Kwa muda mrefu sasa, Tanzania imekuwa Taifa la siasa na wanasiasa! Kila jambo ni siasa na kila mtu ni mwanasiasa! Taaluma na wanataaluma wanawekwa kando au wenyewe wanaweka kando taaluma zao ili kuenzi siasa, kwani siasa inalipa zaidi! Wanaopata nafasi za kisiasa ndio wanaofaidi zaidi matunda ya nchi!
Tumepata Raisi mwanataaluma, natamani atambue thamani na nafasi ya taaluma kwa ustawi wa jamii yoyote ile ili ageuze huu mwelekeo! Hatutaweza kufikia maendeleo tuliyokusudia bila kufanyia mabadiliko ya dhati kwenye mwelekeo huu!