitambulisha nalo kati ya mambo kadha wa kadha yanayotumika kumtambulisha mwanadamu.

  Vigezo vingine vinavyoifanya nchi kuwa na ulinzi imara na madhubuti licha ya uzalendo wa wananchi wake kulipenda taifa lao ni teknolojia ya vita, ushirikiano mzuri na nchi marafiki zikiwemo nchi jirani, wingi wa wanajeshi, bajeti inayotumika kwa ajili ya ulinzi na usalama na idadi ya watu.

  Katika mahojiano hayo yaliyohusisha wananchi kati ya 1,200 na 2,400 katika kila nchi kati ya nchi 16 zilizochaguliwa kufanya utafiti kuhusu ujenzi wa taifa katika nchi za Afrika, wananchi waliulizwa maswali ili kubaini iwapo wanajisikia fahari zaidi kutambulishwa kwa jina la taifa lao kwa mfano Mtanzania, au kwa jina la kitu kingine haswa kabila.

  Kwa mujibu wa maoni ya utafiti huo uliofanywa na taasisi ya kimataifa ya utafiti ya Afro Barometer yenye makao makuu nchini Ghana na kuongozwa na Amanda Lea Robinson wa Chuo Kikuu cha Stanford, Marekani ulionesha kuwa waliojisikia fahari kutambuliwa kwa mataifa yao zaidi ya kitu kingine ilikuwa asilimia 42 ya wahojiwa wote wanaofikia 22,765.

  Robinson ambaye ni mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Idara ya Sayansi ya Siasa ya Stanford University anasema katika utafiti huo uliotolewa Septemba mwaka huu kwamba wakati wastani wa wanaopenda mataifa yao katika nchi hizo ni asilimia 42 ya wahojiwa, kwa Tanzania wanaolipenda taifa lao ni asilimia 88 ya wahojiwa wote.

  Nchi ya pili kwa kuwa na wananchi wanaopenda taifa lao kuliko kabila ilikuwa Afrika Kusini ambayo asilimia 63 ya wananchi wake wanalipenda taifa lao kuliko kabila, ya tatu Namibia ambayo wiki hii ilikuwa katika mchakato wa uchaguzi wa Rais.

  Namibia wao ni asilimia 57. Nchi ya nne ni Senegal asilimia 51 na ya tano Madagascar, asilimia 50. Nigeria imekuwa ya mwisho kwa kuwa na asilimia 17 tu ya wananchi wake wanaolipenda taifa lao kuliko kabila.

  Katika nchi za Afrika Mashariki zilizoteuliwa katika utafiti huo, Kenya ilishika nafasi ya nane kwa kuwa na asilimia 40 ya wananchi ambao wanalipenda zaidi taifa kuliko kabila lao na Uganda ilishika nafasi ya 12 ikiwa na asilimia 31 tu ya wananchi wake wanaopenda taifa lao zaidi ya kabila lao.

  Msomi huyo anasema kabla ya kuanza kwa utafiti huo ambao ni wa kwanza kufanya uchunguzi wa harakati za ujenzi wa taifa katika nchi za Afrika, alitumia nadharia kadhaa za ujenzi wa taifa zikiwemo zinazoelezea ujenzi wa mataifa ya Ulaya na zilizokuwa zikionesha kuwa mataifa ya Afrika ni dhaifu kutokana na wananchi wake kupenda zaidi makabila yao kuliko taifa lao.

  Moja ya nadharia hizo ilikuwa ikijaribu kuoanisha ujenzi wa taifa katika nchi za Ulaya ambazo wananchi wake wanajitambua zaidi kwa utaifa wao na ujenzi wa taifa katika nchi za Afrika ambazo zimekuwa zikitazamwa kuwa hazijafanikiwa kujenga utaifa kwa wananchi wao kama zilivyo za Ulaya.

  Kutokana na nadharia hizo alifanya utafiti wa makabila na kuandaa orodha ya makabila zaidi ya 200 aliyodhani kuwa yangewakilisha taarifa za makabila mengine katika nchi husika ili kufanikisha utafiti wake.

  Robinson anabainisha kuwa katika nchi zote 16 ambazo utafiti huo ulifanyika, asilimia 95 ya wahojiwa walitambua kabila lao lililokuwa katika orodha yake na hivyo alifanikiwa kupata taarifa za tabia ya kabila husika ikiwemo ukubwa na uwezo wa kiuchumi wa kabila ili kuhusisha mchango wa kabila husika na mapenzi ya wananchi fulani katika taifa lao.

  Anasema japo katika utafiti huo asilimia 95 ya wahojiwa katika nchi hizo 16 walitambua makabila yao katika orodha ya makabila iliyokuwa imeandaliwa kabla ya kuanza kwa utafiti huo, walipofika Tanzania walishangazwa kukuta asilimia 60 ya wahojiwa wakisema kuwa kabila lao halipo katika orodha hiyo.

  Kutokana na kuwepo idadi kubwa ya wahojiwa Watanzania ambao walisema kuwa kabila lao halipo katika orodha yake ya makabila, msomi huyo anaeleza kuwa alishindwa kufanya uchambuzi wa mchango wa kabila katika mapenzi ya wananchi kwa taifa lao.


  Hata hivyo anabainisha kuwa Watanzania ambao makabila yao yalikuwepo katika orodha na ambao makabila yao hayakuwepo katika orodha wote walipoulizwa iwapo kati ya taifa lao na kabila lao nini wanaona fahari kutambulishwa nacho, asilimia 88 walisema wanaona fahari kutambulishwa na Taifa lao.

