Tanzania Society for Prevention of Cruelity to Animals

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,986
2,000
Tanzania Society for Prevention of Cruelity to Animals ni chama ambacho kinanatakiwa kuzuia aina yoyote ya ukatili wanaofanyiwa wanyama, lakini katika halo ya ajabu chama hiki muhimu kinaonekana kimekufa.

Tunashuhudia kila aina ya ukatili wakifanyiwa wanyama bila hatua zozote kuchukuliwa na mbaya zaidi ukatili mwingine hufanywa na vyombo vya dola!

Kwa Mara nyingine tutashuhudia vifaranga vya kuku vikichomwa moto na watu wazima kwenye skili timamu!

Watu hawa kwa ukatili wao watahakikisha kila kifaranga kitakachojaribu kujiokoa kinarudishwa kwenye moto bila kuchinjwa kwanza! Huu ni ukatili wa halo ya juu sana na haukubaliki kwenye dunia ya wastaarabu.

Watanzania tupinge ukatili huu kwa kigezo cha sheria.
 

THE BROKER

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
371
500
Labda tunavyozungumza Sasa wameshavichoma maana kumbuka Ni gharama Sana kuvilisha toka juzi. So sad, RIP vifaranga karibu uhasama na nchi jirani.
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
56,265
2,000
Utawachomaje wanyama dah

Wanachomwa kama enzi za holocaust za
Wanazi

Ova
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom