Ninja
JF-Expert Member
- Feb 5, 2010
- 353
- 543
Kuna dhana kwamba Afrika, kiongozi anaweza kufanya lolote analotaka ikiwemo kutukana watu ovyo, kuvunja katiba na kujitangazia uungu huku akiendelea kutawala bila kubugudhiwa. Dhana hii ipo hasa kwa kuzingatia kuwa kuna kiongozi mmoja huko Zimbabwe amewahi kusababisha nchi iporomoke vibaya kiuchumi na bado amefanikiwa kung'ang'ania madarakani.
Kuna watu wanadhani kuwa jambo hili pia linaweza likatokea Tanzania. Wako wanaothubutu kusema kuwa watanzania ni waoga na ni mandondocha.
Tahadhari kwenu viongozi wetu. Tanzania sio Zimbabwe. Huko mnakokwenda siko na mnatakiwa mgeuke haraka sana.
Kumbukeni kipenzi cha Taifa hili, baba wa Taifa alikumbana na majaribio mangapi ya kung'olewa? halafu bado mnadhani hapa ni Zimbabwe!!???
Sasa mjifanye miungu na kudhani kuwa watanzania ni mandondocha, msiseme hamkuonywa!