  "Tanzania ni ya pekee, ambapo asilimia 88 wanaelezea kulipenda zaidi taifa lao, hata wale ambao kabila lao lilikuwepo katika orodha asilimia 87 walisema wanajisikia fahari kutambulishwa kwa taifa lao," alieleza msomi huyo katika utafiti wake huo.

  Utafiti huo ambao ulihoji watu wenye umri wa kupiga kura tu, pia ulibainisha kuwa wakati mataifa yaliyotawaliwa na Uingereza na ambayo yalipata uhuru kwa njia ya amani, wananchi wake walionekana kuwa na fahari sana na makabila yao, bado Tanzania ambayo iliwahi kuwa chini ya uangalizi wa Uingereza kwa kipindi kirefu na ilipata uhuru kwa njia ya amani ilionekana kuwa taifa linapendwa kuliko kabila.

  Kutokana na matokeo hayo, msomi huyo ameitaja Tanzania kama nchi yenye wananchi wanaolipenda zaidi taifa lao na ameshauri kuwa nadharia zilizopo za ujenzi wa taifa katika nchi za Afrika hazifanyi kazi kwa Tanzania labda kama kutakuwa na nadharia nyingine.

  Alifafanua kuwa mapenzi hayo kwa taifa yanaweka mazingira mazuri ya kukua kwa demokrasia kwa kuwa mtu hatazuiwa haki yake ya kuchaguliwa kwa kigezo cha kuwepo katika kikundi fulani ambayo pia itachangia kukua kwa uchumi na maendeleo ya watu.
   
 2. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Proud of my country and my people. Proud Tanzanian
   
 3. l

  libaba PM Senior Member

  #3
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mdini mkubwa weeh, huwezi kuipenda nchi yenye mchanganyiko wa watu, umejaa fitina za kidini
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,610
  Likes Received: 82,191
  Trophy Points: 280
  Matunda ya Mwalimu hayo. Hawa Mafisadi baada yake sidhani kama wangetufanya tujivunie Utanzania wetu kiasi hiki.
   
 5. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mbona hueleweki ndg?udini hapa unatoka wapi?je mdini ni yule anayeipenda Tz pamoja na tofauti ya makundi yote ya watu yaliyopo kidini,kikabila na vinginevyo?
   
 6. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2012
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Siku zote naingia hapa naangalia na kusoma comments sitaki kupost lakini nimelazimika kupost hii post kwa kuwa naipenda nchi yangu.

  Wasilamu wenzangu, hii sio JIHAD, tafuteni characteristics za JIHAD mtagundua kuwa mnachofanya sasa hivi sio JIHAD na haitakuwa JIHAD, kwanini mnatukanisha dini yetu namna hii? Dini yetu ni ya amani kabisa kabisa na haikubali mtu kufanya vurugu

  Mnafanya waisalamu tuone haibu mbele ya wenyekitabu kwa kuwa mnafanya vurungu zisizo na msingi, ni kifungu gani cha Quran kinachosema mwislam akose busara na kufikiri kabla ya kutenda.

  Ili tuendelee kwenda msikitini kwa amani na kumwabudu M/mungu tunahitaji amani. Nawaomba kuweni kuweni wavumilivu ili tuweze kumwabudu M/mungu
   
 7. K

  KIRUMO JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2012
  Joined: Sep 25, 2012
  Messages: 364
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HIVI NI KWELI KUWA iSLAM NI DINI YA AMANI?
   
 8. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2012
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hawa ni wahuni tu wanadhalilisha dini yetu tukufu, hakuna kipengele kinachosema wafanya vurugu kwenye Quran.

  Bedul alikojoa msikitini lakini Mtume Mohamed AS aliwakataza waislam kumpiga kwa kuwa haikuwa busara, sasa kwanini hawa wapuuzi hawachukui hiyo hadithi kama mfano?

  Mimi ni islam lakini sikubaliano nao hata kidogo
   
 9. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  kwanini usianzishe jihad nao basi?Na hii nafasi mlikuwa nayo siku zote wakati wakiwahamasisha hadi waislam wote kwa kiasi fulani wapo sympathetic na hawa akina ponda kuliko waliochomea makanisa na kuwafanya washindwe muabudu Mungu wao ambao sijui kwa akili timamu au ukichaa mnasema ndie huyu huyo mnaomubudu.

  Tunahitaji zaidi tunahitaji nyie mkaonyeshe hizo ghdhabu zenu za kubeep mnatishia nazo watu kwa vitu dhaifu.Na si msubiri jasho zetu tulizochangisha kwa uchungu ili tuweze Abudu Mungu wetu ndipo mtuletee habari zenu za jando hapa.Mnatuahditihia sisi kuwa ni wachache wanawachafulia kwanini musiwawajibishe huko huko?Ngoma zenu mnataka sisi tuzigaramie.

  Napata hasira kusikia waislama vimeo wanakuja tuliza watu kwa blah blah hizi ambazo hata mtoto mdogo kaweza thibitisha kuwa ni upuuzi tuu wananunua waislam.Au ndio malipizi ya mungu wenu kwa Mungu wa kweli,kumchomea huyo Mungu wa majini jehanum?
   
 10. D

  Dr.Who Senior Member

  #10
  Oct 20, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mkuu; Uislam ni dini ya amani, lakini pia haikubali dhulma na jihadi nilazima pale inapoonekana haki haifuatwi, nivizuri uelewe waislam wanacho pambana nacho ni dhulma na kwa taarifa yako bado hawaja tangaza jihadi, bali wametangaza maandamano ya amani kwa kutaka masheikh waliokuwa kidnaped waachiwe

  Nakama wewe kweli ni muislam usingeona aibu bali ungeendelea kudai haki.
   
Loading...