Tanzania siamini kama tutapata kiongozi mzalendo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania siamini kama tutapata kiongozi mzalendo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by zoea, Dec 29, 2011.

?

Lini na nani viongozi wazalendo tutawapata TZ?

 1. AFTER 7 DAYS

  100.0%
 2. AFTER ONE MONTH

  0 vote(s)
  0.0%
 3. AFTER 1 YEAR

  0 vote(s)
  0.0%
 1. z

  zoea Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado siamini kama Afrika hasa tz tutakuja pata viongozi wazalendo,hii ni kwa sababu wote wanapopewa ridhaa husahau raia na kuweka maslahi yao mbele,wanapenda sn sifa,utajiri,nk.nashuri kuwe na strictly rule of law,na raisi asiwe na madaraka ya kuteua viongozi mhimu kwani inapelekea kufanya kazi kwa interest zake au chama.kiongozi akivunja sheria ahukumiwe kama raia wa kawaida kama misri.
   
 2. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #2
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Ni ajabu saana kua mara nyingi wananchi hua twalalama kua hatuna viongozi wazalendo....Wananchi wenyewe hatuko wazalendo... Ikumbukwe kua viongozi hutoka katika hii hii jamii yetu, na jamii yetu ukiiangalia kwa ukaribu saana wananchi tu wabinafsi saana. Wale ambao ni wadau na wakereketwa wa Siasa ni aidha sababu ni wa chama pinzani, ama sababu tu ni mashabiki, ama sababu maisha yanamtandika but ni mara chache hua sababu ya Uzalendo. Uzalendo Tanzania ni mtihani... Wananchi tulo wengi hatuko wazalendo na hilo ndio lapelekea kupata viongozi ambao si wazalendo katika kila nyanja, iwe ba Boss kazini, viongozi wa vitongoji hadi ngazi za juu....
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  hata wewe unajitoa?
   
 4. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kama tutaendelea kutukana badala ya kujenga hoja uzalendo utatoka wapi? Tatizo tunafikri kwamba viongozi tu ndio wanatakiwa kuwa wazelendo
   
 5. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Uzalendo hujengwa hata hapa JF tuna fursa ya kuubomoa au kuujenga. pima nguvu ya hoja kisha hitimisha kama tunashirki kujenga au kubomoa zaidi
   
 6. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  JK ni Rais wa muda awamu yake itapita lakini kuna watu humu wanataka kwa miaka minne ijayo kabla hajaondoka tuzungumze kuhusu yeye na kuacha kujenga nchi. mpumbafu atakuwa Jk au sisi ambao hatuzungumzi kitaasisi tunazungumzia watu ambao kimsingi wanapita lakini taasisi zitaendelea kuwepo.
   
 7. z

  zoea Member

  #7
  Dec 29, 2011
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama jamii yenyewe ndo chanzo tutatumia njia zipi kuleta uzalendo ktk jamii yetu?
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  hata mwanao anaweza kuwa Rais wa nchi siku moja kama hushiriki kujenga uzalendo kwa mwanao usitegemee viongozi ndio watafanya kazi hiyo......Uzalendo huzaliwa, hulelewa na kukua kabla ya kufa kama hakuna jitihada za kila mmoja wetu kuingiza nguvu yake katika ujenzi huo. hata kama kiongoiz ni mzuri lakini wananchi hawana uzalendo ni bure.
   
 9. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Fuatilia sile brand za BEN 10, CINDILLELLA, ANNA MONTANNA na nyinginezo zilivyo na impact kwa watoto wetu zikitokea nchi za magaharibi. Trade name hizi zimefanyiwa kazi hadi zimepata sura ya dunia. Hivyo ndivyo sote tunatakiwa kushiriki kukuza uzalendo.
   
 10. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Ukitaka kujua kwamba mtu hana uzalendo ni pale anapofikrli kwamba tiba ya uzalendo iko kwa viongozi si kwenye jamii tunayoishi. kiongozi anatoka miongoni mwetu na sisi ndio tutajua kwamba amepikwa vizuri na jamii kwa ajili ya kutuongoza. kama jamii haina uzalendo kamwe tusitegemee kupata viongozi wazalendo. kama tulikosea mahala fulani ni wakati muafaka sasa kujitathmini. kumbuka kiongozi ni tunda la jamii, kama amewiva inategemea jinsi tulivyotoa matunza kwenye mtu wa matunda.
   
 11. z

  zoea Member

  #11
  Dec 29, 2011
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli inabidi tufanye changes kubwa ktk malezi na elimu kwa watoto babo wachanga kujua na kaishi kweli uzalendo pia mifumo ya utawala naona bado ni tatizo.
   
Loading...