Tanzania: Taifa linalotegemewa kuendelea likiwa n miundombinu yote mibovu na legelege | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania: Taifa linalotegemewa kuendelea likiwa n miundombinu yote mibovu na legelege

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kasheshe, Jan 18, 2009.

 1. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Watanzania wenzangu,

  Baada ya kufuatia kwa ukaribu ziara ya Mh. Rais kwenye mashirika yalio chini ya wizara ya Miundo Mbinu nimeng'amua kwamba kelele zote tunazipiga siku zote, msingi wake mkuu uko kwenye mashirika ambayo mheshimiwa Rais ameyatembelea hivi karibuni na mengine machache lakini ya miundombinu (infrastructure)... mliotembelea mataifa mengi nitapenda baadaye munipe mfano wa Taifa lililoendelea bila kuwa na miundo mbinu imara.

  Kama kawaida yangu, najinyooshea kidole mwenyewe na waTanzania wote sio Mh. Rais, Mh. Waziri au Mh. Waziri wa Miundo Mbinu mwenyewe...

  Hivi tujiulize, unaweza kuendelea hali ya kuwa nchi yako ina:-

  1. Bandari yako ina performance ya chini kabisa may be 20%, kumbuka hii ni dhahabu isiyo hitaji kuchimba, inahitaji umakini tu basi.
  2. Shirika lako la Reli limekufa, huwezi kusafirisha mizigo mikubwa (bulk cargo) kwa gharama nafuu.
  3. Barabara zako mbovu zikiwa pamoja na za Dar es Salaam, ambapo kila mtu anapoteza at least masaa mawili ya kufanya kazi barabarani.
  4. Shirika lako la ndege (ATCL)limekufa, unaua utalii etc.
  5. Shirika lako la umeme (TANESCO) linafanya kazi Mungu saidia...
  6. Shirika lako la Telecommunication (BackBone) linasuasua yaani TTCL, wanajua ICT wanaelewa, mashirika mengine yote ni ya ugawaji huduma kwenda kwa mtumiaji wa mwisho... lakini shirika la mkongo mkuu (TTCL) liko mahututi.
  7. TPDC; huwezi kuweka petrol ya akiba ya siku tano, ambayo ingeweza ku-cover ukosefu wa mafuta kwa sababu yoyote kama iliyotokea juzi juzi.

  Wandugu hakuna chama, malaika au yeyote yule atakayekuja Tanzania akatuambia atafanya Tanzania uchumi ukue kama mashirika ya miundombinu yataendelea kuwa kwenye hali hiyo.

  Binafsi sitamsikilikiliza mwanasiasa yeyote yule ikiwepo wanaopiga makelele ya EPA kwamba ni wazuri mpaka wanieleze ni lini mashirika hayo hapo juu ya miundo mbinu yatafanya kazi kwa ufanisi wa at least 60% and above.

  Hayo mashirika yakifanya kazi kwa asilimia kubwa tutaweza kuamsha kilimo, tutaweza kujenga shule, zahanati, vyuo na huduma zote za Jamii.

  Ndio utaweza kuzungumzia mdudu anaitwa utawala bora, demokrasia na... politics nyingi za kina Lipumba, Mrema, Mbatia etc.

  Ukiniuliza sasa kwa nini Tanzania ni maskini?

  Nitakuambia kwa kuwa miundombinu yote imekufa... kwenye mwili wa binadamu mshipa wa AOTA haupampu damu vizuri, yet unategemea uweze kukimbia marathoni...lazima uta-collapse: na kweli uchumi wa Taifa ume-collapse.

  Vipaumbele: Kama yawezekana Bandari ingehakikishwa inafanya kazi hata kama italazimika kuweka JKT au JWTZ wafanye hiyo kazi.

  NB: Naomba kuelezwa National Development Corporation (NDC) linafanya kazi gani?

  Mungu Ibariki Tanzania.
  Ahsante kwa kunisoma
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Umesema kweli Kasheshe, tatizo letu ni maneno bila vitendo. Wakenya bandari yao japo nayo huwa inafurika ila wanajitahidi. Imefikia wakati hata waTZ wanaingizia mizigo yao bandari ya Mombasa badala ya Dar. Sasa hao ni wa TZ tu, acha nchi nyingine zisizo na bandari kama Uganda, Rwanda, Burundi nk. Tunajikosesha mapato (kodi) kwa uzembe wetu wenyewe.
   
 3. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwanini wasifanye bandari 24hrs with kitengo kidogo cha jeshi for security during those night shifts kama mwaka angalau while they restructure??? maoni tuu
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Bandari, reli na shirika la ndege vitaimarika tukiacha kufanya siasa katika maeneo hayo. Tutafute watu competent wanaoweza ku-run vitu hivyo kibiashara
   
 5. UramboTabora

  UramboTabora Member

  #5
  Jan 22, 2009
  Joined: Sep 11, 2008
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MOJA ya habari zilizomo katika ukurasa wa tatu wa gazeti la Tanzania Daima ni agizo la Rais Jakaya Kikwete kwa viongozi wa Shirika la Ndege (ATCL), kuwataka kurejesha huduma baada ya kusimama kwa takriban mwezi mmoja sasa.

  Rais Kikwete ameonyesha kukerwa na kutokuwapo kwa huduma hiyo kiasi cha kuweka bayana kuwa taifa linapoteza fedha nyingi kutokana na kutorusha ndege.

  Tunaamini agizo hilo la Rais Kikwete litafanyiwa kazi muda si mrefu, kwani taifa linahitaji kuwa na miundombinu imara, hasa ya usafiri ili kuchochea ukuaji wa uchumi, sambamba na kuwavutia wawekezaji.

  Agizo hilo la rais limekuja siku mbili baada ya kuagiza uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) kuacha kufanya maamuzi mazito bila kuishirikisha serikali ambayo ina hisa ya asilimia 49.

  Lakini kabla ya kukutana na viongozi wa TRL, Rais Kikwete alionana na viongozi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) na Kampuni ya kuondoa makontena bandarini (TICTS), akiwataka waboreshe utendaji wao.

  Tunaunga mkono ziara hizi za Rais Kikwete lakini ni lazima kuwepo na mabadiliko katika sekata husika badala ya maagizo ya rais kubakia kwenye makaratasi.

  Ni aibu kwa taifa kwa kutokuwa na huduma bora bandarini, huduma za reli na ndege, ambazo zote kwa kiasi kikubwa ndiyo uti wa mgongo wa ukuaji wa uchumi.

  Baadhi ya wafanyabiashara wamekwisha kuikimbia Bandari ya Dar es Salaam na kuitumia ya Mombasa, huku wengine nao wakizitumia ndege za kampuni binafsi kwa shughuli zao.

  Lakini pamoja na maagizo hayo ya rais, ni vema serikali ikaangalia kwa makini sababu na vikwazo inavyokumbana navyo na ikiwezekana itoe msaada ili kuwakwamua.

  Kama serikali haitawasaidia kimtaji na utaalamu, hata Rais Kikwete atoe maagizo makali kiasi gain, mambo hayatabadilika.

  Tunaamini bado kuna nafasi nzuri ya kurekebisha makosa yote yaliyotokea kipindi cha nyuma na hatimaye kujenga taifa lenye mwelekeo mzuri wa kiuchumi.

  Tunajua tulifanya makosa kwenye baadhi ya sekta kwa kuwapa wawekezaji wasio na mitaji ya kutosha na utaalamu, lakini ni vema tukawa wakali ili watuheshimu.

  Ukali wa Rais Kikwete kwa wawekezaji, hasa wanaopenda kufanya mambo kinyume na mikataba yao, utasaidia kwa kiasi kikubwa kuwarejesha wawekezaji hao kwenye msitari unaotakiwa.

  Huu si wakati wa kubabaishwa na wawekezaji na wala si wakati wa kurudia makosa yaliyofanyika huko nyuma.

  Ndiyo maana tunaiomba serikali sasa iwe zamu ya vitendo zaidi kuliko maneno ili nchi iondokane na uchumi dhaifu na maisha magumu kwa wananchi.

  Mwageni maoni yenu waungwana
   
 6. Modereta

  Modereta Senior Member

  #6
  Jan 22, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  TUTOE HOJA HAPA SERIKALI IFANYE NINI??????????????????
  Hakuna nchi inaendelea bila miundo mbinu na viungo vyake, yaani NISHATI, MAJI NA USAFIRI (Barabara, bandari, anga na reli) bandari na reli ni njia muhimu za usafirishaji wa gharama nafuu, hasa za mizigo mikubwa, hivyo
  - bila reli mizigo yote iendayo bara itakuwa bei ghali na mengine mengi.
  - bila nishati kama umeme nafuu (sio majenereta ya mafuta au gesi ghali) bei ya bidhaa ni mbaya utashindana vipi na bidhaa toka nje?
  - bila barabara nzuri usafirishaji wa mizigo na watu inakuwa kasheshe, ndio maana nauli ya basi toka dar mpaka morogoro (kilimeta 200) ni ndogo kuliko nauli toka mikumi mpaka ifakara kilomita 100 tu.
  - bandari ya Rotterdam inasafirisha mizigo haraka na kwa urahisi, ndio maana gharama ya usafiri toka luanda kuja dar ni kubwa kuliko toka rotterdam kuja dar.

  Hivyo maendeleo yatakuja haraka kama MIUNDO MBINU ITAKUZWA.
   
 7. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Umesahau kuwa hatuna barabara, kuanzia mjini hadi vijijini.

  Kama inavyosemekana kuwa nchi yetu inategemea Kilimo kiuchumi (Ref John Mashaka), haya mazao yatafikaye kwenye masoko bila kuwa na barabara zua uhakika. Ndizi zitaozea pale Mbingu, nafaka zitanunuliwa kwa bei chei na walanguzi ambao wanasacrifice magari yao kwenda vijijini kupitia hizo barabara mbovu....list ni ndefu.

  Pamoja na kufikiria kuwa na ndege, meli; umuhimu wa kuwa barabara za uhakika zinazopitika majira yote ya mwaka upewe kipaumbele. Ni muhimu kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja kuanzia wakulima vijijini hadi wachuuzi mijini na hatimaye kusababisha ukuaji wa uchumi wa nchi kwa ujumla.
   
 8. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hii ipo kwenye thread ambayo nilishaanzisha... "Tanzania: taifa linalotegemea kuendelea wakati likiwa na miundo mbinu mibovu na legelege"
   
Loading...